Ninavyoikumbuka 24-25th November

Lucas

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,457
1,108
ilikuwa ni ijumaa ya tarehe 24-11-2000, kipindi hicho nikiwa mwanafunzi wa Tosamaganga Iringa, siku hii tulifunga shule na kuruhusiwa kwenda makwetu baada ya kumaliza mtihani wa mwisho.
kwa hamu ya kwenda nyumbani, tuliamua kutafuta usafiri wa kuondoka Iringa siku hiyo hiyo na kwa bahati tukapata basi la kampuni ya safina lililokuwa tupu bila abiria yeyote mnamo saa nane na nusu mchana, tulikuwa kama wanafunzi 20 kutoka Tosa boys, na abiria wengine kama wa 3 hivi, safari yetu ilianza vizuri sana...
 
nakumbuka tulisimama kula pale Ilula mnamo saa 9, kisha tukaendelea na safari yetu saafi tukiwa na matarajio ya kufika Dar around saa 2 usiku.

Tulipofika Mikumi hapo ndipo safari yetu ilibadilika! tulifika na kukuta umati mkubwa sana wa watu ambao tulikuja kujua ni walikuwa abiria wa treni ya tazara iliyokuwa imeharibika huko Mang'ula kwa siku tatu hivyo wakaamua waje kutafuta usafiri mikumi.

kondakta alipofungua tu mlango, hakuweza kuuzuia umati ule, akawaambia kwa nauli ya kulangua 9000....
 
wale watu walipanda na kujaa utadhani Dcm ya kwenda mbagala, ile raha ya safari ikaisha! seat ya watu 2 walikaa watatu! njia ya kupita haikuwepo tena, kwa ufupi gari ilikuwa na zaidi ya abiria 100, speed ya gari ikapungua na matumaini ya kufika mapema yakapungua...

baada ya muda si mrefu tukaingia kwenye eneo la hifadhi ya taifa ya mikumi.

tukiwa tunakaribia kutoka mbugani, eneo linalofahamika kwa tembo wengi na karibu na kibao cha kikoboga, hapo ndipo tukakutana na kadhia...
 
Ilikuwa yapata saa 12 jioni, dereva akajaribu kuwakwepa swala waliongia barabarani, alipoondoka ghafla muungurumo wa engine ulibadililika, na baada ya hapo gari ilizima tukiwa kilimani, piston moja ilivunjika! abiria wote walishuka na kuanza kutafuta usafiri, sisi tuliotoka iringa tukaambiwa tusubiri tutafutiwe usafiri... kumbuka tulikuwa katikati ya mikumi national park!
 
nakumbuka tulisimama nje ya gari hadi around saa moja! baada ya kusikia muungurumo wa simba ilibidi wote tukimbilie kwenye basi! tembo walikuwa wakipita around ila hawakuwa na shida na sisi, baadhi ya abiria walipanda malori na kuondoka, and a lot of stuffs. to cut short the storry, tulilala porini ndani ya basi akaja simba usiku pale jirani hadhuru mtu... kwa wanaume ilitubidi kutumia madirisha kwa haja ndogo na kwa wakinamama ilibidi waende mlangoni...
 
stori za kufarijiana na kuchekesha ndio zilitawala na baadhi kusali. kesho yake asubuhi abiria waliendelea kuondoka, na mie niliondoka saa 8, mchana! nikiwa na basi la masiah kutoka mbeya... nilipofika morogoro tumbo likachafuka nikaenda msalani, niliporudi sikulikuta basi! nikapanda basi la sadiq line kuja dar, (nauli ilikuwa 1500) nilipofika ubungo nikaambiwa mizigo iko mnazi mmoja, nikaenda mnazi mmoja nikaambiwa gari imerudi na mizigo ubungo, na nilipofika ubungo nikaambiwa begi liko mnazi mmoja...
 
....mmmh kuna ndugu zetu flani washawahi chokoza tembo hapo Mikumi, mbona walikiona cha mtema kuni!!!....

ila binafsi huikumbuka novemba 25 kama siku niliyozaliwa
 
ilibidi kesho yake, tar 26 nov ndio nikachukue begi langu ... sijui kama nitaisahau safari hii....


leo ni miaka 12 tangu inikute habari hii!


samahanini wadau, natumia simu ndio maana imebidi kukata kata sana story....
 
....mmmh kuna ndugu zetu flani washawahi chokoza tembo hapo Mikumi, mbona walikiona cha mtema kuni!!!....

ila binafsi huikumbuka novemba 25 kama siku niliyozaliwa

ah ah ah sie tuliambiwa tusichokoze mnyama yeyote, na tulikaa macho yakiwa attention kweli kweli...


by the way hepi basdei mkuu
 
siku hiyo nov 24, 2000 ndio nilikuwa naoa. Na kesho yake ilikuwa reception. Nami pia nilisoma Tosa, h/master alikuwa Mpogole a.k.a Dudu. Nakumbuka sifongo na nyali, maandazi ya Kontolengo. Anyway pole sana kwa yaliyokukuta
 
siku hiyo nov 24, 2000 ndio nilikuwa naoa. Na kesho yake ilikuwa reception. Nami pia nilisoma Tosa, h/master alikuwa Mpogole a.k.a Dudu. Nakumbuka sifongo na nyali, maandazi ya Kontolengo. Anyway pole sana kwa yaliyokukuta

hongera sana mkuu, annivesary yako kumbe ina kumbukumbu chungu kwangu! by the way mpogole nilipata kumsikia mie nilisoma kipindi cha mzee mkangwa... yale maandazi tuliyaita mabanzi, mboga za majani zilikuwa shs 10/= tu, samaki wa mtera shs 50... raha!
 
pole sana, lkn nadhani kwa namna fulani ilikuwa nzuri kwa kusikia live mzee simba akiunguruma.
 
pole sana, lkn nadhani kwa namna fulani ilikuwa nzuri kwa kusikia live mzee simba akiunguruma.

nakumbuka kuna mtu alituambia ukimsikia kwa mbaali basi ujue yupo karibu, na vice versa holds the case! na tulimsikia not once, ila ni burudani kiasi fulani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom