Ninawahamasisha wenye magari binafsi kugoma!

Serikali haina tatizo na anayefuata sheria,wala huwezi kupigwa faini kama Gari yako imekamilika kila kitu.
 
Watanzania hawana tamaduni ya kugoma. Sisi watu wa kunyanyaswa milele daima. Trafiki manyanyaso pale pale, msilegeze kamba hadi wayauze magari kwa usumbufu wanaoupata. Trafiki Tanzania oyee!
 
Mzee Mwanakijiji alihamasisha watu wagome kutumia laini za simu kwa kuzichomoa ili kupinga tozo hakufanikiwa, hili lako sijui kama utafanikiwa kwa namna ambavyo watu wamekuwa wagumu kufanya mazoezi
 
Watawapiga bao madereva wa daladala. Njaa ikizidi watakimbilia hadi magari ya mwendokasi. Mentalities zao zishaoza na rushwa
Walivo ma...... watapiga paka gari za fire na ambulance wakikosa kila kitu.
 
Wazo zuri sana...mgomo syo Kwa trafik tu hadi Kwa serikali hauwezi lipia road license na kodi zingine huku unatumia barabara mbovu..

Ova
 
Tuki goma, watahamia kwenye bodaboda, bajaji na daladala pengine mwendokasi.
Na wanaweza kuanza kukamata watembea kwa miguu ,kama umevuka barabara bila kuangalia Kushoto au kulia unapigwa fine hapo hapo.
 
Si ajabu wakakamata pia Ambulance
 
Kama huwezi kutii sheria goma utatusaidia sana madereva watiifu kwasababu wavunja sheria mnatukera hata madereva wenzenu. Btw trafiki hawako perfect huwa wanakosea kama binadamu ila sio kweli kuwa wanasingizia watu wote makosa.

Wabongo mnaujua uendeshaji wenu tuache unafiki.
 
Umeandika hii sababu ya watu kuonewa au kutembea na makosa na hivyo kutishia usalama a wengine barabarani?
 
Poleni kwa manyanyaso mnayoyapata pamoja na kugeuzwa na jeshi la polisi kikosi cha usalama wa bara barani kuwa kitega uchumi kipya na chanzo chao cha kuongezea mapato na kujipatia sifa.
'These people have made u fool of theirs and now its your time to make them fool of themselves'.
'They have shown us who they are and now its our time to show them who we are'. ..
Nawahamasisha myapaki magari yenu nyumbani kwa mda wa wiki moja au mbili hivi na muwe mnayaendesha nyakati za usiku ili tuone watakamata nini.
Hakuna haki inayokuja kirahisi.. Wacheni bara bara nyeupe polisi waweke magari yao.. Mkiwachekea mishahara yenu itaishia kwenye fine huku watoto wenu wanakufa njaa.
Kwani tatizo nini hapa kiongozi?
 
Kweli unawaletetea hao watu!!?
Siwatetei Wana usalama barabarani,najua kuwa wanatimiza matakwa ya sheria.

Na kama kila kitu Kiko sawa hautapigwa faini.

Na ukisoma ile sheria vizuri na wana usalama wakisema wasimamie yote kama sheria inavyotaka nadhani yatatembea magari machache sana barabarani.

Wamekuwa wana angalia vitu vya msingi zaidi ili maisha yaende otherwise makosa ya faini ktk Gari ni mengi sana.
 
Mkuu hivi kweli mtu anatalalamika bila kosa, kwa kuwa watanzania tunapenda kulalamika au? Mkuu wewe ni mmoja wao au? Unaambiwa "mwendo kasi baada ya 50 ndefu, speed 59" umeongozana na gari nyingine yupo mbele yako tena sio ati unataka kumpita hapana, kama wa Nyuma Ana 59 wa mbele Ana ngapi? Na tumemkuta kasimamishwa tunafika sisi anaruhusiwa kwamba hana makosa wenye makosa ni sisi picha imepigwa kwa Nyuma, labda hatujui sheria basi watoe somo tueleweshwe. Bila kutoa elimu tutawalaumu kila siku. unatetea!?
 
Waliokuwepo eneo la tukio ndiyo wanaweza kuwa na majibu sahihi.

Najua barabarani siyo magari yote yanasimamishwa,na siyo yote yanapigwa tochi ya speed na huwezi kukadiria speed zaidi ya kusema ulikuwa speed kubwa sana,wastani au pole pole.

Yawezekana wa mbele yenu alisimamishwa kwa mambo mengine na hakupigwa tochi ila nyie ndiyo mlipigwa tochi ya speed.
 
Back
Top Bottom