toplemon
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 4,581
- 4,631
Mimi ni mwanaume ambaye ninavumilia mambo sana na kuyatafutia utatuzi kwa namna yoyote ile.
Ila kuna wakati mambo yananifika na kuniumiza sana hadi najikuta nakata tamaa au jambo baya linanifika au taarifa mbaya hapo unachanganya na shida za dunia.
Huwa najikuta nalia sana na nikiwa mwenyewe nitalia weee hadi nitaona kabisa kwa sasa inatosha na hii imekua siri yangu.
Nikikumbwa na madhila ya dunia nitajikaza na kuonyesha ukakamavu mbele ya hadhira kwamba ninalimudu na nina roho ngumu na watu wanaamini hivyo lakini nikishaondoka hapo nikifika sehemu nipo mwenyewe tu hususan usiku nitalia mno kwa lile jambo.
Kiukweli napenda kulia sana, tena sana tu, lakini nikiwa mwenyewe tu ndani huko hii imekua kama njia yangu ya kupunguza machungu.
Hata nikikaa na rafiki yangu mfano katoka safari kaja tumekaa wote tumeshazoeana kama zamani na kampani nk...aisee siku akiondoka kuna uwezekano mkubwa sana kulia au hata mtu wangu wa karibu niliyemzoea ananipenda na kunithamini siku akiondoka na ukute ndo harudi tena mimi machozi lazima yanitiririke humo nikiwa nimejifungia
Sijui unalizungumziaje kwa upande wako ndugu mwana JF?