Ninauliza Je Kula Mihogo Mibichi kuna Faida gani? Je hakuna Madhara kula Mihogo Mibichi?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Mihogo.png



Biashara ya mihogo ya kutafuna inaenea kwa kasi jijini Dar. Mihogo hii mibichi ya kutafunwa wauzaji wake wengi ni wanawake. Mara nyingi huuza na nazikavu ya kutafuna (mbata). Uchunguzi unaonesha wateja wengi wa bidhaa hizi ni wanaume. Pichani anaonekana dada akiandaa mihogo hiyo huku akiongea na simu.
Je wewe ni mmoja wa walaji







 
Mkuu hilo lori lililobeba kontena.....ni pancha au?usikute ndo yaleeee makontena .....
 
MziziMkavu nafurahi tena kuona udadisi wako kwenye masuala ya afya. Hili la mihogo mibichi nami pia nililisikia wengine wakilihusisha na masuala ya nguvu za uzazi na kunivutia kutaka kujua kwa undani!

Baada ya kupitia pande zote mbili, niliona madini ya zinki na potasiam kama kiungo mojawapo kinachoweza kusababisha uhusiano wa ulaji mihogo na nguvu za kiume. Madini ya zinki na potasiam yanapatikana kwa wingi katika mihogo na upatiakanaji wake huwa mzuri zaidi kabla muhogo haujapikwa kwani kupika sana kunasababisha "reaction" itayopelekea kupungua kwa asilimia ya madini yatayopatikana.

Lipo chapisho linalothibisha kuwa zinki ni kichocheo muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za kiume, majimaji na homoni za mapenzi. kunapokuwa na muunganiko wa uzalishaji mkubwa wa mbegu za kiume, majimaji ya kuziweka hai mbegu zinazozalishwa, na kichocheo cha hamu ya tendo la ndoa, ni wazi kuwa ulijali wa mwanaume unaweza kuonekana pasi na shaka.

Pia lipo chapisho linaloonesha jinsi potasiamu ilivyo na mchango mkubwa kwenye uzalishaji wa majimaji mwilini, ikiwa na maana ya maji yanayotumika sehemu mbalimbali za mwili. Kutokana na tabia hii, potasiamu imethibitika kuwa na mchango mkubwa sana katika kupunguza presha na mapigo ya moyo. Its obvious, mtu ambaye amepata "effect" ya zinki, atahitaji usaidizi wa kushusha presha na mapigo ya moyo... teh teh teh!!

Kwa hali hii, nadhani kuna uhusiano japo mdogo kati ya dhana vichwani mwa madereva wa vyombo vya usafiri hasa ukizingatia madhara wanayoyapata kwa kukaa sana kwenye siti za magari, huku miguu ikiwa imebanwa, na joto litokalo na kuchemka kwa injini ya gari. Licha ya kwamba vipo vyakula vingi vinavyoweza kuwasaidia, lakini upatikanaji rahisi wa mihogo katika jamii yetu, ladha na mchango wake katika kuongeza nguvu, kunasabbisha mihogo kuwa kimbilio la walio wengi.
 
Back
Top Bottom