Ninashukuru uliacha kutumia kauli hii nilipokuonya sasa nakuonya tena mimi na wenzangu sio wazembe,tambua hujawai ongeza mishahara ya watumishi

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,368
Sikimbuki ilikuwa lini? Ila ninakumbuka ni kupitia hapa Jf niliwai kuwasilisha onyo kubwa kwa viongozi wa kisiasa hasa wale ambao tuliwachagua kwa kura zetu kuacha kutuita sisi watu masikini.

Nilikataaa nikasema wazi kuwa mimi sio masikini na sitaki kuitwa maskini ili hali mimi kwa hiyari yangu kuwapa nafasi walizo nazo hao watu kupitia boksi la kura.

Nakumbuka nilisema wazi endapo nitaendelea kuitwa masikini nilikusudia kufungua kesi dhidi ya watu hao pasipo kuyumba kabisa.

Sasa leo ninakuja kuonya tena nimechoka mimi binafisi na jirani zangu na ndugu zangu kuambiwa kuwa sisi HATUFANYI KAZI, hii kauli inatolewa sana na Raisi wetu ila kwa kifupi mimi nataka nimwakikishie kuwa sisi tunafanya kazi sana udhibitisho wa ilo ni ongezeko la kodi tunazolipa kutokana na kazi zetu.

Kuna ongezeko la kodi linalipwa na ili halitokani na watumishi wa umma tu kwani akumbuke kuwa yeye tangu aingie madarakani hajawai kuongeza mishahara kwa watumishi wenzake hii ina maana kuwa kodi kubwa inatoka kwetu wananchi wa hali ya chini.

Kwa kifupi tumechoka kuitwa wazembe, sasa jambo ambalo anatakiwa alijue yeye ni kuwa sisi tunachapa kazi na tunaposema kuwa MTAANI HAKUNA PESA tuna maana kuwa mfano zamani ilikuwa kujenga msingi wa vyumba vinne ni shilingi 1200,000 sasa hivi ni shilingi laki400,000 kujenga msingi nakwambia achia pesa sisi tunao chapa kazi tulipwe tunachostaili au tulipwe kile kijachoendana na kazi tuliyoifanya sawasawa na wewe unavyobana pesa halafu ulipwe kidogo ila najua wewe unajichotea tu maana hizi unazogawa sjui za toka wapi? Ni mshahara au ni?
 
Makato nhif ni 40,000 kuanzia January 2020
Nimeona kimemo kinasema watu wa kima cha chini serikalininwatakatwa 40,000.

Ina maana hiyo ni minimum, kuna wengine watakatwa zaidi kwa sababu wanaliowa zaidi?

Mtu anayelipwa 400,000 au chini ya hapo (nafikiri kima cha chini hakizidi 400,000, right?) Ukimkata 40,000 kwwnda NHIF, ushamkata 10% au zaidi hapo.

Hapo bado kodi, mafao, mazagazaga mengine.

Usipoangalia mtu anarusi nyumbani na take home 20%.
 
Makato nhif ni 40,000 kuanzia January 2020
1575015413504.png
 
Kwani Kazishikaje fedha. Mimi naomba kueleweshwa
Rais wa Tanzania ana nguvu sana kuhusu nzunguko wa fedha.

Hi,i ninnamna kumi anaziweza kudhoofisha mzungukonwa fedha.

1.Kwa kukataa nyongeza za mishahara tu anadhoofisha mzunguko wa fedha.

2. Kwa kuchelewa kulipa madeni ya ndani tu anadhoofisha mzunguko wa fedha.

3. Kwa kulazimisha makampuni yaweke fedha kwenye akaunti ya BOT tu anadhoofisha mzunguko wa fedha.

4. Kwa kuingilia biashara ya korosho na kusababisha mismanagement iliyopelekea mapato ya exports za kilimo kuanguka kwa asilimia 55, kwa mwaka mmoja wa kuishia Agosti 2019, kwa kulinganisha na mwaka uliotangulia, kwa mujibu wa ripoti ya BOT ya October 2019, anadhoofisha mzunguko wa fedha.

5. Kwa kuwekeza bila mpango, kisiasa, kwenye biashara ya ndege, na kununua ndege kwa cash, ndege zinazokamatwa hata kabla ya kufika Tanzania, anadhoofisha mzunguko wa fedha.

7.Kwa kuongeza ukiritimba hata katika process ya kutuma hela kutika nje kuja Tanzania, siku hizi hata tukitaka kutuma hela kutoka Wave kwenda M Pesa hatuwezi, anadhoofiaha mzunguko wa fedha.

8. Kwa kukataza makampuni ya nje yasiwalipe mishahara mikubwa Watanzania, anadhoofisha mzunguko wa fedha.

9. Kwa kuzidisha makato kwenye mishahara ya watu wa kima cha chini, NHIF imeoanda mpaka 40,000 kwa watu wa kima cha chini, hiyo ni zaidi ya 10% ya mshahara, ka kato moja tu, anadhoofisha mzunguko wa fedha.

10. Kwa kujiingiza katika vita ya uchumi asiyoijua wala kuiweza, na kutukana wafadhiki wake kama "mabeberu", wakati bado anawahitaji kwenye misaada, na hivyo kujuweka katika positiin ya kike Waswahili walichokiita "Baniani mbaya, kiatu chake dawa", anadhoofisha mzunguko wa fedha.

Kuna namna nyingi sana, ila niishie hapa kwa leo.
 
Nini maana ya mshahara serikalini, ni kwamba tutakupa 100% halafu tutakuchukulia zaidi ya 40% kutoka hiyo 100%
 
Naomba sana Mungu na hii iwe MOVIE kama ile ya MIFUKO YA JAMII.

ATENGENEZEE TATIZO MWENYEWE HALAFU ATUSHAWISHA WATU KULALAMIKA KISHA AJE ATATUE..PAAP 2020 HII IPA ..ANARUDI MAGOGONI KWA 95%.

Just mawazo tu
 
Back
Top Bottom