Ninatatuaje tatizo la best friend wangu asie na marafiki wengine kudhani nampuuza napokuwa na washakaji wengine

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Kiufupi mimi ni mtu wa watu sana na nina marafiki wengi sana

Hawa mrafiki sio marafiki basi tu, Ni marafiki haswa, Yani kwa siku lazima tuchekiane kwenye simu, wanakuja home mara kwa mara, nikipata matatizo husaidia, n.k

Sasa ishu inakuja kwa besti yangu hapa yaani naonaga kama vile hapendagi navyopeana kampani na watu wengine na mbaya zaidi namjua vizuri kwamba nje ya mimi hana marafiki wengine wa nguvu, namjua tu rafiki yake moja tu ambae hata sio urafiki mzito.

Mke wake huwa ananiambia hata simu yake nje ya mawasiliano ya kazini na ndugu zake, mara nyingi ni mimi tu ndie naewasiliana nae kirafiki na huwa anachangamka sana ikiwa ni mimi, Kiukweli ni besti wa nguvu kuzidi marafiki zangu wote ila ndio vile tena upweke unamsumbua.

Nadili vipi na hii hali
 
Fuatilia ujue tabia za watu ambao ni Introverts haitakupa shida,na usifikiri yeye kutokuwa na marafiki wengi inampa matatizo,ubongo wake tayari umeshaji tune kuwa maisha yanawezekana kwa jeshi la mtu mmoja tu au hao marafiki zake wachache kama wewe,wakati wewe unaona bila ya marafiki maisha hayatakwenda...
 
Kabisa mkuu.
 
Huyo huenda kunatatizo lilishawahi tokea hapo kabla kutokana baadhi ya marafiki zake
 
Mimi pia nina tatizo hilo pia yaani msaada mkubwa kwangu huwa ni girlfriend ambae atacheza pande zote mbili yaani awe Rafiki na mpenzi kwa wakati mmoja!ukiondoa sms za biashara sms zingine nazopokea ni za tatu mzuka tu
 
Rafiki yako ni mgonjwa ,urafiki wa kawaida wa wanaume huwa hakunaga wivu kabisa tena mm ninavutiwa kuwa na marafiki wenye marafiki wengine maana huwa naona wananiongezea marafiki ,urafiki huleta connection za hela,ujuzi ,fursa etc ikiwa unachagua marafiki kwa makini.Mimi rafiki zangu majority wako busy na biashara na familia zao( wake zao) so muda wetu huwa kuonana ni bar tunakutana saa 3 saa 6 tunaaga na hakuna hata kuulizana ulifika salama .
 
Nilichoelewa jamaa ni introvert halafu ww ni mtu wa washkaji, so ukiwa na washkaji wengine inabidi yeye awe kando maana kwake hao watu ni kama kero kwake.
Nakubali,mm pia ni mtu wa aina hiyo na huwa najihisi hivyo mara nying. Siwezi mfanya rafiki awe wangu peke yangu, lakn pia napenda atambue uwepo na nafasi yangu kwake kama ilivyo kwake kwangu. Sipendi kuchanganywa na wimbi la watu wengi ambao sijawazoea au sio washkaji zangu,hivyo ni sawa kama ana spend nao mda lakn pia atambue pia na mm nipo
 
Usidhani ulivyostaarabika ww ndivyo walivyostaarabika wengine. Sio kosa lako kwamba kwann dhana yako ktk urafiki ipo hivyo na sio kosa lake mleta mada kama dhana yake juu ya urafiki ipo vile. Hivyo jifunze kuwa na tolerance pale unapokutana na vitu huvijui au vigeni
Urafiki wa kiboya huo nyie ndo mnaanzaga ivyo ivyo mambo ya ushoga pumbavu kabisa mwanaume unaanzaje kumuonea wivu akihang na marafiki tofauti tofauti kama anaona hamuelewi anaachana nae wanaume hatufosi urafiki
 
Rafiki yako ni mgonjwa ,urafiki wa kawaida wa wanaume huwa hakunaga wivu kabisa tena mm ninavutiwa kuwa na marafiki wenye marafiki wengine maana huwa naona wananiongezea marafiki ,urafiki huleta connection za hela,ujuzi ,fursa etc ikiwa unachagua marafiki kwa makini.Mimi rafiki zangu majority wako busy na biashara na familia zao( wake zao) so muda wetu huwa kuonana ni bar tunakutana saa 3 saa 6 tunaaga na hakuna hata kuulizana ulifika salama .
Huo ndo uanaume sasa nikiwa na mshikaji naye ana washkaji tunaungana tunakuwa wana sasa wewe hupendi niwe na wana unataka nini sasa mm nakutema tu
 
Mambo ya kishoga hayo na nyie lazima mtakua mash-ga.. You got that right.
 
Back
Top Bottom