Ninapenda aina ya uwasilishaji wa hoja na majibu wa Prof. Paramagamba Kabudi

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,635
29,967
Mfungo wa ramadhani umeanza vema uko,

Mtanzania mwelevu atakubaliana na mimi kwamba professor kabudi ni makini na mara nyingi akiwa anafanya uwasilishaji wa hoja au kujibu swali haishii hapo , anatoa somo kabisa, ninapenda sana aina yake ya uwasilishaji,
Unaweza kunibishia hapa kwa mihemko lakin ukiwa peke yako sikiliza uwasilishaji wake katika hoja mbali mbali, maeneo mbali mbali anapokuwa anatolea maelezo,

Ninahisi tumetakiwa kuwa na aina ya watu kama hawa wengi katika sekta zinazotaka maelezo,

1. Sikiliza hapa wakati wa ufafanuzi wa sheria ya ndoa

2. Msikilize hapa pia

Uwasilishaji huo unanikumbusha wa mheshimiwa sospeter muhongo kipindi akiwa waziri wa nishati

Maana wote wana majigambo ya kujua wanachowasilisha kujua ni raha sana ,hakuna raha kama kuwasilisha kitu na kuwa na uelewa juu ya kujua vitu ambavyo unawasilisha,

Pia uwasilishaji huo unanikumbusha Magufuli akiwa bado Magufuli kule bungeni, mwenye data za kutosha kichwani na mwenye kujiamini anapotoa ufafanuzi wa jambo,

Kwa upande wa upinzani, mheshimiwa Tundu Antipass Lissu akiwa anawasilisha hoja yake ni lazima uwe na shauku ya kumsikiza kwa makini

Waliobaki kina zitto sina uhakika naye,

Heko Mr Kabudi
 
Mtanzania mwelevu atakubaliana na mimi kwamba professor kabudi ni makini na mara nyingi akiwa anafanya uwasilishaji wa hoja au kujibu swali haishii hapo , anatoa somo kabisa, ninapenda sana aina yake ya uwasilishaji,
Unaweza kunibishia hapa kwa mihemko lakin ukiwa peke yako sikiliza uwasilishaji wake katika hoja mbali mbali, maeneo mbali mbali anapokuwa anatolea maelezo,
Na hapo ndio tatizo lake litakapo anzia. Mwenzake Muhongo alikuwa na style inayo fanana na hiyo tena yeye alikuwa anajigamba kwamba ni mwana sayansi akasahau yuko kwenye kilinge cha siasa hadi yalipo mkuta wanasiasa wale wakamkaanga (2X). Sasa huyu anapitiliza kutoa somo, nakuambia wanamsubiri tu siku ikifika watamtenda. Huwezi ukaongea na watu wazima tena wanasiasa ukawa unawaona kama wanafunzi. Binafsi hainipi shida sana lakini hao wenzake wanamlia timing tu.
 
Kama alidiriki kusema kuwa katiba si kipaumbele kwa sasa wakati alishiriki katika tume ya Warioba utamwelewa huyo??!!
Yapo ya kiuchumi na ni mengi na muhimu kuliko hizi siasa za kukaa kwenye bunge maalum la katiba halafu inatumika pesa nyingi na watu wanaishia kuwaita wenzao intarahamwe.

Mkuu hizi siasa hazina maana sana kulinganisha na ujenzi wa treni ya umeme kutoka Dar mpaka Rwanda. Kulinganisha na ongezeko la utalii, kulinganisha na ongezeko la mikopo kwa wanafunzi wa elimu za juu.

Umasikini wa Afrika huchangiwa kwa kiasi kikubwa na hizi mbwembwe za wanaharakati kudai katiba mpya kana kwamba kuna kifungu cha kikatiba kinachozuia ubunifu wanaopaswa kuwa nao vichwani mwao.
 
Ndugu yangu hii nchi imekwama hapa kutokana na katiba mbovu hii tuliyonayo.
Nchi nyingi zilizoendelea katika mfumo wa demokrasia ni Kwa sababu ya katiba nzuri.
Yaani hatuwezi kuendelea na hili likatiba letu hili la hovyo eti kuna kipengele kinasema kutakuwa na Baraza la mawaziri ambalo ndio litakuwa mshauri mkuu wa rais halafu hilohilo likatiba linakipengele linasema eti rais hatalazimika kusikliza ushauri wa mtu yeyote. Halafu Ikulu kuna watu eti washauri wa rais.
Katiba kabisa inaelekea eti rais hawezi kushtakiwa, usenge mtupu . Ndio maana wanafanya mambo ya kipuudhipuudhi kama ya Mkapa kujibinafsishia mgodi wa makaa ya Mawe kiwira.
Katiba inampa mamlaka makubwa Rais ya uteuzi na kumfanya kuteua baadhi ya watu wa hovyo kama kina bashite kuwa viongozi, nchi iendelee wapi.
Majirani zetu Kenya wataendelea kutuacha sana Kwa sababu ya katiba yao nzuri na yenye kueleweka.
Ni kwamba umasikini Kwa raia wengi wa nchi nyingi za Afrika Tanzania ikiwemo huku viongozi wachache tu wanasiasa wapiga domo wanakuwa matajiri kulipo wafanyabiashara wengi wanaohangaika usiku kucha
 
Hao wengine wasiopewa mamlaka na katiba mbona wamekuwa wakifanya madudu kila kukicha!!.

Walioiua ATC walifanya hivyo kwa sababu ya ubovu wa katiba!. Waliobinafsisha viwanda na kuviuza kwa bei ya kutupa walifanya hivyo kwa sababu ya katiba!.

Kenya ilikuwa nyuma yetu kwenye suala zima la lugha ya kiswahili lakini kwa sasa wanatuzidi, na hilo nalo ni la udhaifu wa katiba!.

Tunaendekeza uzembe halafu kisingizio chetu kila mara ni katiba mpya, hata tukiipata mpya bado ni kuna mambo ambayo kama yasipobadilika basi tutaishia hapa hapa.

Tunakubali kuwa incompetent kwenye kila sekta halafu matokeo yakiwa mabovu kimbilio letu ni katiba mpya.
 
Vedio sijasikiliza 'sina mb za kutosha' ila huyo waziri namkubali sana

Na mimi Prof Kabudi hunikumbusha Prof Muhongo
 
britanicca ,

..Prof.Kabudi alinivutia sana mwanzoni.

..lakini sasa hivi hanivutii tena.

..ujengaji hoja wa PROF.KABUDI ni rahisi kuzoeleka/PREDICTABLE.

..ana tabia ya kunukuu na kurejea BIBLIA.

..hilo ni kosa kwasababu shughuli za kiserekali haziongozwi kwa kutumia misahafu au maandiko ya kidini.

..Prof pia anazungumza mno, na matokeo yake "hupoteza mawasiliano" na misingi ya hoja anayoitetea.
 
Kuusifu ujinga ni zaidi ya ujinga. Kabudi huyuhuyu anayetetemeshwa na G. Lema hadi macho na povu kumtoka simultaneously?
 
kwa hakika na ukweli uliotukuka prof.kabudi paramagamba ni fundi wa kupresent vitu kuntu.namkumbuka tulipokuwa nkurumah hall pale udsm.
 
Yapo ya kiuchumi na ni mengi na muhimu kuliko hizi siasa za kukaa kwenye bunge maalum la katiba halafu inatumika pesa nyingi na watu wanaishia kuwaita wenzao intarahamwe.

Mkuu hizi siasa hazina maana sana kulinganisha na ujenzi wa treni ya umeme kutoka Dar mpaka Rwanda. Kulinganisha na ongezeko la utalii, kulinganisha na ongezeko la mikopo kwa wanafunzi wa elimu za juu.

Umasikini wa Afrika huchangiwa kwa kiasi kikubwa na hizi mbwembwe za wanaharakati kudai katiba mpya kana kwamba kuna kifungu cha kikatiba kinachozuia ubunifu wanaopaswa kuwa nao vichwani mwao.

Mkuu lakini mchakato wa katiba mpya si ulianzishwa na serikali yenyewe?! Kwani ulianzishwa na wanaharakati??!!

Kama walijua kuwa watautelekeza mchakato kabla ya kukamilika kwa nini wakatumia mabilioni ya pesa ambazo zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo?!
 
Mchakato aliuanzisha JK na ni yeye anayejua kwanini muda ule ulikuwa muafaka.

Wanasiasa wakauharibu kwa sababu ya ubinafsi wao na ni katika wakati ambapo fedha nyingi ilikuwa imeshatumika.

Muda ukawa umepotea bure, lakini bado mimi naamini katika kujituma kwetu kuliko kuitegemea katiba kama kisingizio cha umaskini wetu.

Rwanda ni udogo wake leo hii imeingia mkataba na Arsenal wa kuliweka jina la nchi hiyo kwenye mikono ya jezi ya timu hiyo ya London, jezi itakayotumika msimu ujao. Hapo kilichotumika ni ubunifu tu na wala sio masuala ya vifungu vya katiba.

Wafanyabiashara wa nje na ndani wanalalamikia kodi zisizo na vichwa wala miguu, ambazo zinakwaza maendeleo ya kibiashara. Hili wala halihitaji vifungu vya katiba kutambua namna ambavyo kodi nyingi zinavyoathiri ukuaji wa biashara.

Yapo mengi tu ambayo yanathibitisha namna ambavyo tatizo ni sisi wenyewe kutojua namna ya kubadilika ili tuendane na matakwa ya dunia ya sasa. Katiba mpya ni kisingizio tu cha umaskini wetu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom