Ninavyomkumbuka Maalim

hata Raisi akiteua Mawaziri 23 toka kabila lake, jinsi mnavyopenda kujikomba, mtasema yuko sahihi na ametenda haki.

Anaweza kuwa sahihi kufuatana na KATIBA lakini atakuwa hajatenda haki Iwapo aliowaacha wenye sifa kiubaguzi!
 
..kweli.

..binafsi siamini kama Raisi akitoa maelekezo apelekewe Waislamu 15 wenye sifa za kuteuliwa ktk Cabinet au Katibu Mkuu ktk wizara itashindikana.

Hapo you are assuming huyo anayeomba apelekewe hayo majina ana busara which might not be the case!!
 
JK,
Tatizo kubwa ninaloliona mimi ni kuwa lau kama serikali inajua na kuona hili tatizo lakini kwa kuwa Waislam wenyewe hawajaweza kulifikisha serikalini serikali inahisi iko salama.

Hapa nitasherehesha kidogo.

Waislam ndiyo dini pekee ambayo haina uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka kuanzia mwaka wa 1968 EAMWS ilipopigwa marufuku kuundwa BAKWATA.

Serikali inatambua BAKWATA peke yake kama wawakilishi wa Waislam.
Waislam hawaitaki na haitambui BAKWATA.

Rais Mwinyi yeye katika mambo makubwa aliyowafanyia Waislam ni kuruhusu wakati wa kipindi chake Waislam kusajili taasisi nyingine nje ya BAKWATA.

Tatizo ni kuwa lau kuna taasisi nyingine lakini hizi hazitambuliwi na serikali kama wasemaji wa Waislam.

Kwa hiyo msimamo wa BAKWATA na serikali katika tatizo hili ni mmoja na sawa kuwa Waislam wa Tanzania wana haki sawa nchini na wana fursa zote hawana malalamiko yoyote.

Yapo mengi lakini naamini kwa hayo niliyoeleza hapo ndipo lilipo tatizo.

Kama Mufti wa BAKWATA siku moja tu angekuwa jasiri na kusema kuiambia serikali kuwa Waislam wana malalamiko kuwa wanabaguliwa...

Waislamu wanabaguliwa wapi? Leo kwa mfano serikali ikaruhusu taasisi nyingine zaidi ya Bakwata zisajiliwe, unafikiri atakayeathirika ni nani? Ni kweli serikali au kutatokea "vita ya wenyewe kwa wenyewe"?
Tuombe Mwenyezi Mungu atuzidishie hekima. Kuna maswali magumu kamwe hayawezi kujibiwa kirahisi kama tunavyopenda.
 
..kweli.

..binafsi siamini kama Raisi akitoa maelekezo apelekewe Waislamu 15 wenye sifa za kuteuliwa ktk Cabinet au Katibu Mkuu ktk wizara itashindikana.

Driving force iwe kukidhi vigezo. Tusianze kuchaguana sababu ya dini tu hata kama hatuna sifa na vigezo. Mimi si muumini wa kushirikiana na mtu sababu ya dini au kabila lake. Naamini katika competence. Ndio maana nimeshaajiri mara kadhaa watu tofauti na dini na kabila langu katika kazi
 
..asante kwa maelezo yako.

..lakini wapo Wakristo wengi tu ambao waliteuliwa ktk nafasi mbalimbali na utendaji wao haukuwa wa kuridhisha na wameliingizia taifa hasara.

..mimi nadhani hatua za kuonyesha kwamba "keki ya taifa" inagawanywa kwa usawa zinatakiwa kuwa endelevu.

..siyo jambo zuri kuwa na sehemu ya jamii ya Watanzania ambao wanajiona hawatendewi haki ktk taifa lao.

Hoja ya kuchagua na kutengua isiwe dini ya mtu. Iwe uwezo wa mtu katika nafasi anayopewa. Tutaliangamiza taifa kama kila siku tunadanganyana dini fulani inaonewa na dini fulani inapendelewa. Bila kusema kivipi.
Kuna watu ni wadini sana. Hawafurahi kushirikiana chochote na mtu asiye wa dini yake. hata kama kwenye kundi lake kuna watu ambao wananuka sababu yaubabaishaji wanaoufanya.
Tuna mifano kadhaa ambayo vigezo vya kidini vimetuletea dhahama. Tukumbuke, kusoma na kupata Phd au degree kadhaa, sio kigezo pekee cha mtu kufaa kuwa kwenye nafasi ya utumishi wa umma, kwa kuchaguliwa au kuteuliwa.
Imagine Mzee Kitwana Kondo(RIP) na vurugu zake, ndio anabeba agenda ya nafasi sawa kwa dini zote. Tuwe tunaona aibu wakati mwingine. The good intentions, being executed without credible and reliable people, make the whole thing looks like a soap opera.
 
Sasa tumetoka katika mjadala wa kumkumbuka Maalim Seif, tunajadili udini: ukristo na uislamu. Mtoa mada, "MS" warudishe wachangiaji kwenye kichwa cha mada yako!
 
Hoja ya kuchagua na kutengua isiwe dini ya mtu. Iwe uwezo wa mtu katika nafasi anayopewa. Tutaliangamiza taifa kama kila siku tunadanganyana dini fulani inaonewa na dini fulani inapendelewa. Bila kusema kivipi.
Kuna watu ni wadini sana. Hawafurahi kushirikiana chochote na mtu asiye wa dini yake. hata kama kwenye kundi lake kuna watu ambao wananuka sababu yaubabaishaji wanaoufanya.
Tuna mifano kadhaa ambayo vigezo vya kidini vimetuletea dhahama. Tukumbuke, kusoma na kupata Phd au degree kadhaa, sio kigezo pekee cha mtu kufaa kuwa kwenye nafasi ya utumishi wa umma, kwa kuchaguliwa au kuteuliwa.
Imagine Mzee Kitwana Kondo(RIP) na vurugu zake, ndio anabeba agenda ya nafasi sawa kwa dini zote. Tuwe tunaona aibu wakati mwingine. The good intentions, being executed without credible and reliable people, make the whole thing looks like a soap opera.

..wanapoteuliwa Wakristo 23 na Waislamu 3 ndipo hoja ya DINI inapoibuka.

..mimi naamini teuzi za aina hii ndio zinawapaisha watu wabaya WADINI wakaonekana watu wazuri na watetezi wa ndugu zetu Waislamu.

..nakubaliana maoni yako unaposema,"hoja ya kuchagua na kutengua isiwe dini ya mtu."

..mtizamo wangu ni kwamba ili tufike hapo ni lazima tuonyeshe kwa VITENDO na BILA SHAKA YOYOTE kuwa dini siyo kigezo cha kuchagua na kutengua.

..Na kuteua Wakristo 23, huku Waislamu ni 3, is moving in an opposite direction from where we should be going, kule ambako dini sio kigezo.
 
Waislamu wanabaguliwa wapi? Leo kwa mfano serikali ikaruhusu taasisi nyingine zaidi ya Bakwata zisajiliwe, unafikiri atakayeathirika ni nani? Ni kweli serikali au kutatokea "vita ya wenyewe kwa wenyewe"?
Tuombe Mwenyezi Mungu atuzidishie hekima. Kuna maswali magumu kamwe hayawezi kujibiwa kirahisi kama tunavyopenda.

..Why do you believe kutatokea "vita ya wenyewe kwa wenyewe" ikiwa Waislamu watakuwa na taasisi zingine mbali ya Bakwata?
 
..wanapoteuliwa Wakristo 23 na Waislamu 3 ndipo hoja ya DINI inapoibuka.

..mimi naamini teuzi za aina hii ndio zinawapaisha watu wabaya WADINI wakaonekana watu wazuri na watetezi wa ndugu zetu Waislamu.

..nakubaliana maoni yako unaposema,"hoja ya kuchagua na kutengua isiwe dini ya mtu."

..mtizamo wangu ni kwamba ili tufike hapo ni lazima tuonyeshe kwa VITENDO na BILA SHAKA YOYOTE kuwa dini siyo kigezo cha kuchagua na kutengua.

..Na kuteua Wakristo 23, huku Waislamu ni 3, is moving in an opposite direction from where we should be going, kule ambako dini sio kigezo.

Jokakuu;

Kuna mama mmoja anaitwa Carly Fiorina. Kuna wakati alikuwa ni CEO wa HP. Anasema kwenye diversity issue, viongozi wanaongalia circle zao tu au network zao, mara nyingi wanashindwa kupata watu ambao wako nje circle na network zao. Hivyo unapoona kuna mapungufu ya diversity, lawama isiwe kuwa kuna lack of resource kwenye jumuia fulani. Mara nyingi ni ufinyu wa yule mwenye madaraka ya kutafuta talents.
 
..wanapoteuliwa Wakristo 23 na Waislamu 3 ndipo hoja ya DINI inapoibuka.

..mimi naamini teuzi za aina hii ndio zinawapaisha watu wabaya WADINI wakaonekana watu wazuri na watetezi wa ndugu zetu Waislamu.

..nakubaliana maoni yako unaposema,"hoja ya kuchagua na kutengua isiwe dini ya mtu."

..mtizamo wangu ni kwamba ili tufike hapo ni lazima tuonyeshe kwa VITENDO na BILA SHAKA YOYOTE kuwa dini siyo kigezo cha kuchagua na kutengua.

..Na kuteua Wakristo 23, huku Waislamu ni 3, is moving in an opposite direction from where we should be going, kule ambako dini sio kigezo.

lakini viongozi wakuu wote ukiondoa Rais ni waislamu. Who cares? Mbona wako kisheria na wanafuata taratibu. Nina mashaka sana na hili lengo la kubalance dini. Kama wahindi, waarabu na wazungu nao wanegkuja na hoja kama hii, it could be a disastor
 
..Why do you believe kutatokea "vita ya wenyewe kwa wenyewe" ikiwa Waislamu watakuwa na taasisi zingine mbali ya Bakwata?
Ubaguzi una laana ndani yake. Hata kwenye dini moja kumbe kuna madhehebu. Hii si nadharia hata kidogo. Ni kitu kipo kabisa
 
Tangawizi,
Hili ndilo tatizo la kutaka kujadili kitu usichokijua.
Madhehebu katika Uislam si ubaguzi ni ikhtilaf katika mafunzo na uelewa.

Kabla hujaandika ingia hata Google ujifunze kwanza kile unachotaka kuandika.

Ubaguzi unaozungumziwa hapa ni huu ambao dini moja toka uhuru upatikane mwaka wa 1961 imekuwa ikihodhi fursa zote nchini kuanzia elimu, nafasi katika serikali, bunge, baraza la mawaziri unawakuta wao peke yao.

Wale walio nje ya fursa hizo wanapouliza hakuna majibu yanayotolewa ila wanatokea wale wale wanaonufaika na hali hiyo kutoa kejeli.
 
Mzee Mohammed,

Kwa bahati mbaya Wamisionari wa Kikristu walipokuja kutangaza dini yao, waliwafundisha pia waumini wao elimu dunia.Hivi ndio kusema elimu dunia ambayo ndio inatumika serikalini ilisambazwa sana na hawa Wamisionari.Ukiangalia shule nyingi ambazo baadae serikaali hii unayoilaumu ilizichukua kutoka kwa Wamisionari ili wananchi wote hata sisi tusiokuwa na dini tupate elimu.Hapa nazungumzia Shule kama Pugu,Minaki,Ihungo, Tosamaganga,Tabora Boys, na nyinginezo kama hizo.Hizi zote zilikuwa zinamilikwa na Wamisionari Wakikristo.

Kumbe basi kutengwa huku unako kupigia chapuo Mzee wangu ni kwa kuwa tu, historia ilikuwa hivyo.Kuwa wasomi wengi (wa elimu dunia) aghlabu wametokea kwenye shule za hawa mambwana. Huu ni ukweli mchungu. Hata serikali za kikoloni zilikuwa zinaajiri watu waliopata elimu dunia.

Binafsi shida pekee nayoiona kwa Wamisionari Wa Kiislam ni wao kutozingatia sana kutoa elimu dunia. Sasa hapa ndio ikazirudisha nyuma sana jamii za Kiislam katika kupata ajira Serikalini. Huwezi kupewa ajira kama huna elimu dunia. Hii ni kwa kipindi hicho cha zamani mpaka sasa.

Nitawapeni. Mwaka 1993 nilijiunga kidato cha kwanza Kibaha Secondari nikitokea Moshi Vijijini.Wakati huo Mkoa mzima wa Kilimaanjaro una shule 85 za sekodari huku Mkoa wa Pwani ukiwa na Sekondari, zisizozidi 5 za binafsi na serikali.Hapa nataka kusema nini? Vijana wengi kutoka Pwani amabo majority in Muslim walikuwa wana nafasi haba sana za kupata elimu ya sekondari.Sababu ni uhaba wa Shule hii inatoka na jamii ya mkoa huu kukosa msukumo wa elimu dunia toka kwa Wamisionari waliokuwa maeneo haya. Kama hawa wangelijenda Sekodari miaka hiyo ya 1920-1960 wangezalisha wasomi wengi amabo wangekuwa chachu ya maendeleo na wao kujenga sekondari nyingi zaidi mkoa wa Pwani. Hiki ndio kilifanywa na Baba na Bu zetu Kilimanjaro. Kwa kuwa wao walibahatika kusoma elimu dunia basi mwitikio wa ujenzi wa shule za binafsi ulikuwa mkubwa sana. Binafsi nisingepata bahati shule ya Serikali, ningesoma Sekondari ya Kata miaka hiyo. Dhana ya kila kata kuwa na sekodari mkoani Kilimanajaro ilianza miaka ya 1985.

Sasa basi hali hiyo ya mkoa wa Pwani iweke hivyo kwa mikoa mingine.Kiufupi maeneo yaliyokaliwa na Wamisionari wa Kikristo yalipata msuko wa elimu dunia ikilinganishwa na maeno ya wamisionari wa Kiislam.

Mwaka 2000 Nilijiunga Chuo Kikuu Cha Dar.Nikiwa Kitivo Cha Biashara. Kati wa Wanafunzi 150 tuliojiunnga wanafunzi takribani 50 walitokea Kilimanjaro.Hii ni kusema hawa sio kwamba walikuwa wako bright zaidi ya mikoa mimngine, la hasha hawa wamebahatika kutoka maeneo ambayo shule zilikua nyingi.

Niwape kisa kingine, kabla sijamalza mjadala. Mwaka 2003 tukiwa tunakaribia kumaliza Shahada zetu, Kampuni iitwayo kipindi hicho (Massawe Ernst & Young) ilihitaji Gradute Trainee Auditors. Wakaja pale Mlimani kwenye Kitivo Chetu.Walihitaji watu 10 tu. Basi wakatupa mtihani. Wakapata watu wao 10. Wakatoa majina yao. La hasha wote walikuwa Wachagga tupu. Sasa baadae watu wakalalamika kuwa kwa Kuwa Partner ni Mchagga basi alichagua wachagga wenzio. Sasa sisi wachagga wengine tukasema hapana , hakuchagua Wachagga amechagua Warombo.Maana Massawe yeye ni mrombo. Lakini hii kwetu ilikuwa ni husda tu maana waliochaguliwa walikuwa vipanga kweli kweli. Kumalizia hii hadith, haya maneno yalipofika kwao wakaweka tume kuchunguza mchakato. Kumbe basi aliongoza mchakato alikuwa Prtner kutoka Zimbabwe akiitwa Sydney Bvurere na Manager Mwingine kutoka Nigeria. Hawa wato hawakuwa wakijua majina ya Kichagga.Na tuliokosa ni kuwa hatkuwa na viwango.

Kumbe basi ubaguzi huu ulituandama sisi Wachagga including walio kuwa Waislam Wachagga kwenye selection za kuingia TRA,BOT.

Kwa kumalizia ubaguzi wa dini,kabila etc hauwezi kuwa justified kwa sababu yoyote. Kusema Baraza lina Mawaziri 23 wakristo hslimsaidii Mkristo independently. Tufocus kwenye maendeleo mwenye sifa apewe. Mimi sijali kama viongozi wote serikalli nzima wawe Waislam tupu as longo as wanatuletea maendeleo. Na vile vile tusiwanyinme watu nafasi sababu ya dini au kabila.

Kwa kumalizia Mzee Mohammed, mambo ya historia itachukua muda kuyabadili.Tusijenge chuki miongoni mwetu kwa dini zetu.
 
Fideline,
Hujui historia ya Waislam na ndiyo maana unadhani kwangu mimi kuisahihisha historia rasmi najenga chuki katika jamii.

Ningekushauri usome vitabu hivi ili uelewe hali iliyoko Tanzania.

Msome Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2000).

Kitabu cha Njozi serikali imekipiga marufuku.

Kitabu cha Bergen killikuwa kinauzwa Cathedral Bookshop kimeondolewa madukani kimya kimya hali kadhalika kitabu cha Sivalon.

Umechelewa sana kuingia na mimi katika mjadala huu.

Huu mjadala tumuemaliza miaka mingi sana iliyopita.
 
Asante Mzee Wangu Mohamed, je mlijadili mjadala huu hapa jamvini? Nitavitafuta vitabu ulivyosema nivisome.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom