Ninapojiuliza kuhusu waafrika na kuumia sana

Halitafakariki hili...

Pamoja na kua inauma hili halina nafasi yake kwenye siasa za Tanzania
Kwa wale wanaotaka kuamini na kudekeza hayo yaliyoandikwa, atabakia kama alivyo!

Kwa wale watakao kubaliana na mimi kuwa huyo mwandishi mwenyewe alihitimisha kuwa 'hao waafrika' hawata soma hilo, linatubakisha kwenye kundi tofauti kabisa ...kwani tumesoma na tunaweza kuchambua pumba zake elekevu kwa walengwa wasiolengeka!

Hivyo kama umesoma, hautabakia kwenye kundi hilo analodai mwandishi.

Kusudi kubwa, la mwandishi huyo, kwa maoni yangu ni la kichochezi kutaka kutafuta mdahalo, ambao upo na unajadiliwa kila kukicha na wadau. Hivyo kumbakisha kwenye kusudi lisilo na mwelekeo maalum!


Hakuna jipya analolisema pamoja na madai lukuki aliyoambatanisha.

Mie huwa "Ninapojiuliza kuhusu Waafrika...." Nafurahi sana! Kwani Afrika ndio mama wa fikra zangu.
Ahsante
Syllogist,
Mi nakubaliana na wewe kabisa. Napinga dhana kwamba sisi waafrika/watu weusi tuko duni kiakili tukilinganishwa na watu weupe. Hakuna uhusiano wowote wa lazima kati ya weupe/weusi na umakini/uduni. Nashangaa kuona baadhi wameongea kwa conviction kabisa kwamba mtu mweusi ni duni mbele ya weupe. Ajabu!

Kusema mtu mweusi ni duni maana yake ni ku-affirm kwamba si mtu kamili, ni mtu nusu kwani mtu kamili ni yule mwenye akili na utashi. Aliye na uwezo wa kutumia faculties zake kuyatawala mazingira yake na kuubadili ulimwengu. Siamini kwamba sisi waafrika ni watu nusu, na kwamba wazungu ni watu kamili. Kushikilia mawazo haya ni kujidhalilisha na kuogopa kuukabili ulimwengu.

Mwafrika ni mwerevu kama watu wa race nyingine. Mwandishi anaposema kwamba watu weusi ni WAJINGA, WALAFI (greed) na WABINAFSI kwa hakika hajaongea cha PEKEE kinachomtofautisha mwafrika na watu weupe. Kama ni ujinga, hakuna anayezaliwa na maarifa. Wote tunazaliwa tukiwa tabularasa. Tunaanza kupata maarifa kwa milango 5 ya fahamu.

Mwandishi anasema waafrika hawasomi vitabu. Ajue kwamba kusoma vitabu ni njia mojawapo ya kujipatia maarifa. lakini ziko njia nyingi tu kama za informal education, "kusoma" kwa kutazama na kuelewa mambo, kwa kusikiliza, nk. Pengine hatujatumia sana njia kusoma vitabu. Lakini hii ni kwa sababu ya mazingira yanayowanyima wengi nafasi ya kusoma vitabu. Kumbe mwandishi anaposema tu wajinga na si wapumbavu sioni kama ni kitu kibaya sana kwa sababu mjinga anafundishika (he has the potentials to be knowledgeable). Mpumbavu ni yule asiyefundishika kwa sababu hana uwezo wa kupokea maarifa. Si tuna uwezo wa kupokea maarifa.

Mwandishi anasema weusi ni watu WABINAFSI. Wote (all races) tunazaliwa na ubinafsi (umimi . . . wenye lengo la kujilinda for survival). Lakini jinsi tunavyokua na malezi tunayoyapata tunaanza kuushinda ubinafsi na kutoa nafasi kwa watu wengine. Tunajifunza kujinyima kidogo kwa ajili ya wengine.

Hakika ubinafsi si wa mwafrika tu. Mzungu ni mbinafsi zaidi kuliko mtu mweusi na ndiyo maana amejenga taratibu za kibinafsi katika kufaidi mali ya dunia hii. Fikiria juu ya ubepari, ukolonimamboleo, utandawazi, nk. Kama waafrika wanakuwa wabinafsi ni kwa sababu WAMEIGA na WANAENDELEA KUIGA mifumo ya kimagharibi ya watu weupe. Kwa sababu kutokana na malezi yetu ya tangu zamani waafrika tumefundishwa kuwa wakarimu, kuwa WAJAMAA. Na ndio maana Tanzania tulijaribu kuujenga ujamaa, kitu ambacho hakikuwa kipya kabisa kwa waafrika. Ulishindwa kwa sababu ya athari za kimagharibi na hasa MAWAKILI watanzania wa mfumo wa kimagharibi wakishirikiana na watu wa magharibi.

Mwandishi amezungumzia greed (labda Ulafi - kisw.). Wazungu ndo walafi wa walafi. Waafrika tunajua starehe na anasa kuwazidi wao? Siamini kabisa.

KUMBE kusema waafrika tu WAJINGA, WALAFI NA WABINAFSI kana kwamba ni SIFA za PEKEE kwa waafrika tu SI KWELI. Ndiyo nakubali wapo baadhi ya waafrika/watu weusi wenye kasoro hizi kama walivyo baadhi ya weupe wenye kasoro hizo pia. Lakini kusema waafrika wote ndivyo walivyo ni ku-generalise mno na kukosa breki katika conclusions. Mbaya zaidi ni kule kusema kwamba kasoro hizi ni inborn yaani tumezaliwa nazo kama race (weupe hawana), ni sehemu ya hulka yetu ndani ya damu, mifupa, genes na cells. Hii si kweli!! Kusema hivo ni kukataa dynamism of the human being. Mwafrika ni mtu anayebadilika kama watu wa race nyingine, anaelekea kuzuri. Kama kuna kasoro ni za kimazingira, ambazo hata kwa hao wazungu zimekuwepo kwani si weupe wote wameendelea kwa wakati mmoja na kwa namna moja. Hata wao wamepishana. Sasa utasema kwamba hao walio nyuma wamezaliwa na kasoro kutoka matumbo ya mama zao? Nawasilisha.
 
Naona mtu mmoja kaja na some hoax literature wasio na upeo wanakuja na self loathing innuendos.Hizi tunazijua, zipo kwa weakhearts wote, hata wazungu wapo self loathing, ila afadhali wao wana justification za ubaya wa wazungu wenzao, lakini hakuna cha ku justify self loathing.

Katika waafrika hakuna wabaya? Of course wapo.Waafrika ni wabaya/ wajinga naturally? Of course not, mtu mbaya/mjinga tu ndiye anayeweza kufanya hii gross justification. Hapa kuna saratani ya uvivu wa kufikirin a haraka ya kupatia maswali mazito majibu rahisi, maswali ambayo hata volumes za pages 500 haziwezi kuyafanyia justice yanakuwa dismissed na vimisemo mbuzi vilivyoself defeating na pessimistic kama "Waafrika Ndivyo Tulivyo".Vimsemo vyenye generalization zinazo suggest kwamba matatizo yetu waafrika wote yapo katika DNA zetu, bila kuangalia geografia, historia na mambo mengine mengi.

Sitaki ku sound kama apologist wa incompetency inayofanya Afrika kubaki nyuma ya -wachilia mbali ulaya ambayo kujilinganisha hakutakuwa sawia, bali hata nchi kama Korea Kusini na Pakisatan Malaysia, ambazo tulikuwa nazo sawa wakati wa uhuru-.Matatizo yetu Afrika ni uongozi, na kama kuna kitu kimoja wananchi wa Afrika tunaweza kubeba lawama ni kuuruhusu uongozi mbovu huu kuendelea.

Lakini unaposema "kuuruhusu" mara nyingine unakuwa kama vile una mlaumu mhanga, kwa maana tulipopata uhuru Africa ilikuwa vastly un-urbanized, vastly underemployed, vastly illiterate, kwa hiyo tulitengeneza ka class kadogo tu ka watawala waliokuwa wanajitwalia "matunda ya uhuru" na kuwaacha wengine wote kwenye umaskini mkubwa -ikiwa ni pamoja na kuwakosesha elimu na hudumajamii zote bora- kwa hiyo kuwalaumu watu hawa ambao hawakuwa na elimu wala nguvu za kisiasa inakuwa si sawa.

Ndiyo kwanza tunapata muamko wa kisaiasa wa kweli kudai accountability kutoka hii second colonialism, ambayo ni ngumu zaidi kuitoa kwa sababu mkoloni ni "ndugu yetu" mweusi, isitoshe katika hao hao wanaojituitumua kupigia kelele wananchi kuna ma false prophets kina Chiluba types kibao.


I am currently enjoying Richard Dowden's "Africa:Altered States, Ordinary miracles" which seems to reinforce my notion that these problems are far more complex than the idiocracy of "Waafrika Ndivyo Tulivyo" would allow.

Moja ya matatizo makubwa yanayotukabili waafrika ni kukosa self-consciousness na self-respect itakayoweza kutupa uwezo wa kusimama na kuyakabili matatizo yetu, characteristic mojawapo ni hizi generalizations za kukata tamaa along the lines of "Waafrika ndivyo tulivyo".

Kwa kweli mkuu umezungumza mambo ya msingi na mimi siku zote nasema nguvu tungeielekeza ktk kubadirisha uongozi. Matatizo ya waafrika ni uongozi mbovu na wala siyo mambo ya kusema waafrika ndivyo tulivyo. Hata wanaotoa maneno ya namna hii mimi huwa nasema wanakurupuka ku-generalize mambo.

Angalia nchi kama china wanavyo pambana na rushwa na uongozi mbovu, nahii ndi ilikuwa kinga ya kulinda uchumi wao lakini ukisha ruhusu hawa watu wa magharibi (marekani na ulaya) basi watakuwa wakikuyumbisha kila mara.

Huu upumbafu wote eti free market, globalizaton etc. ni janja ya hawa wahuni (wazungu) kutuhadaa tu ili wachote mali zetu. Sasa kwa kuwa tuna uongozi mbovu wa kina mkapa basi unauza kila kitu na pesa unaweka mfukoni.

Mbona wahindi sasa hivi wanaendelea? Lakini kaangalie walivyo wakali kwenye ukusanyaji wa kodi, wala hakuna eti mwekezaji anapewa muda wa miaka 5 ya kuangalia hali ya biashara, hakuna!! hiyo utaikuta Tanzania tu. Wao wanasema huwezi kufanya biashara ondoka.

Hoja ya msingi hapa ni "tubadili mfumo wa uongozi" na maendeleo yatapatikana.
 
Kama ukisoma kwa makini literature inayohusu mtu mweusi utafurahi sana. Naona mpaka sasa ni mtu mmoja tu anaeilewa naye ni Nyani Ngabu. Mimi naungana lwa asimilia 100, kuwa miafika ndivyo tulivyo.
Obssed with sex...which is true
excessive use of alcohol...ukweli
kupenda kujionesha kuwa anavaa vizuri kichwani sifuri...ukweli
ubinafsi---KWELI
wizi....angalia kama kuna mtu haaibia serikali, ukienda nyumbani utakuta vitu kibao vya ofisini
they very loud.....ukweli mtupu
wanajifanya wajaua kila kitu wakati hata city ndogo hawawezi kujenga...ukweli mtupu
wanaharibu nchi zao wenyewe halafu wanapenda za wengine..........ona tunavyokata miti ovyo, kuua wanyama wetu na kuuza mano ya tembo etc etc
Wavivu wa kazi.....siwezi kusema zaidi nina mifano 1000
Wapenda kupiga domo.............kazi sifuri
Ni wabunifu sana kwenye mambo ya uharibufu............very true(hii inaonesha si wajinga)
Extravangants------angalia msafara wa Gordon Borwn ulinagnishe na wa Pinda
Wavivu wa kufikiri...........Mkapa ameconfirm hilo, na ametuonesha kweli
They can not manage themselves........miaka zaidi ya 40 ya uhuru inathibitisha

Kama ni kweli unauliza swali hili ndugu yangu, inabidi ujikaze sana wasiliana na Nyani Ngabu anajua vizuri sana.

Inaonekana baadhi ya mnaochangia na mlio changia in favour of the article basi mna matatizo. Unasema waafrika ni wabunifu sana wa mambo ya uharibifu, je, ndoa za jinsia moja kaleta mzungu au mwafrika??

Unasema mkapa pia ka-confirm kwamba waafrika ni wavivu wa kufikiri. je, yeye kujimilikisha mgodi wa kiwira ndo mwepesi wa kufikiri??

Wakati mwingine mchangie kwa hoja za maana siyo kushabikia tu. Ninyi wenyewe pengine mko kwao wazungu mnabeba box ndo maana mnawapamba eti wao siyo wajinga ili hali mijinga mizungu ipo kibao.
 
Inaonekana baadhi ya mnaochangia na mlio changia in favour of the article basi mna matatizo. Unasema waafrika ni wabunifu sana wa mambo ya uharibifu, je, ndoa za jinsia moja kaleta mzungu au mwafrika??

Unasema mkapa pia ka-confirm kwamba waafrika ni wavivu wa kufikiri. je, yeye kujimilikisha mgodi wa kiwira ndo mwepesi wa kufikiri??

Wakati mwingine mchangie kwa hoja za maana siyo kushabikia tu. Ninyi wenyewe pengine mko kwao wazungu mnabeba box ndo maana mnawapamba eti wao siyo wajinga ili hali mijinga mizungu ipo kibao.

Ndio maana nasema kwenye mijadala kama hii Nyani Ngabu anafunga mabao bila ya yeye ku-type anything.

Imani na ability ya kufanya vitu ni viwili tofauti. Kukataza au kuruhusu ndoa ya jinsia moja ni masuala ya kiimani lakini sio uharibifu.
 
Ndio maana nasema kwenye mijadala kama hii Nyani Ngabu anafunga mabao bila ya yeye ku-type anything.

Imani na ability ya kufanya vitu ni viwili tofauti. Kukataza au kuruhusu ndoa ya jinsia moja ni masuala ya kiimani lakini sio uharibifu.

Tatizo watu wanaobisha kuwa Waafrika Sivyo Tulivyo wanabisha kwa kutumia maneno tu. Na kama tunavyojua, talk is cheap. Wote tunaweza kuongea. Laiti matendo yetu Waafrika yangelingana na maneno yetu tungekuwa mbali sana. Pengine watoto wetu wasingekaa chini kwenye sakafu shuleni. Pengine watu wetu wengi wasingekuwa wanaishi kwenye nyumba za udongo...
 
Wakati mwingine mchangie kwa hoja za maana siyo kushabikia tu. Ninyi wenyewe pengine mko kwao wazungu ....mnawapamba eti wao siyo wajinga ili hali mijinga mizungu ipo kibao.

Slow down!

Wengi walio kwenye kundi la "waafrika ndivyo walivyo" ukiwapeleka ng'ambo hakika mtazamo wao utabadilika. Nina hakika ya hilo, atakayebisha hana mifano hai.
Yule ambaye yuko ng'ambo bado akawa na mtizamo huo wa "ndivyo tulivyo" ...muombee kwa Mola. (Siku hizi kuna kila aina ya unga ati, huko ng'ambo!)
 
Tatizo watu wanaobisha kuwa Waafrika Sivyo Tulivyo wanabisha kwa kutumia maneno tu. Na kama tunavyojua, talk is cheap. Wote tunaweza kuongea. Laiti matendo yetu Waafrika yangelingana na maneno yetu tungekuwa mbali sana. Pengine watoto wetu wasingekaa chini kwenye sakafu shuleni. Pengine watu wetu wengi wasingekuwa wanaishi kwenye nyumba za udongo...

Nyani,

Naona tatizo ni hii linear thinking ya kwamba Waafrika either ndivyo tulivyo or sivyo tulivyo

Hakuna option ya kuweza kuona kuwa Waafrika ni complex na wana defy hii oversimplification, kwamba si ndivyo tulivyo wala si sivyo tulivyo, in fact hata si either ndivyo tulivyo or sivyo tulivyo.

Hao waafrika wenyewe tu definition yao complex, je utawajumuisha wakaskazini kule kina Misri, Libya, Algeria Tunisia na Morocco?

Vipi kuhusu "Waafrika Weupe" wa South Africa?

Vipi kuhusu visiwani -Mauritius, Seychelles,Madagascar, Comoro, Cape Verde, Sao tome and Principe etc-, utawahesabu nao, kama ndiyo kwa nini, kama sivyo kwa nini?

Vipi waafrika waliokaa nje kwa generations?

Kama muafrika kum define tu kazi, unapata wapi audacity ya ku generalize kwamba Waafrika wako hivi
 
Vipi kuhusu "Waafrika Weupe" wa South Africa?

Hao Waafrika weupe wa Afrika Kusini tunajua wametoka wapi na umeona umuhimu wa wao kuwepo huko Afrika Kusini. Leo hii Afrika Kusini ndio super power ya Afrika. Mwakani wana host kombe la dunia. This is not an accident Bluray....you know it ain't.
 
Hao Waafrika weupe wa Afrika Kusini tunajua wametoka wapi na umeona umuhimu wa wao kuwepo huko Afrika Kusini. Leo hii Afrika Kusini ndio super power ya Afrika. Mwakani wana host kombe la dunia. This is not an accident Bluray....you know it ain't.

Are you neglecting the historical factors?

The plunder and the pillage, the looting and the shooting, Sharpeville and Soweto.Robben Island and countless other injustices.

Are those really the marks of intelligence?
 
Are you neglecting the historical factors?

The plunder and the pillage, the looting and the shooting, Sharpeville and Soweto.Robben Island and countless other injustices.

Are those really the marks of intelligence?

They are marks of injustice....no doubt. But marks of intelligence are galore.
 
They are marks of injustice....no doubt. But marks of intelligence are galore.


An intelligence based on injustice is intellectually inferior to a mediocrity based out of justice.

And thats an original Bluray gem.
 
Waafrika Ndivyo Tulivyo.....

You cannot analyze a situation you cannot transcend, kama wewe ume resign kwamba "Waafrika ndivyo tulivyo" - obviously including yourself in this rather tired observation- what makes you think that you are qualified to look from a position that transcend that situation and make a meaningful observation?

Ni kama vile unasema mimi kipofu tangu nilivyozaliwa, halafu unataka kubishana kuhusu rangi.
 
You cannot analyze a situation you cannot transcend, kama wewe ume resign kwamba Waafrika ndivyo tulivyo" - obviously including yourselfin this rather tired observation- what makes you think that you are qualified to look from a position that transcend that situation and make a meaningful observation?

Ni kama vile unasema mimi kipofu tangu nilivyozaliwa, halafu unataka kubishana kuhusu rangi.

Upofu na Ndivyo Tulivyo havilingani. Njoo na analogy nyingine.
 
Tatizo watu wanaobisha kuwa Waafrika Sivyo Tulivyo wanabisha kwa kutumia maneno tu. Na kama tunavyojua, talk is cheap. Wote tunaweza kuongea. Laiti matendo yetu Waafrika yangelingana na maneno yetu tungekuwa mbali sana. Pengine watoto wetu wasingekaa chini kwenye sakafu shuleni. Pengine watu wetu wengi wasingekuwa wanaishi kwenye nyumba za udongo...

Mkuu nakuunga mkono. Mpaka leo ukiwauliza kaka zetu wanasema mkoloni alikuwa mshenzi sana, lakini wote wanasema walikuwa na discpline kwenye kazi hata walikuwa na heshima fulani kwa waliokuwa wanawatawala. Pamoja na kuwa walikuwa savages like wakawafundisha kuvaa suti,tai viatu na kuendesha magari, still walikuwa wanwaheshimu kiasi. Hata mishahara waliyokuwa wanawalipa wakata mkonge ilikuwa inatosha kwa mwezi na nusu, hebu angalia mtawala wetu wa sasa.
Ukiangalia shule alizojenga mkoloni hadi leo zinaonekana shule, hebu ngalia shule nilizojenga mimi na masanja, inaanza kubomoka hata kabla haijaisha.
Angalia yule daktari mmoja aliyefundishwa na mkoloni, na uangalie hawa 1000 tuliowafundisha sisi, unaweza kucheka.
Tuna hela kuliko ilivyokuwa serikali ya mkoloni, lakini tunashindwa kuijenga Tanzania hata nusu ya alivyofanya mkoloni. Kwanini tusubishe kuwa ndivyo tulivyo?
Waafrika, hasa wa Tanzania ni hodari kweli kuongea. Ukiangalia ilani ya CCM inaweza kuwa best hata kuliko ya Republicans, lakini inatekelezwa vipi hadi utacheka......na watu kila siku wanadanganywa wanakubali. Ndivyo tulivyo.

Mpaka leo tunaimba eti mkoloni ametufanya tuwe maskini, uongo mtupu. Nchi ngapi zimetawaliwa na zimepiga hatua.
Tanzania ikiwa na viongozi serious, wenye vision TAnzania inaweza kuwaprove watu wrong kuwa ndivyo tulivyo. Lakini kwa style ya sasa, hata miaka 1000 hakuna la maana litakalotokea. Ndivyo tulivyo.
 
Upofu na Ndivyo Tulivyo havilingani. Njoo na analogy nyingine.

Ndivyo tulivyo ina imply deficiency, that we are inherently inferior.

Upofu nayo equally ni deficiency, a condition of impaired vision.

There goes the analogy.

Huwezi ku discuss complexities za matatizo ya Africa (rangi) wakati wewe mwenyewe umo katika mentality deficient ya "Ndivyo Tulivyo" (upofu wa kuzaliwa).
 
Back
Top Bottom