Ninaomba kama kuna mtu anaweza kunipa uchambuzi wa hii ndoto anisaidie

Dim Ray

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
318
247
Habari zenu wana jamvi natumai tuwazima wa afya. Niende moja kwa moja kwenye mada,usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto ambayo imeniachia kiulizo ndoto yenyewe ni hii.

" Tulikuwa tunaelekea katika kijiji fulani ambacho kwa kufananisha balabala nilikuwa ninajua ni sehemu ambayo mzee(baba) anamiliki shamba , tulikuwa wengi lakini mimi nilipanda baiskeli . Watu tulokuwa nao kwenye safari waliniambia tunaenda kwenye mechi ya mpira, kiukweli ni kwamba nilionekana kuwafuata tu bila ya kuwa na jambo lolote la kufanya.

Cha ajabu ni kwamba haikuwa ivyo bali ilikuwa watu wako kwenye nyumba ambayo ilikuwa inaonekana inaendelea kujengwa ingawa iliwekewa bati na kutiwa mchanga kwa nje, nilimuona mzee(baba) yangu ambaye ingawa nilijaribu kumuambia tuondoke alinitizama usoni na kucheka tu, baadaye nikamuona ambaye nadhani alkuwa incharge wa mahali hapo akidai fedha kwa watazamaji.

Bila hiana niliondoka nikiwa na baiskeli yangu ,punde si punde nilifikia kwenye kanisa fulani (dhehebu kapuni) ghafla angani ukatokea mwanga kama mawingu ukionekana ukijichora na punde alama ya tarumbeta ikatokea ,kwa haraka nilitaka nichukue simu nipige picha lakini nilichelewa lakini kwa nyuma nilimuona mtu aliyefanikiwa kupiga hiyo picha, ghafla rafiki yangu wa A-level akanifuata nakuniambia mbona mbona si muda ilitokea alama ya ndege angani akasema ndo siku zimeisha.

Niliporudi nyumbani nilimkuta mama na mdogo wangu wa kike lakini mama alikuwa ameumia mguu upande wa chini wa sole na ankle mguu ulifungwa bandage na hapo ndo ikawa mwisho" sasa kiukweli ndoto sijaielewa kwakuwa ina vitu vingi sana ,ninaomba kama kuna mtu anaweza kunipa uchambuzi anisaidie .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom