Ninaomba vyama vya siasa viwe makini kupendekeza Mgombea Mwenza kwenye Uchaguzi Mkuu

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,789
2,383
Katika mchakato wa kupata Rais wa JMT, katiba inaelekeza kuwa ni lazima kuwe na mgombea mwenza ambaye Rais akishinda uchaguzi then mgombea mwenza huyo anakuwa Makamu wa Rais.

Nikiri kuwa sikuwahi kuchukua cheo cha Makamu wa Rais kwa uzito mkubwa. Mara nyingi niliona kuwa makamu wa Rais ni takwa la kikatiba tu kwa kuwa mara nyingi niliona kazi nyingi zikifanywa na Rais na Waziri Mkuu akisaidiwa na Mawaziri. Nilikuwa nikimwona Makamu wa Rais kama mtu wa kutembea na mikasi tu kwenye koti kukata utepe wa kuzindua hiki na kile.

Kifo cha Hayati JPM imenionesha kwa vitendo umuhimi wa kuwa na makamu wa Rais anayeweza kufanya kazi za Rais. Kumbe mgombea mwenza sio cheo cha kimasihara.

Nimejikuta nawaza mgombea mwenza wa Tundu Lissu, ndg. Salim Mwalimu. Nikawaza kama Tundu Lissu angeshinda urais na likatokea kwamba ilivyokuwa kwa JPM? Pamoja na ukweli kuwa namuheshimu sana Ndg. Salim Mwalimu lakini sidhani kama ana haiba ya kuwa Rais wetu.

Kimsingi hatoshi kuwa Rais wa nchi hii ukimlinganisha na Rais wake ambaye angekuwa Tundu Lissu. Sasa ni afadhali sana hata huyo Salim Mwalimu. Nimewaza wagombea wenza wengine kama yule wa mzee wa ubwabwa.

Tafadhali vyama viwe serious wanapotafuta mgombea mwenza.
 
Acha dharau basi! Haiba unayoitaka wewe ni ipi? Ni lazima mtu awe babu, awe na kitambi, au! Mbona Rais aliyepita alikuwa ana mapungufu mengi ya kiuongozi, lakini tumemvumilia kwa miaka yote hii!!

Na wewe umekua na akili za kindezi kama zile za yule Nabii Samweli wa kwenye Biblia? Aliye ambiwa akamtie mafuta Daudi awe Mfalme, badala ya Sauli, lakini akaishia kiwatamani watoto wakubwa wa Yesse akidhani ndiyo walifaa zaidi! Kumbe ikawa ni tofauti kabisa na mpango wa Mungu
 
Haiba ni nini
Ni muonekano?
Kama ndiyo unahusika vp na urais
 
Asee kwanza yule Jamaa mie nilikuwa kabisa simjui nimemfahamu kupitia majukwaa ya ugombea mwenza hupo vizuri sana kichwani.

Yani ukimtoa Lissu na Mbowe pale CHADEMA anayefatia Kwa hoja ni Salum Mwalimu.

Tatizo la miafrika tunaangalia maumbile ya mtu, hatumwangalii mtu upstair kama wenzetu huko duniani.

By the way,mtoa mada fahamu kuwa viongozi wengi walio acha historian Duniani haijalishi ni historian nzuri au mbaya wengi wao vimili vyao ndio hivyo vya akina Nyerere .
 
Awamu hii mtateseka sana. Sisi tulioteseka muhula wa kwanza, huu muhula wa pili tunakula bata tu.

Ingawaje CCM ni ileile ila kipindi hiki cha mwisho lazima mtakuwa na adabu maana meza imepinduka kibabe. Wale akina James washaanza kutubu, maombi yanaendelea.
 
Yaani hata mimi huwa najiuliza mpaka leo; yaani eti Salum Mwalimu "angelikuwa" Rais wa Tanzania!!!? Chadema acheni dharau. Mwaka wa 2025 wekeni mtu bwana!
 
Back
Top Bottom