Ninapomshangaa Magufuli na libeneke la foleni (UFUMBUZI WAKE HUU HAPA!)

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
704
Waungwana,

Naomba kuwauliza. Hivi ni kweli kwamba Mhe. John Pombe Magufuli (MB, CCM, Chato) ametamka kwamba amewapa wakurugenzi wa idara mbali mbali za Wizara ya Ujenzi kutatua zengwe la foleni Jijini Dar es Salaam kwa muda wa MWEZI MMOJA tu? Sidhani kama, kwa akili ya kawaida, hili linawezekana. Hebu tuangalie kinachowezekana.

 1. Kwa hali ya kawaida, barabara zinazopita kati kati ya vitongoji zinaweza kukarabatiwa na kuwa katika kiwango cha changarawe au lami. Kama ni changarawe, basi, mitaro ya kupitishia maji machafu au ya mvua itawezesha barabara hizi kudumu kwa muda mrefu. Zoezi hili lilifanikiwa kwa muda mrefu kwenye kitongoji/mtaa wa Kijitonyama, lakini sasa, baada ya mifereji hiyo kutelekezwa, hali ya barabara imerudi kuwa mbaya kama ilivyokuwa awali. Iwapo barabara hizi, kwa mfano, zilizopo ndani ya Wilaya ya Kinondoni, zitaimarishwa na kuwa katika hali nzuri, zitachangia kupunguza (au kuondoa) msongamano huo wa magari. Lakini SIO KWA MUDA WA MWEZI MMOJA! Hili linawezekana, kwa kiwango cha chini kabisa cha MIEZI SITA!
 2. Lakini permanent solution sio kuweka miundombinu mipya kwenye miundombinu iliyopo, hapa nazungumzia suala la mabasi yaendayo kasi (DART). Mradi huu umekufa kabla haujaanza! Suala hili ni tata, kwani linahitaji ufumbuzi wa kina zaidi. Tatizo ni la kimazingira, sio kwamba mradi haulipi, la hasha! Haufai kwa mazingira ya TZ! Kama kweli tuna nia ya kumaliza hili tatizo, tunapaswa kuweka Public Transport System ambayo itakuwa sahihi na inayolipa kwa wawekezaji, kwa mfano, Monorail System! Miundo mbinu ya Monorail ina faida nyingi sana, na inawezekana kabisa kujengwa hapa nchini, kwani ni ya uhakika na katika uendeshaji wake, suala la hasara halipo kabisa. Kila anayepanda kwenye vyombo hivyo LAZIMA alipe nauli KABLA ya kupanda. Hakuna suala la kumwambia konda akurudishie chenji! Unaenda kituoni, kuna mashine, inakuelekeza, unakata tiketi yako, au kuna mfumo wa kadi za kulipia kwa wiki au mwezi, ambazo ukishalipia, unaitumbikiza kwenye sehemu maalum, kisha mlango unafunguka kukuruhusu kuingia kituoni, ukisubiri "treni ya njia moja" (monorail) ifike kituoni na upande ili uende utakako.
 3. Kwa wale ambao wangependa kusoma zaidi juu ya hili, waende Monorail - Wikipedia, the free encyclopedia na watapata habari zote.
 4. Njia kuu ambazo zinaweza kuanzishwa ni kama ifuatavyo:
  1. Morogoro-Chalinze-Dar
  2. Bagamoyo-Dar
  3. Pugu-Dar
  4. Kimanzechana-Dar
 5. Njia hizi zitawawesha wakazi wanaoishi nje ya Jiji/Mkoa wa Dar kufika kazini na kurudi makwao bila ya kuingia kwenye msongamano wa magari na daladala, hivyo, kwanza, kupungua kwa magari na daladala barabarani kutawezesha ukarabati mzuri na wa kudumu wa miundombinu ya barabara kufanyika, lakini, pili, kutawezesha mamlaka husika kupanga vizuri sehemu za makazi na biashara, kwa kuondoa majengo ambayo yanazuia au yanaharibu mandhari halisi ya Jiji la Dar. Pia, kupungua kwa magari na daladala (kwa kuwa watu watakuwa wanaegesha magari yao kwenye vituo vikuu vya Monorail na kuyakuta wanaporejea makwao) kutapunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na kupungua kwa kiwango cha hewa-ukaa kinachozalishwa na magari, daladala na mabasi, hivyo kupunguza pia viwango vya magonjwa ya saratani. Inaeleweka kwamba uchafuzi wa hali ya hewa kutokana na uzalishaji mkubwa wa hewa-ukaa husababisha pia maambukizi au magonjwa ya saratani.
 6. Lakini jambo la msingi, ambalo ni faida kubwa itakayopatikana kutokana na kuwapo kwa mfumo huu wa Monorail, ni kwamba, taifa litapata faida kubwa kutokana na ukweli kwamba mfumo huu utawawezesha watu wengi kusafiri kutoka maeneo ya makazi yao na kuwahi kwenye sehemu zao za kazi, jambo ambalo kwa sasa limekuwa gumu na shida kwao. Wengi wao wanalazimika kusafiri alfajiri mapema, ili kuwahi kazini. Kwa mfano, kuna watu wanaoishi Morogoro, ambao hufanya kazi Dar es Salaam, na kurejea nyumbani jioni. Hawa hulazimika kuondoka Morogoro takriban saa 11.30 alfajiri, ili kuweza kuwahi Dar, kufika hapa saa 1:30 au 2:00 asubuhi. Tujiulize: Wanalala saa ngapi na kuamka saa ngapi? Pia, hali hii inajitokeza kwa wakazi wa Mbagala na Bunju-Boko-Tegeta pia, hata kwa wale wanaotoka Kibamba, Kiluvya, Mbezi, achilia mbali wanaotoka Kipunguni, Kitunda, Kimanzechana, Segerea, Kinyerezi na kadhalika.
 7. Mwendokasi mzuri, kutokana na ukweli kwamba Monorail inatumia njia yake pekee, na haiingiliani na miundombinu yoyote, unarahisisha watu kuwahi wanapoenda. Lakini, cha msingi hapa ni kuangalia jinsi ambavyo mfumo huu unafanya kazi. Kwanza, hakuna "dereva" wa treni hizi. Zinaendeshwa na computer, kwa kiwango cha usahihi kabisa, bila makosa wala ajali. Pili, wahudumu wanaopatikana ni wanausalama na wakaguzi wa tiketi tu. Tatu, vyombo haviruhusu watu kujazana kupita kiasi. Kuna viwango ambavyo vikizidishwa, chombo kinapiga kelele (alarm) na hakinyamazi mpaka watu wapungue. Hivyo, usalama unakuwa unazingatiwa kila wakati, kwani, HUWEZI KUIHONGA COMPUTER ikukubalie kuzidisha idadi ya abiria. Wapo watakaosema kwamba Wabongo "watachakachua" viwango hivyo ili vyombo viruhusu abiria kujazana. Lakini wakumbuke kwamba, licha ya kwamba haitawezekana, kila kituo kitakuwa kinaweka kumbukumbu ya idadi ya watu wanaoingia kwa wakati mmoja. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kila chombo kitakuwa nacho kina kumbukumbu ya idadi ya watu, kwa hiyo, iwapo chombo kitakachokuwa njiani kitakuwa kimefikisha kiwango chake cha mwisho cha abiria, iwapo kitasimama kwenye kituo kimoja, idadi ya abiria watakaoshuka itakuwa sawa na idadi ya abiria watakaopanda. Iwapo idadi ya abiria wanaoruhusiwa kupanda kwenye chombo itakuwa imefikia tamati, wakati wowote kwenye kituo, milango haitafunguka kuwaruhusu abiria wengine kuingia kituoni ili kupanda, mpaka pale ambapo idadi hiyo itakapokuwa imepungua. Suala la udhibiti na usalama limezingatiwa ipasavyo.
 8. Kwa kuwa watakaokuja kuwekeza mfumo huu wa usafirishaji watakuwa ni wageni (ama kutoka bara ulaya au bara asia), basi, sidhani kama wataruhusu mitambo/vyombo vyao vichezewe na vichakachuliwe na wabongo, kwani watapenda kupunguza gharama za uendeshaji ili kuweza kupata faida na kurejesha pesa ambazo watakuwa wamewekeza, ama kwa kukopa au kutoka vyanzo mbali mbali. Hawataruhusu mzaha au upuuzi wa aina yoyote ile! Watakuwa makini. Labda, baada ya sisi - Watanzania - kukabidhiwa mradi, ndio tufanye mzaha, lakini kwa kuwa mfumo wa Build-Operate-and-Transfer (BOT) kwa sasa unatumika baina ya wawekezaji binafsi wa nje na wa ndani pekee, mradi huu usingeweza kuhamishwa kwenye miliki ya serikali kutokana na kwamba serikali ilikwishajitoa mapema kwenye uendeshaji wa biashara. Atakayeupokea mradi huu anaweza kuwa mbia/mwekezaji mwenza, ambaye naye atahakikisha kwamba mradi utadumu na miundombinu yake haitahujumiwa na mtu yeyote.
 9. Changamoto zipo nyingi, lakini zote zitakabiliwa kadri muda utakavyosonga. Mojawapo ya changamoto ni ukweli kwamba vigogo wengi serikalini wanamiliki daladala, mabasi na vyombo vingine vya usafirishaji kama vile teksi, hata bajaj na bodaboda pia. Hawa ndio watakaokuwa wa kwanza kuupinga mradi huu utakaokuwa na manufaa mengi kwa taifa na Watanzania kwa ujumla. Lakini sisi tunasema, tutatanguliza maslahi ya taifa KWANZA, na iwapo tutakwamishwa, basi, TUTAPIGA KELELE ZOTE kila mahala, ili Watanzania wasikie kwamba SERIKALI YAO inawanyima MAISHABORA KWA KILA MTANZANIA! Tunataka kuleta mapinduzi kwenye sekta ya usafirishaji, na sasa CHAMA CHA MAPINDUZI ndio chama tawala. Iwenye, chama hiki chenye kutetea MAPINDUZI kiyakatae mapinduzi haya ya msingi? Kuna wale ambao watasema suala la nishati ni tata, kwani Monorail zinatumia umeme. Hii si hoja ya msingi hata kidogo. Kuna vyanzo vingi vya hapa nchini vya nishati mbadala ambavyo HAVITEGEMEI umeme wa gridi wa TANESCO. Kuna upepo mwingi kwenye pwani ya Bahari ya Hindi, ambapo hata 200MW zinaweza kuzalishwa kwa ajili ya mradi huu, lakini pia, gesi ya kibaolojia (biogas) nyingi inapotea kwenye vyoo vya shimo vilivyopo "uswazi", kuanzia Mtaa wa Makanya hadi Tandale, kwa Wilaya ya Kinondoni, na hata Mburahati na Kigogo Pia, lakini kuna maeneo kama vile Mikocheni "A" (Kwa Ester) na Msasani Bonde la Mpunga, ambako nako, biogas inaweza kuvunwa, na VINU vya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya biogas vinaweza kujengwa, ili umeme huo uende moja kwa moja kwenye mradi wa Monorail. Biogas hii itawawezesha Watanzania, hususan, wakazi wa Dar es Salaam, waepuke na magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu ambacho mwaka hadi mwaka kinawasumbua wakazi wa Dar es Salaam, kutokana na kutiririka kwa maji-taka yanayotoka kwenye mashimo ya vyoo hivyo, pindi ambapo mvua zinaponyesha, na kadhalika. Kwa kuwa gesi itazalishwa kwa wingi, hakutakuwa na haja ya kuyazoa maji-taka hayo, hivyo, mabaki yatakayosalia kwenye mashimo hayo yatakuwa sawa na samadi, ambayo inaweza kutumika kama mbolea nzuri kwenye mashamba, ili kukuza jitihada za Kilimo Kwanza. Tusione kinyaa kwamba kinyesi cha binadam kinatumika kuzalisha nishati ya umeme na samadi (mboji), kwani jambo hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa kule Namibia, ambalo linawasaida sana kuepuka na shida hizi za MIGAO ya umeme kila wakati, kama ilivyo hapa nchini!

Nimemaliza hoja ya msingi, kuhusu ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa msongamano wa magari jijini Dar es Salaam. Mimi niko tayari kushirikiana na Serikali, nikitumia rasilmali-akili yangu, kuishauri Serikali ili kuunda timu itakayosafiri hadi nchini Malaysia, ambayo ni mojawapo ya nchi iliyofanikiwa kwa muda mfupi zaidi kuliko nchi nyingine (ambapo monorail zinatumika), kujenga mtandao wao wa Jiji la Kuala Lumpur, na kuondoa kabisa tatizo la misongamano ya magari. Waliofika Kuala Lumpur watathibitisha hili. Jiji la Kuala Lumpur ni KUBWA SANA, mara tano zaidi ya Dar es Salaam. Bila monorail, ingekuwa SHIDA KUBWA kusafiri kutoka upande mmoja wa jiji hilo hadi mwingine. Sisi hapa Dar tunaelekea huko. Itafika wakati watu WATAACHA kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine, na hapo ndio SHIDA YENYEWE itakapojitokeza! Tunangoja mambo yaharibike zaidi, kwa kuwa, eti, daladala zetu zitakosa soko, au mabasi yetu yatakosa abiria? Kwa nini TUWAKWAZE wananchi, waendelee kuteseka, wakati mradi huu ni MKUBWA na wenye manufaa kwa kila mtu, na ambao utawawezesha Watanzania kunufaika nao, kwani, baada ya miaka tano ya kwanza, kampuni (jina lililopendekezwa ni MetroDar) itaanza kuwekeza hisa zake kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, ambapo kila atakeyependa ataweza kununua na kuwa mmojawapo wa wamiliki wa MetroDar?

Kwa yeyote atakayeweza kuufikisha ujumbe huu kwa Waziri Magufuli, basi, aufikishe, mimi niko tayari. Nikihitajika, mtafuteni Maxence, atawapa namba zangu zote za simu!

Asanteni kwa kunisoma!

> Mwana wa Haki

-----------------
MwanaHaki ni mchumi, mtaalam wa TEHAMA, mwandishi wa habari wa kujitegemea, na mshauri-elekezi katika sekta ya TEHAMA na vyombo vya habari.
 
jyfranca

JF-Expert Member
Oct 3, 2010
297
7
Huyo Magufuli hana akili hata kidogo, suluhisho si kuwapa wakurugenzi amri watoe jawabu. Kwa Dar kutoa suluhu ni rahisi sana. Ukitaka kupunguza misongamano rahisi. Ongeza bei ya parking, kwa sehemu zote za posta, hii itafanya watu waache magari nyumbani watumie magari ya wengi (car pool). Pia njia nyingine apanue mji, waanze kutoa vibali vya majengo ya kisasa nje ya mji kama Boko, Mbagala, na Gongo la Mboto. Hamisha huduma za jamii ikiwepo baadhi ya wizara nje ya mji. Kwa nini asitafute njia pakawa na treni inazunguka mji hasa asubuhi na jioni. Mfano barabara ya G/Mboto, Morogoro na Ali Mwinyi? Au mpake tuunde tume itumie bilioni ndo tupate jawabu, ita watu kwenye mkutano wa wazi omba mawazo ya kila mmoja
 
Yote yanawezekana, lakini Serikali imesahau kwamba hili zaidi ni suala la SERA kuliko utendaji. Kwa mfano, kwa kuwa TEHAMA sasa inaruhusu (hasa kupitia mkonga wa taifa - fiber optics cable) mawasiliano ya uhakina na ya haraka, Serikali inaweza kujenga ofisi ndogo za wizara kwenye maeneo ambayo ni karibu na makazi ya wana-Dar, kwa mfano, Mbagala, Tegeta, Mbezi Luis, Kibamba, n.k. Zijijengwa "Government Clusters", kisha wakawekwa wafanyakazi ambao wanaishi karibu na hizo clusters, suala la kufunga safari kwenda mjini, ati unaenda Wizara ya Afya, Ardhi, Fedha, n.k. litaondolewa. Wale watakaokuwa wanaenda mjini watakuwa labda ni wafanyakazi wa idara nyeti za serikali au kampuni binafsi, na wateja wao watakuwa wanapata huduma hizo kwenye "cluster" offices! Hili ni suala la "resource management", ambalo mimi nimelisomea huko Marekani! Nina uhakika na ninalolisema!

Ni rahisi zaidi kuweka "government clusters" kuliko kuendelea na mfumo huu mbovu wa daladala na huo mbuvu zaidi wa DART! Magufuli si mjinga wala mpumbavu; HAJAPATA WA KUMSHAURI!
 
Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,745
7,757
Waungwana,

Naomba kuwauliza. Hivi ni kweli kwamba Mhe. John Pombe Magufuli (MB, CCM, Chato) ametamka kwamba amewapa wakurugenzi wa idara mbali mbali za Wizara ya Ujenzi kutatua zengwe la foleni Jijini Dar es Salaam kwa muda wa MWEZI MMOJA tu? Sidhani kama, kwa akili ya kawaida, hili linawezekana. Hebu tuangalie kinachowezekana.

Asanteni kwa kunisoma!

> Mwana wa Haki

-----------------
MwanaHaki ni mchumi, mtaalam wa TEHAMA, mwandishi wa habari wa kujitegemea, na mshauri-elekezi katika sekta ya TEHAMA na vyombo vya habari.

Huyo Magufuli hana akili hata kidogo, suluhisho si kuwapa wakurugenzi amri watoe jawabu. Kwa Dar kutoa suluhu ni rahisi sana. Ukitaka kupunguza misongamano rahisi. Ongeza bei ya parking, kwa sehemu zote za posta, hii itafanya watu waache magari nyumbani watumie magari ya wengi (car pool). Pia njia nyingine apanue mji, waanze kutoa vibali vya majengo ya kisasa nje ya mji kama Boko, Mbagala, na Gongo la Mboto. Hamisha huduma za jamii ikiwepo baadhi ya wizara nje ya mji. Kwa nini asitafute njia pakawa na treni inazunguka mji hasa asubuhi na jioni. Mfano barabara ya G/Mboto, Morogoro na Ali Mwinyi? Au mpake tuunde tume itumie bilioni ndo tupate jawabu, ita watu kwenye mkutano wa wazi omba mawazo ya kila mmoja

...sasa, kama nyie mmetoa mapendekezo kwa haraka namna hii, kwanini iwe ngumu kwa hao waliopewa jukumu washindwe within a month?
 
Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,535
5,928
Wakiweka Taa za barabarani na kupana kidogo sehemu za Makutano ya barabara, foleni zitapungua.

Siku zote hapa ndipo foleni huanza.
 
jyfranca

JF-Expert Member
Oct 3, 2010
297
7
Ni wabishi kuelewa na wanaona ufahari kwa mji kuonekana mzuri posta tuu. Kwa masuala ya benki wanajitahidi kuyapeleka nje ya mji, lakini haitoshi, izi huduma za jamii kama maji, umeme, afya, elimu zipelekwe mitaani wanakokaa wananchi. Kwa nini mtu anakaa Sinza aamue kwenda Posta kisa ana tatizo la kwenda kusahihi bili yake ya maji. Tatizo hawa viongozi wetu bado wanapenda kukariri kila kitu. Kama wataamua kuongea na wananchi wa kawaida watapata suluhu kuliko kuajiri hata hao wasomi au wakurugenzi kutoa takwimu. Dar kila mtu anaona ufahari kuendesha gari kuipeleka posta wakati anajua kuegesha ngumu kupata. Ongeza pesa ya kuegesha, watu wataacha kupeleka magari posta.
 
Tundapori

JF-Expert Member
Aug 12, 2007
568
163
Mwanahaki,

Mawazo mazuri. Kuhusu monorail za kuendeshwa na computer, vipi swala la umeme wa tanzania? ni kweli mgawo utakuwa historia kama alivyosema Ngereja na monorail hizi ziweze kufanya kazi kwa ufanisi?

Nafikiri Serikali izinunue tu hizi generators za Dowans!!
 
MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
704
...sasa, kama nyie mmetoa mapendekezo kwa haraka namna hii, kwanini iwe ngumu kwa hao waliopewa jukumu washindwe within a month?

Kaka, ukinisoma vizuri, utajua kwamba NIMEFANYA UTAFITI kuhusu suala la MONORAIL. Si suala la siku moja wala la haraka. Nimefanya utafiti.

Awamu ya kwanza ni kuimarisha barabara za ndani, vitongojini. Awamu ya pili ni kujenga mtandao, awamu kwa awamu, wa monorail. Kazi itachukua miaka 10 kwa kiwango cha chini.

Si suala la haraka, lakini ni ufumbuzi. Nimelitafiti kwa zaidi ya muda wa miaka 7!
 
MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
704
Mwanahaki,

Mawazo mazuri. Kuhusu monorail za kuendeshwa na computer, vipi swala la umeme wa tanzania? ni kweli mgawo utakuwa historia kama alivyosema Ngereja na monorail hizi ziweze kufanya kazi kwa ufanisi?

Nafikiri Serikali izinunue tu hizi generators za Dowans!!

Soma vizuri hapo kaka. Umeme wa kuendesha monorail utakuwa HAUTEGEMEI umeme wa gridi wa TANESCO. Hatuwezi kuitegemea Serikali kuleta mfumo wa umeme wa uhakika! Ngeleja (si Ngereja) ALIKATAA mradi wa umeme kwa kutumia nishati ya upepo kwa kuwa (a) upepo haununuliwi, na (b) kwa kuwa haukuwa na maslahi binafsi kwake, kwani, wawekezaji wa mradi huo hawakutaka kutoa BAHASHA YA KAHAWIA kwake ili asaini mkataba wa uwekezaji huo. Ninao ushahidi. Sasa kama Ngeleja amezuia mradi wa umeme ambao ungeleta manufaa makubwa kwa taifa, mwaka 2006, LEO HII atatuambia kwamba kuna mwekezaji anakuja kutusaidia kumaliza matatizo yetu hayo, kwa MUUJIZA UPI? Au makubaliano yametimia? LOL
 
MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
704
Tafadhali, unaweza kuiweka 'Abstract' ya huu utafiti hapa?

Nilichoandika kwenye Main Post ndio "abstract"! Unataka kingine au wewe ndiye wale wanaosema kwamba WATANZANIA HATUWEZI, huku tukijua TUNAWEZA? Watu kama wewe MNATURUDISHA NYUMA KAKA!

Mimi nazungumzia maendeleo ya TAIFA, lakini naona wewe, kama jina lako lilivyo, INAKUCHOMA?! Kisa na mkasa?

Kama huna hoja ya msingi, usitupotezee muda! Tunaweza na mradi huu utakuwa BILA RIDHAA YAKO! Kwani wewe ni NANI?
 
Uongozi haujaribiwi.
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,683
8,208
...sasa, kama nyie mmetoa mapendekezo kwa haraka namna hii, kwanini iwe ngumu kwa hao waliopewa jukumu washindwe within a month?

Hivi nyie mnaotoa mapendekezo haya mmebobea fani ya highways? Au basi kila mtu ni lazima ashauri? Mliwapa Majembe Auctions kazi za highways Je, wana wataalam waliobobea hiyo fani? Tatizo la foleni hata Magufuli mwenyewe hafahamu linaweza kutatuliwa namna gani kwa njia za kitaalam. Yeye atawaita wataalam wamwambie kitu cha kufanya ambao wataletwa na serikali.

BTW mtasikia Japanese Co. kupitia JICA kama sikosei watapewa funds kufanya hiyo kazi lakini tatizo litabaki pale pale. Nina uhakika kabisa kuna Watanzania either ndani na nje ya nchi ambao wana uwezo kabisa wa kulitatua hili swala bila kukuru kakara za nguchiro na kenge.
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,556
3,102
hivi kwa kuanzia hizi reli zinazo pita toka wazo kwenda ubungo, mpaka stesheni haziwezi kusaidia, au toka Nyerere (pugu) road changombe kuja stesheni jingine ni affirmative action magari binafsi mjini marufuku ni public transport kwa kwenda mbele, kwa kuweka mabasi ya hiyo bei ndogo na kwa wale ma-excutive au wenye pesa zao nauli yao na mabasi yao bei juu, njia nyingine ni kuwepo na mabasi kwa kipindi cha peak hours yana simama vituo vikubwa vikubwa tu kwa bei kubwa kidigo sema toka ubungo -manzese- magomeni, cbe- posta mpya.
route nyingine posta ya zamani, mnazi moja- shule ya uhuru, ilala boma, bunguruni .
na wale wa vituo vidogo vidogo kuwe na mabasi madogo madogo (vipanya kuwa sogeza karibu watu wa vitu vya kati ya hivyo vikubwa, kwa bei nafuu kidogo ya hiyo vituo vikubwa. mfano kuna kuwepo na kipanya kati ya manzese na ubungo, na manzese na magomeni, na kwa sasa na hapo mbeleni wizara ya ardhi na wizara ya ujenzi wana takiwa wa shirikiane kwa kuwa karibu zaidi ili kuzui ujenzi hole , na kupokwa kwa viwanja vya wazi ambavyo vingeweza kusaidia parking, stendi ya mabasi, njia za reli nk.
na hata raisi mwenye dhamana ya kutoa open space awe anafanya hivyo kwa kushauriana na wataalamu, na kufikisha kwenye baraza la mawaziri, sio kwa sababu ana mamlaka basi anafanya anavyo jua yeye, au anavyo shawishiwa.
 
chamajani

JF-Expert Member
Sep 22, 2010
552
31
Soma vizuri hapo kaka. Umeme wa kuendesha monorail utakuwa HAUTEGEMEI umeme wa gridi wa TANESCO. Hatuwezi kuitegemea Serikali kuleta mfumo wa umeme wa uhakika! Ngeleja (si Ngereja) ALIKATAA mradi wa umeme kwa kutumia nishati ya upepo kwa kuwa (a) upepo haununuliwi, na (b) kwa kuwa haukuwa na maslahi binafsi kwake, kwani, wawekezaji wa mradi huo hawakutaka kutoa BAHASHA YA KAHAWIA kwake ili asaini mkataba wa uwekezaji huo. Ninao ushahidi. Sasa kama Ngeleja amezuia mradi wa umeme ambao ungeleta manufaa makubwa kwa taifa, mwaka 2006, LEO HII atatuambia kwamba kuna mwekezaji anakuja kutusaidia kumaliza matatizo yetu hayo, kwa MUUJIZA UPI? Au makubaliano yametimia? LOL

tafadhali ban mwanahaki, ebu eka huo ushahidi tushuhuie! How openly speak is?
 
popiexo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
742
180
Soma vizuri hapo kaka. Umeme wa kuendesha monorail utakuwa HAUTEGEMEI umeme wa gridi wa TANESCO. Hatuwezi kuitegemea Serikali kuleta mfumo wa umeme wa uhakika! Ngeleja (si Ngereja) ALIKATAA mradi wa umeme kwa kutumia nishati ya upepo kwa kuwa (a) upepo haununuliwi, na (b) kwa kuwa haukuwa na maslahi binafsi kwake, kwani, wawekezaji wa mradi huo hawakutaka kutoa BAHASHA YA KAHAWIA kwake ili asaini mkataba wa uwekezaji huo. Ninao ushahidi. Sasa kama Ngeleja amezuia mradi wa umeme ambao ungeleta manufaa makubwa kwa taifa, mwaka 2006, LEO HII atatuambia kwamba kuna mwekezaji anakuja kutusaidia kumaliza matatizo yetu hayo, kwa MUUJIZA UPI? Au makubaliano yametimia? LOL

Mwanahaki hebu weka hapa huo ushahidi ili tuweze kujadili kwa uhakika zaidi, la sivyo mtake radhi Ngereja
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom