Ninaomba wana jf tuijadili picha hii. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ninaomba wana jf tuijadili picha hii.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchonga, Nov 28, 2010.

 1. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Na Mwandishi wetu Happy
  Katika hali iliyoonekana kuwavutia watanzania wengi waishio nchini Urusi, Tawi la CCM Moscow limefanya sherehe ya kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Raisiwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni. Sherehe hiyo iliyoanza majira ya saa kumi na moja jioni ya tarehe 27/11 na kumalizika majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi ya tarehe 28/11 iliwavutia sii tuu watanzania waishio nchini Urusi na Maeneo ya jirani, bali pia natu wengine wasio watanzania.

  Miongoni mwa wageni muhimu waalikwa na Capt. Mstaafu Jaka Mwambi ambaye pia aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi Tanzania ikiwemo ukatibu mkuu msaidizi wa CCM Taifa. Mh. Mwambi katika htuba yake kwa wapenzi, wanachama na wakereketwa wa CCM waliohudhuria amesisitiza kuwa vijana sio tuu taifa la kesho, ila pia ni Taifa la Leo na la Keshokutwa. Mh. Mwambi amesema kuwa vijana wasifikirie kuwa kujiunga na chama ni kujinufaisha kifedha, bali ni kukomaa kimawazo na kisiasa na lengo kubwa ni baadae kuwatumikia wananchi na sio wananchi kuwatumikia.

  Mwenyekiti wa Tawi la CCM Urusi Dk. Alifred Kamuzora katika hotuba yake alihoji kuwa katika uchaguzi wa hivi karibuni, ambapo wapinzani wanadai matokeo yalichakachuliwa, isije kuwa wenyewe wanaotoa madai hayo ndio waliojichakachua wenyewe. Akisisitiza jambo, Dk. Kamuzora alisema Matokeo ya Uchaguzi kuanzia ya uraisi hadi wabunge na madiwani yalikuwa sio ya ubabaishaji na uchaguzi ulikuwa huru na, salama na Haki, hata taarifa ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Africana SADC walithibitisha hilo. Aither Dr. Kamuzora alisisitiza kuwa katika kipindi cha mwanzo cha uongozi wa Raisi Kiwete CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza ilani yake ya uchaguzi. Katika kauli mbiu ya CCM ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania, CCM imeweza kuboresha huduma za hospitali, kuongeza shule za msingi, shule za sekondari kwa kila Kata na hata vyuo vikuu nchini vimeongezeka kutokana na sera na Ilani ya CCM.
  Mengine ni uboreshaji wa mahakama huru, ambapo watanzania wameshuhudia hata watu waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini wakisimama kizimbani, uboreshwaji wa chombo imara cha dola, jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, na Jeshi la kujenga Taifa.
  Aidha, CCM imeweza kuboresha elimu, maji, umeme, barabara nk. hayo ndio maisha bora yanayozungumzwa.


  source: http://ccmmoscow.blogspot.com/2010/11/tawi-la-ccm-moscow-lafanya-sherehe.html
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hahahah sura zao zinaonyesha hao ni majuha!
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Inaelekea hata wao hawamtambui JK km ni rais mbona picha yake wamiharibu machoo:teeth::teeth::teeth:
   
 4. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu waambie hiyo picha ya rais imechakaa waibadilishe.
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Aibu ya mwaka kwa nyie wanywa VODKA huko urusi kusema uchaguzi haukuchakachuliwa wakati sisi tuliopo nchini tuliopiga kura tunasema ulichakachuliwa. Najua mnajipendekeza kwakuwa mmepata nafasi za upendeleo kwenda huko kusoma ndo maana mnatumia huo ujanja kujibu fadhila. Hivi hamjionei huruma kuwa hata huko mliko mnazurura mahotelini kufanya vibarua vya kuosha vyombo kwa ujira mdogo na wakati mwingine mnafagia barabara, kazi ambazo huku bongo wasomi piga ua hatukubali coz tunafanya kazi tulizosomea. Hamuwaonei huruma wazazi na ndugu zenu wanaozidi kuzama ktk dimbwi la umaskini kwa sababu ya ccm na jk wake nyie mnasherehekea. Ole wenu mrudi nyumbani muone moto mtakapotembea mwaka mzima na vyeti kwenye bahasha bila mafanikio kwa kuwa sera mbovu za ccm zimeshindwa kutengeneza ajira za maana kwa watz na nyie hamuepuki huu mtego hata mjipendekeze vipi....
   
 6. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Hao ni wakereketwa au ni baadhi ya hao hao mafisadi waishio hapo? Alichokisema Capt Jaka kina mashiko zaidi kwani wajue kuwa wanapaswa kuwatumikia wananchi na si wananchi wawatumikie wao....
  Hata hivyo inatia kichefuchefu kwa maneno yake haya ...''Mwenyekiti wa Tawi la CCM Urusi Dk. Alifred Kamuzora katika hotuba yake alihoji kuwa katika uchaguzi wa hivi karibuni, ambapo wapinzani wanadai matokeo yalichakachuliwa, isije kuwa wenyewe wanaotoa madai hayo ndio waliojichakachua wenyewe. Akisisitiza jambo, Dk. Kamuzora alisema Matokeo ya Uchaguzi kuanzia ya uraisi hadi wabunge na madiwani yalikuwa sio ya ubabaishaji na uchaguzi ulikuwa huru na, salama na Haki, hata taarifa ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Africana SADC walithibitisha hilo. Aither Dr. Kamuzora alisisitiza kuwa katika kipindi cha mwanzo cha uongozi wa Raisi Kiwete CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza ilani yake ya uchaguzi''haya ni maneno ya mtu asiyekuwa na hekima na sidhani kama huo uwenyekiti wa tawi hakika litakuwa tawi la wajinga wenzie!

  Kumbe wapo watanzania waishio nje ya Tanzania wanamawazo mgando kama haya? Inasikitisha sana!
   
 7. S

  Siao Member

  #7
  Nov 28, 2010
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mgando mgando...

  hata wao wanajua wanabembeleza vyeo... hawako serious!!

  mtu mweye akili timamu huwezi kufanya wanachofanya...

  ole wao watu wetu wa vijijini waliokwisha amka wajue ujinga huu hapa...
   
 8. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dr. FEKI hao ndio wakirudi huku wanatunyesha sumu wafie mbali.

  Wamepigwa bari hadi nyuso zimeganda, haya ndiyo tangu yazaliwe yana "gene za kutokuelewa" inherited genetically hayawezi kubadilika.

  Pia "VODKA" ZINAUA SANA THINKING CAPACITY.

  HUYO KAMUZORA HAELEWI CHOCHOTE na ukute wakati akihutubia alikuwa KESHA KATA KILAJI "VODKA"

  AKAWA ANATEMA KAM ZA babu YELSIN, merehemu mungu amrehemu.Amen

  Ila ngonjera za KAMUZORA inaonyesha jinsi gani ni MTU WA KUKARIRI.
   
 9. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,954
  Likes Received: 1,770
  Trophy Points: 280
  majuha hawa.....illiterates.....hawajui kuchambua maziwa na tui....nadhani kama walienda kupata elimu basi haijawasaidia kitu...wabaki huko huko hadi fikra mgando zitakapowaisha...nonsense n' hopless...mnatia kinyaa...wengine mnaonekana watu wazima...watoto wenu watarithi nini...mbaki huko huko na kizazi chenu chenye mawazo ya kufa...msije mkaongeza matatizo tanzania...
   
 10. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,806
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Mbona wanaonekana kuchoka na kukata tamaa ya maisha heheheh!:help:
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  This is what UWT can do best kuwa neutralise watanzania mlioko nje. specifically kwa ajili ya CCM. Tusiwashangae hawa tu wa Urusi hata huko UK USA, kuna matawi.

  Hatujawai kusikia watanzania wakimarch au kufanya demosntation kwenda ubalozi wa tanzania wakitaka serikali ishughulikie mafisadi.

  Wote wa tanzania wa nje na ndani .Tumebaki kuelezea hisia zetu electronically kupitia JF. SIku si nyingi na JF itakuwa chombo cha UWT.
   
 12. m

  mpingomkavu Member

  #12
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hear say, kwani hawakuona hata karatasi za kura zilikuwaje
   
 13. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tulioko nchini ndo tunajuwa kilichoendelea, wenyewe wako Urusi hata kura hawakupiga lakini kiherehere kibao. Kunyweni VODKA mlewe mkalale mkimaliza masomo ndo wa kwanza kukimbia nchi huku mmechukua mikopo ya kodi zetu.
   
 14. T

  Thesi JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Imekuwa ni mtindo kwa watanzania wenye uroho wa madaraka waishio nje kujitambulisha kama wanachama wa chama cha mapinduzi CCM kwa kuwa ndiyo ina dola na inamilki serikali ili iwe rahisi kwao kuingizwa kwenye system wakirudi. Eti kwa kuwa wako nje wakija waonekane ni watu muhimu wa wanaoipenda CCM. Hii inadhihirisha tabia mbovu tu ya mwafrika ya kupenda ulafi na njia rahisi kwenye maisha.

  Hao ni manyan'gau kama manyan'au au mafisadi wa bongo wanajiandaa kunywa damu zetu ila kabla hawajafanya hivo mtanzania mzalendo wa kweli kama Dr Slaa watakuwa wamatukomboa na hao mafisi wa CCM na hao wanafunzi wa nchi za nje wanaonusa harufu ya damu yetu na wanatamani wapewe wanywe wakimaliza hizo degrii zao feki zisizowakomboa kuwa wazalendo na kupigania baba na shangazi zao maskini kijijini na badla yake wanataka wawanyonye hao hao maskini.
  Mmelaaniwa na namwomba shetani awatangulie vyema mtafune hadi kokoto na huo ulafi wenu wa kunywa damu zetu kama fisi na mfe kwa taabu. Amen
   
 15. m

  magesa jr Member

  #15
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pumba tupu. Wabongo ni wepesi wa kukosoa na lawama tu lkn hakuna vitendo.
   
 16. zoeca

  zoeca Senior Member

  #16
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  waongo wakubwa jk mwenyewe wamemchana macho kuonyesha ukipofu wa jk hvi hajaona wanvyampaka mafuta na mgongo wa chupa!!!!!!!!!:whoo:
   
 17. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,385
  Trophy Points: 280
  Unazi mwingine bana shida tupu!
   
 18. M

  Mutu JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  njaa mbaya
   
 19. N

  Njaare JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Mh! Kitendo cha kushi nje ya nchi na kuona wenzetu walivyo makini kwenye kazi zao bado ukaendelea kuwa CCM .......................!!!:angry::frown:
   
 20. jyfranca

  jyfranca JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Urusi nao njaa zimewazidi, upuuzi huu huwezi kuukuta kwa watanzania waliopo, Uingereza au Amerika
   
Loading...