Ninatarajia kupokea milioni moja na laki mbili. Nataka nilime

Kwa huo nsimu wa January mpaka March au April mazao hayo yanafaa mkuu? Ngoja nisome utafiti kidogo juu ya ushauri wako nitakurejea.
Mtaji wako ni mdogo sana kulima mazao Kama nyanya na hoho kwa shamba lenye ukubwa wa heka 1.
Kwa hyo pesa nyanya na hoho hapana sikushauri. Labda mahindi
 
Okay safi sana kilimo ni hela sana...mimi nakushauri usilime mazao ambayo kila mtu analima, yani mazao ya mkumbo. Maana kuna watu wakisikia matikiti yana hela wote huko, mara mahindi yana hela nao wote huko jambo ambalo mwisho mnalima wengi na soko ndio hivyo hela ndogo.

Nakushauri kwanini usilime zao kama soya, soya ni muhimu sana kiafya na ni zao ambalo linavumilia hali zozote. Soya hustahimili ukame, udongo wa tifu tifu pia unalima hadi udongo wa mfinyanzi. Matunzo yake ya kawaida sana, magonjwa makuu ya soya ni ukungu na bacteria tu. Ambazo kuthibiti bacteria kutumia kilimo cha mzunguko yani crop rotation. Haya mbolea hahitajiki sana katika soya ni inategemeama na rutuba ya udongo unaolima. Fanya utafiti kuhusu soya, mazao ambayo hayazingatiwi sana na watu soko lao linakuwaga zuri sana sana. Ama kwa hakika ukifuata huu ushauri na ukaacha kulima kwa mkumbo kama wengine, utaona kilimo ni bora sana
 
Ungeniambia sh ngapi kwenye haka moja ungenifaa sana, ninaweza kuongeza pia naomba tusaidiane hapa
Mtaji wako ni mdogo sana kulima mazao Kama nyanya na hoho kwa shamba lenye ukubwa wa heka 1.
Kwa hyo pesa nyanya na hoho hapana sikushauri. Labda mahindi
 
miminimama,

Kilimo au aina yeyote ya uwekezaji ina hitaji kwanza kujua wateja wako, lenga soko kwanza, angalia gape lililopo then tumia fursa. Ukichunguza kwa umakin,unaweza jikuta hata huingii shambani kulima ila utaweza onekana mkulima kwa kuwa utakuwa na product za kutosha.

Kila kitu kina hela, isipokuwa ni kuamua kuingia katika masafa hayo na kuinusa pesa humo.

Ukiishi kwa kumsikia fulan anasema matiki yanalipa, mara vitunguuu, mara miti, utakuja kuyumbishwa hadi katika chai. Utajikuta unachoma pesa na kitu hakionekani, zao utalo ambiwa leo lina soko, utakuta baada ya miezi mitatu hadi unavuna halina ishu.

Tanua na fungua macho kisha angalia fursa zozote kwa kuwa open minded, chunguza fursa then ingia, lakini baada ya kufanya utafiti binafsi sio fulani kasema.
 
Mtaji wako ni mdogo sana kulima mazao Kama nyanya na hoho kwa shamba lenye ukubwa wa heka 1.
Kwa hyo pesa nyanya na hoho hapana sikushauri. Labda mahindi
Nisinge mshauri kulima mazao kama hayo. ni pasua kichwa
 
Kwa haraka haraka mpaka sasa utakuwa na laki 6;hizo zinatosha kuanzia

kama utakuwa na mda wa kusafiri kwenda mkoani kuangalia shamba mara moja kwa wiki au wiki mbili. nicheki nikusaidie.
kwa hizo pesa ulizo nazo utaweza kulima shamba kuanzia heka 10 na kuendelea. na zikabaki.

Msaada nitakaokupa ni

1. kukumegea heka kuanzia 5 - 10 kny shamba ninalotaka kuanza kulima ambalo utalilipia baada ya kuvuna.
2. nitakupa ushauri wa mazao ya kulima pamoja na mchanganuo wa gharama
3. Nauli ya kwenda kukagua shamba nitatoa mimi (kwani shamba langu na lako vitakuwa vimepakana hivyo utakuwa unaniangalizia na la kwangu pia.
4. gharama za msimamizi wa shamba nitatoa nitatoa mimi.

Nimeanza matayarisho ukiwatayari nitafute.
 
Mkuu ungesema japo kwa kifupi mashamba yako, yapo sehemu gani huenda ungepata wadau wengine wenye nia za kumiliki mashamba ok
 
Kama ni mara ya kwanza usijaribu utapata hasara, kilimo hakipo hivyo unaweza kulima hata mara 5 ukapata hasara ila unaweza kuja lima mara ya sita utapiga sana hela. Kikubwa usikate tamaa wekeza kwingine ila kusemea kwa 100%utapata kwenye kilimo siafiki.
 
Pesa ulo nayo ni ndogo sana kuizika kwenye kilimo kwani kilimo kinahitaji mambo mengi ukizingatia umesema ni mara yako ya kwanza.

Badala ya kulima bado una uwezo wa kununua mzigo na ukapeleka sokoni ukauza na kupata faida kubwa tu ambayo kwa miaka miwili au mitatu utakuwa juu sana.

Ukija mbeya kwa pesa hiyo kwa kuanzia waweza amua kununua kimoja kati ya ndizi,karoti,mchele,mahindi mabichi,viazi mviringo au maharage.Sijataja nyanya kwa sababu maalumu.

Ukitaka kufaidi biashara hii jitahidi uanze na mtaji wa milioni 3 na uwe mtulivu siyo mtu wa papara na tamaa.

Ni heri ukavuta ukaongeza capital ila ukafanya kitu cha maana.Pia ni kwa yeyote bado inafaa tu.
 
Nenda Iringa kalime green beans soko uhakika unamuuzia Kjadija (GIBRI) gharama za kulima ni million 1.5. Ukitunza vizuri unaweza pata kg 3500 mpaka elf 4500 kwa ekari
 
Back
Top Bottom