Shairi: Ninatafuta Upendo!

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Nimechoka taabani, niko hoi sijiwezi
Bado nipo safarini, mwisho sijaumaizi
Ninatafuta upendo.

Ninausaka upendo,kwema kule ulipo
Ninaongeza mwendo,nifike nipatakapo
Ninatafuta upendo


Anayejua ni nani, haraka aniambie
Kwani u mahala gani, aseme nimsikie
Ninatafuta upendo

Sitochoka kutafuta,mpaka mi niupate
Tamaa sitoikata, mpaka niufumbate
Ninatafuta upendo

Upendo ni mbegu bora,iotayo mioyoni
Kadhalika ni ishara, ya mtu alo makini
Ninatafuta upendo

Upendo pia ni dawa,kwa walokata tamaa
Upendo kionyeshewa,nguvu zinawajaa
Ninatafuta upendo

Siupendi unafiki, kutabasamu usoni
Kumbe umejawa chuki,kinyongo tele rohoni
Ninatafuta upendo.
Ninatafuta upendo.
 
Ni mwema wake moyo
Mengi anipa bila choyo
Mazuri ayafanyayo
Huba kulipalilia.

Ni njema yake roho
Kwa mahaba simroho
Ameshanivika joho
Mahaba anipatia

Penzi anipa kwa dhati
Penzi liso tashtiti
Nami sitomsaliti
Penzi lake nitalienzi

SIYABONGA
 
Ni moyo wa namna gani
Shujaa alokuwa nao?
ule usiotamani
kupendwa na wapendao?

Mgumu kiasi gani
Usivutwe na sumaku?
nguvu ilo upendoni
Aijua hata kuku

Ona tajiri wa pesa
Alivyojikondea
Mtazame profesa
alivyonyong'onyea
kwa sababu wamekosa
upendo wanalilia
 
Back
Top Bottom