Ninavyowafahamu wateule wapya wa Rais Samia kwa historia yao ya nyuma na uhusiano wao na viongozi wa leo

mtifuano- tayari team mbili kati ya zile tatu zimeungana kupinga uteuzi, na kila team ina sababu zake binafsi za kupinga.
Ushauri wangu kwa mama SSH apige kazi bila kuzijali hizi team kwani kuna wakati zinajiunga nae automatically na kumdiss automatically.

Kwa sisi wazalendo tunasema kazi iendelee
Pamoja sana ndugu. Kazi iendelee!
 
Uchambuzi wako kwa kiasi kikubwa nakubaliana nao. Tunarudi pale pale. Hata tubadilishe marais namna gani kila mmoja anayeingia akifanya uteuzi, ni lazima uegee kwenye mapenzi yake kwa wateuliwa zaidi kuliko uwezo wao. Tunarudi kule kule. Bila kufumua system na kuhakikisha rais hafanyi uteuzi kwa kutumia ''mahaba'' badala ya ''uwezo'' hakuna kipya.
Ukisha dhibiti bunge hata nabii tito unawaza mpa uwaziri na akaonekana genius
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Umenena kweli nilipata nafasi ya kuongea na rais mmoja miongoni mwa wastaafu alipotutembelea katika taasisi yetu.
Alisema na hapa namnukuu:
nilipokwenda Uingereza wazari mkuu aliniuliza je rais unao watu wako wa karibu katika baraza la mawiri? Nikasema ndiyo sisi wote ni watanzania akasema hapana lazima uchaguwe watu wako wa karibu.
Hasa katika wizara nyeti ndivyo nafanya mimi na nchi zote kubwa unaziona. Mwisho wa kunukuu.
Hasa USA hilo huwa ni la muhimu sana.
 
Uchambuzi wako
Wote walioteuliwa wanafahamika kwa sura na kwa tabia. Sababu za kuteuliwa kwao ndo vigumu kuzitambua. Hapa nitajaribu kuzitaja kadri ninavyowafahamu.

Tuanze na Stergomena Tax
Huyu ni mtu mwenye elimu nzuri, mwanamke ambaye ktk wengi walioko baraza, hatuna wanawake wenye uwezo. Ana matatizo yake ya elimu ya u-daktari lakini haina shida. Tutegemee atumie Masters yake na siyo Ph.D uonayo kwenye jina. Kwa tamaa ya kuwa na akina mama, ameweza kuuzika kiurahisi kwa wizara ambayo kazi yake ni kusoma bajeti tu!

Ashantu Kijaji
Ni msomi, aliyeanzia kwenye akademia. Akiwa naibu waziri hakufanya vibaya na ana tabia ya kupenda maendeleo ktk jimbo lake sana, kwa kuwasikitikia viongozi wa serikali wasiojali maisha ya walio chini. Ni kiongozi mzuri ambaye haijulikani ni kwa nini hakupanda baada ya kuwa Naibu wa wizara ya fedha. Akiwa mwanamama, anastahili kujaribiwa.

Januari Makamba
Ana uwezo mdogo ambao hufichwa na ushujaa wake wa ku-pozi kama mwerevu. Hakustahili kuingia tena ktk baraza, lakini kuna nguvu kubwa ya urafiki. Ni misheni tauni sana na nasaha za internet kwa wingi ili aonekane ni msomi. wapo akina Rostam, wanufaika wa wizara yake na bado wanapenda kunufaika. Yupo na mstaafu JK anayemkumbuka kwa kuamini atapanda kulinda maslahi yake. Nishati ni wizara ambayo inawanufaisha watu kupitia umeme migodini, mafuta, na vituo vya hovyo hovyo na ukwepaji kodi ktk sekta hii. Ameingizwa ili kazi iendelee. Tutalizwa tu!

Makame Mbarawa
Ni waziri wa kuteuliwa miaka mingi, akitokea Pemba ambako CCM kwao ni ndoto kushinda kihalali. Amekuwa akiteuliwa ili kulinda nafasi ya Pemba. Alikuwa waziri mzuri kwa misingi yake ya kutokea akademia. Tatizo lake alijiingiza kwenye rushwa za wizara ya maji na akaanza kutafuta pesa alizoziita za uchaguzi, akifahamu Pemba hawezi pita. Naamini ameingizwa kwa msimamo wa rais kuinua kuonekana kwa Z’bar pamoja na kwamba uaminifu wake ulishaingia doa.

Eliezer Feleshi na Adelardus Kilangi
Hawa wamekuwa ktk mkanganyiko sana lakini Kilangi tangu alipoingia alikuwa ni mtu ambaye ni kama alibebwa saana bila kujali uwezo wake. Badala yake tukaambiwa sijui anaaminika wapi na wapi lakini msingi wake ktk sheria na hata sifa ya profesa haina msingi wa kuaminika.

Feleshi simfahamu sana ktk mambo yake ya kiofisi. Je ni uzoefu wake wa kunyamazia maovu ktk awamu ya 4? Kama ni hivyo basi naye kaingizwa kwa mtindo wa kazi iendelee. Tutapigwa hadi nchi ichakae.
Uchambuzi wako hupo deep sana.Umenifanya nitoe machozi.Na nione kuwa ,Tanzania hatuwezi kusonga mbele.Mama ameishiwa tayari.Ambao walishawahi kuwa mawaziri na kufeli ,wanarudishwa.Je, nn kiliwaondoa na nn kimewarudisha?Je, katika watanzania million 60 hakuna wengine?Je,January Makamba ana kitu gani cha maana mpaka arudishwe kuwa waziri?Je,Prof Makame ana nn cha maana mpaka arudishwe kuwa waziri?Tanzania tupo kwenye break even point .CCM imechoka kabisa .Wapinzani pia wamechoka kabisa.Tutafute watu tofauti waunde vyama ili tuwaondoe CCM .Mama alitupa matumaini mwanzoni kuwa mtanzania yeyote anaweza kupata nafasi serikalini.Lakini naona ,mama amechoka.Hana jipya.
 
Tukifanikiwa kuandika Katiba mpya na bora kwa kila mtu tutafika mahali tutajishangaa na kujiuliza tulichelewa kwa nini?
 
JPM alijaribu kuharibu hizi circle za madaraka kwa kuleta walau akili mpya lakini sasa tunarudishwa mule mule tena kwa lazima.

Ina maana hii nchi hakuna brain nyingine za kuongoza hadi turudie makosa haya haya kila mwaka?
Magufuli???hakukuwa na rais mule,ule ulikuwa mzigo ambao taifa hili lisingeuweza kuubeba,usiombe uwe na raisi fisadikteta utaimba haleluya.
 
January Makamba miongoni mwa wanasiasa wenye IQ kubwa ndo maana sikushangaa kuwa na urafiki mkubwa na Ruge RIP kwani ndege wafananao huruka pamoja sitoshangaa akija kuwa rais wetu hapo badae
January Makamba ni hana huo uwezo unaosema chief anatembelea nyota tu tangu enzi ...
 
Uchambuzi wako kwa kiasi kikubwa nakubaliana nao. Tunarudi pale pale. Hata tubadilishe marais namna gani kila mmoja anayeingia akifanya uteuzi, ni lazima uegee kwenye mapenzi yake kwa wateuliwa zaidi kuliko uwezo wao. Tunarudi kule kule. Bila kufumua system na kuhakikisha rais hafanyi uteuzi kwa kutumia ''mahaba'' badala ya ''uwezo'' hakuna kipya.
Nyie watu mnaotaka system ifumuliwe, mnataka nani atuongoze? Mbowe?
 
mtifuano- tayari team mbili kati ya zile tatu zimeungana kupinga uteuzi, na kila team ina sababu zake binafsi za kupinga.
Ushauri wangu kwa mama SSH apige kazi bila kuzijali hizi team kwani kuna wakati zinajiunga nae automatically na kumdiss automatically.

Kwa sisi wazalendo tunasema kazi iendelee
CCM ni powerful kuliko yeyote, Kama Lowasa na Rostam waliishindwa hamna yeyote anaweza kupambana nayo siku za karibuni
 
Mimi nawaonea huruma wakina mabeyo wanawapigia saluti wakina mama tu!

Halafu karibu wizara zote muhimu zipo chini ya wakina mama!
 
Wote walioteuliwa wanafahamika kwa sura na kwa tabia. Sababu za kuteuliwa kwao ndo vigumu kuzitambua. Hapa nitajaribu kuzitaja kadri ninavyowafahamu.

Tuanze na Stergomena Tax
Huyu ni mtu mwenye elimu nzuri, mwanamke ambaye ktk wengi walioko baraza, hatuna wanawake wenye uwezo. Ana matatizo yake ya elimu ya u-daktari lakini haina shida. Tutegemee atumie Masters yake na siyo Ph.D uonayo kwenye jina. Kwa tamaa ya kuwa na akina mama, ameweza kuuzika kiurahisi kwa wizara ambayo kazi yake ni kusoma bajeti tu!

Ashantu Kijaji
Ni msomi, aliyeanzia kwenye akademia. Akiwa naibu waziri hakufanya vibaya na ana tabia ya kupenda maendeleo ktk jimbo lake sana, kwa kuwasikitikia viongozi wa serikali wasiojali maisha ya walio chini. Ni kiongozi mzuri ambaye haijulikani ni kwa nini hakupanda baada ya kuwa Naibu wa wizara ya fedha. Akiwa mwanamama, anastahili kujaribiwa.

Januari Makamba
Ana uwezo mdogo ambao hufichwa na ushujaa wake wa ku-pozi kama mwerevu. Hakustahili kuingia tena ktk baraza, lakini kuna nguvu kubwa ya urafiki. Ni misheni tauni sana na nasaha za internet kwa wingi ili aonekane ni msomi. wapo akina Rostam, wanufaika wa wizara yake na bado wanapenda kunufaika. Yupo na mstaafu JK anayemkumbuka kwa kuamini atapanda kulinda maslahi yake. Nishati ni wizara ambayo inawanufaisha watu kupitia umeme migodini, mafuta, na vituo vya hovyo hovyo na ukwepaji kodi ktk sekta hii. Ameingizwa ili kazi iendelee. Tutalizwa tu!

Makame Mbarawa
Ni waziri wa kuteuliwa miaka mingi, akitokea Pemba ambako CCM kwao ni ndoto kushinda kihalali. Amekuwa akiteuliwa ili kulinda nafasi ya Pemba. Alikuwa waziri mzuri kwa misingi yake ya kutokea akademia. Tatizo lake alijiingiza kwenye rushwa za wizara ya maji na akaanza kutafuta pesa alizoziita za uchaguzi, akifahamu Pemba hawezi pita. Naamini ameingizwa kwa msimamo wa rais kuinua kuonekana kwa Z’bar pamoja na kwamba uaminifu wake ulishaingia doa.

Eliezer Feleshi na Adelardus Kilangi
Hawa wamekuwa ktk mkanganyiko sana lakini Kilangi tangu alipoingia alikuwa ni mtu ambaye ni kama alibebwa saana bila kujali uwezo wake. Badala yake tukaambiwa sijui anaaminika wapi na wapi lakini msingi wake ktk sheria na hata sifa ya profesa haina msingi wa kuaminika.

Feleshi simfahamu sana ktk mambo yake ya kiofisi. Je ni uzoefu wake wa kunyamazia maovu ktk awamu ya 4? Kama ni hivyo basi naye kaingizwa kwa mtindo wa kazi iendelee. Tutapigwa hadi nchi ichakae.
---tutapigwa hadi nchi ichakae----
 
Sioni shida makamba kurudi kwny baraza.

Hata jpm alianza nae.
shida haipo.

Hata simbachawene au mwigulu walianza kwny awamu ya tano wakaondolewa,
lakini badae walirudi.

Waziri muhongo alilazimishwa kujiuzulu awamu ya 4.

Awamu ya 5 ikamrejesha.baadae kamati ikapendekeza ajiuzulu.
 
Na akitaka kulifahamu Hilo vizuri,,, afuatilie idadi ya wasukuma kwenye system,,, utanikumbuka
kwahyo akiteuliwa msukuma na msukuma mwenzie ni ukabila.

Mbona samia kamteua mbarawa mpemba mwenzie napo tuseme ni unyumbani.

Samia kamteau AG mpya feleshi msukuma.
huo huiti ukabila
 
Hivi ni sharti kila rais akiingia madarakani Mawaziri, RCs na DCs lazima wawe ni watu wale wale wa miaka yote? Kwamba uteuzi lazima uteue watu waliowahi kuwa mawaziri hata kama walitoka baadae kwa ufisadi, ni sharti uchague kutoa hao ama kuwa badirisha tu hao hao. Maana miaka yote majina ni yale yale tu
Sasa mkuu kwa CCM unazan Nani Ana afadhali maana wote wezi tu, Sasa imagine ndo wamebaki akina Babu tale na kibajaj
 
Back
Top Bottom