Ninaomba niwe Mtetezi wa waTanganyika, na sisi tunataka nchi yetu iliyo zikwa na wakoloni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ninaomba niwe Mtetezi wa waTanganyika, na sisi tunataka nchi yetu iliyo zikwa na wakoloni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasimba G, Apr 12, 2012.

 1. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Mara zote kuna malalamiko juu ya muundo wa muungano toka upande mmoja, yaani Zanzibar, lakini kwa waTanganyika, watu wamekaa kimya huku wakinung’unika either kimoyomoyo au wakinung’unika lakini bila upande wa pili wa muungano kujua, yaani Zanzibar, kwa waTanganyika, wanaona sijui ni aibu kuiongelea kero hiyo au sijui wengi wetu ni wanafiki! Muungano kwa kizazi hiki wengi wetu I mean waTanganyika wanaudoubt ila wanaongelea Kwenye blangeti!

  Naomba nivae ujasiri na kusema na sisi waTanganyika tunataka uhuru wetu, kwanza, Taifa letu liliuwawa tofauti na wenzetu ambao Zanzibar yao ipo, Tunaomba turudishiwe taifa letu Tanganyika halafu kama muungano una faida kwetu tufanye makubaliano upya, Naililia Tanganyika yetu.

  Kwa waZanzibari, wanaona kamawamemezwa, lakini Zanzibar ipo, je na sisi waTanganyika tusemeje? tuseme hatujamezwa ila tuliuwawa, hebu naomba niwe advocate wa ufufuaji wa Tanganyka. Naomba mniunge mkono katika hili.

  Nawasilisha.
   
Loading...