Ninasikitishwa sana kupanda kwa kasi ya ajabu bei ya vifaa vya ujenzi

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Tunakoelekea siyo kuzuri. Ninasikitishwa sana kupanda kwa kasi ya ajabu bei ya vifaa vya ujenzi. Pamoja na kupanda kwa mafuta haiwezekani bei ya vifaa kupanda kwa kasi vile. Nitoe tu mifano michache.

(1) Sheet moja ya alluminium ilikuwa inauzwa hapa Mwanza kwa Tshs.160,000 jana nimeambiwa sasa ni Tshs. 280,000. (2) Sementi mfuko moja ilikuwa inauzwa Tshs.19,500 sasa sementi mfuko huo moja unauzwa Tshs.22,000.

Mifano ni mingi ukichukulia nondo, mabati, gypsum powder, gypsum boards, rangi aina ya plascon, vitasa, misumari aina zote, mbao n.k vyote hivi bei imepanda kwa kasi sana.

Ni vema Serikali ikaingilia na kuona kuna tatizo gani na kutoa mrejesho kwa wananchi haraka iwezekanavyo.
 
1B460A2F-63D7-4DE2-B489-1184D8C6CCE6.jpeg
 
Tunakoelekea siyo kuzuri. Ninasikitishwa sana kupanda kwa kasi ya ajabu bei ya vifaa vya ujenzi. Pamoja na kupanda kwa mafuta haiwezekani bei ya vifaa kupanda kwa kasi vile. Nitoe tu mifano michache. (1) Sheet moja ya alluminium ilikuwa inauzwa hapa Mwanza kwa Tshs.160,000 jana nimeambiwa sasa ni Tshs.280,000. (2) Sementi mfuko moja ilikuwa inauzwa Tshs.19,500 sasa sementi mfuko huo moja unauzwa Tshs.22,000. mifano ni mingi ukichukulia nondo, mabati, gypsum powder, gypsum boards, rangi aina ya plascon, vitasa, misumari aina zote, mbao n.k vyote hivi bei imepanda kwa kasi sana. Ni vema Serikali ikaingilia na kuona kuna tatizo gani na kutoa mrejesho kwa wananchi haraka iwezekanavyo.
Pole sana ndugu yangu wa Koryo. Kupanda kwa gharama za ujenzi ni nchi nzima. Siyo vifaa vya ujenzi tu hata soda sasa imepanda mitaani tunanunua 600. Chakushangaza eti soda nayo imekuwa bidhaa adhimu jijini Dar es salaam.
 
Ninachoipenda hii serikali sikivu ya CCM in anapoharibu,huwa inaharibiya wote bila kujali wewe ni chama gani,tunaisoma namba wote

Ninachojua mimi Raw materials hakuna au zinapatikana kwa uchache baada ya China kupunguza uzalishaji

Pia Meli hazifiki Tanzania kwa Wakati
 
Hii nchi kwa sasa inaendeshwa kwa utaratibu wa kujipimia, usitarajie improvement yoyote kwa viongozi wa aina hii.......white powder imepanda kutoka elf 15 kwa mfuko hadi elf 35 hukoo ndani ya miezi sita tu, tumerudi kulekule kwa majizi.........
 
Back
Top Bottom