Ninasikitishwa na jinsi Watanzania wanavyoshangilia mauaji na kutamani itokee vita kati ya Marekani na Iran

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Pengine wataalamu wa saikolojia wanaweza kutusaidia kwa nini hali iko hivi.

Nimefuatilia JamiiForums Instagram maoni ninayoona masikitiko matupu. Mtu anashangilia kuuwawa kwa wanajeshi 80 wa Marekani. Inawezekana ni kweli Wamarekani wameanza wao, ila ni nini kinafurahisha watu kuhusu hili?

Mimi huwa najiuliza, iwapo Marekani isingekuwa na nguvu, dunia ingekuwaje?

Je, kungekuwa na utulivu na amani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nje ya mada kidogo..

Umenikumbusha documentary moja nilikua naangalia ya WW2. Kwamba wakati vita ile inaanza, vijana wengi hasa wa nchi za ulaya walijitokeza kwa hiyari kwenda kupigana. Wengi walikua wakionekana wakishangilia tukio hilo huku wakipiga kelele, kuruka ruka na kila aina ya shangwe wakati wakielekea kwenye uwanja wa mapambano. Ndani ya wiki mbili, wote walikua ama wameshakufa, au hawana miguu, mikono, vichwa nk.

Watu wengi wanashangilia vita kama vile wanavyoshangilia mpira, kwamba Marekani akimtwanga Iran au Iran akimtwanga Marekani as if vinavyopigana ni vichuguu. Wasijue kila anaekufa ni mtu kama wewe, mwenye mipango, familia, watu wanaomtegemea nk. Pia vita hua haitabiriki, unaweza sema wanaopigana ni Iran na Marekani ukashangaa athari zake zinakupata hadi wewe kwa namna moja ama nyingine. Vita yoyote sio kitu cha kushabikia.
Pengine wataalamu wa saikolojia wanaweza kutusaidia kwa nini hali iko hivi.

Nimefuatilia JamiiForums Instagram maoni ninayoona masikitiko matupu. Mtu anashangilia kuuwawa kwa wanajeshi 80 wa Marekani. Inawezekana ni kweli Wamarekani wameanza wao, ila ni nini kinafurahisha watu kuhusu hili?

Mimi huwa najiuliza, iwapo Marekani isingekuwa na nguvu, dunia ingekuwaje?

Je, kungekuwa na utulivu na amani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achilia mbali yote, ila Muajemi kamfanya US kitu inaitwa mikwara kawapige wanao siyo mimi.
 
Wacha washangilie hawana maono wala hawajawahi kuona hata vita ya siafu achilia mbali ya silaha za maangamizi
Wengi huwa wanapenda hata nyumbani kinuke lakini wasichokijua ni kuwa kila mtu atakimbia kivyake kutafuta pa kujificha


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Narudia tena vita sio lele mama na ndio maana marekani pamoja na nguvu zake kaufyata.
 
...Vita si nzuri kabisa!

Hata hao washangiliaji wanalijua hilo ila wanachofanya ni kuchangamsha mjadala tu.

Kiuhalisia hawana uwezo wowote wa kuchochea vita kati ya Marekani na Iran maana hawa ni Watz tu sio Waajemi au Wamarekani.
 
Back
Top Bottom