Ninani atazirudisha pesa za wahindi na matajiri wa kiswahili wanaoichangia CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ninani atazirudisha pesa za wahindi na matajiri wa kiswahili wanaoichangia CCM?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngonini, Oct 12, 2010.

 1. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Juzi niliingia duka la mhindi mmoja nikiwa natafuta kitu fulani. Nilishangaa kuona nguo za kijani nyigi zikiwa kwenye shelf, nilipouliza je anauza, aliniambia haziuziki, ila tunatoa bure kama nyongeza kwa mtu anayenunua kitu hapa. Nilijaribu kudadisi namna wavyozipata ikaonekana CCM huwalazimisha kuzinunua hizi nguo kama mchango kwa chama. Kinachotokea ni kwamba hazinunuliki hivyo huamua kuzigawa bure kwa anayetaka kama bakhishishi. Nilipata uhakika kwamba huyu muhindi alikuwa amelazimishwa kununua nguo hizo na si kwa mapenzi yake kwa chama.
  Kitu kimoja ambacho kiko dhahiri nikwamba mtu akishakusaidia kwa fedha, umekuwa mtumwa kwake wala hutaweza kuyakataa matakwa yake. Wahindi ni watu wenye akili nyingi inapokuja kwenye swala la pesa,HATATOA HELA YAKE BURE BILA KURUDI!

  Kuna jamaa yangu mmoja alinipa udaku wa uchaguzi wa 2005, aliniambia tajiri wa mabasi fulani yanayoenda dodoma, alichangia chama kwa mkataba kwamba angerudisha fedha yake kwa kuua usafiri wa train ya Dar mpaka dodoma ili mabasi yake yatumike. Nilijaribu kukumbuka na kweli kukawa na ukweli fulani ndani ya udaku huu. Nikweli kwa kipindi kirefu kulikuwa hamna usafiri wa train toka dar-dom. Inasemekana ulirejea mara baada ya jamaa kurudisha fedha yake na faida.

  Kwangu mimi hii ni hujuma kwa wantanzania masikini, sijuwi kunahujuma ngapi za namna hii zilifanyika baada ya 2005 na ni ngapi zimepangwa kufanyika baada ya 2010.

  NIAMINIVYO MIMI: KIONGOZI ANAYESHIRIKIANA NA MATAJIRI KUTAWALA HAWEZI KUPELEKA NCHI MASIKINI KAMA TANZANIA KWENYE MAISHA BORA! NI MAISHA BORA KWA KILA TAJIRI NA BORA MAISHA KWA KILA MASIKINI.
   
 2. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kuna mtu humu JF anajiita RAJ PATEL. Ameshatamba wazi wazi kuwa ccm wakishinda uchaguzi wataendelea kushika uchumi wetu. What brash arrogance!
   
 3. M

  Myamba Senior Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mwisho wa yote ni 31/10/2010. Hakuna kunyanyasika tena katika tanganyika yetu.
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kwa hili mnakisaidia CHAMA chenu kwa constructive ideas za ushindi..hongereni sana kwa kuingia ikulu
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Naona Mkuu ngonini si mtanzania. Kama angekuwa mtanzania angejua ni kwanini watu leo wana remote control. Watu wanaweza kununua remote control ili waweze kucgaua channels wakiwa mbali, si lazima waende kwenye TV na kuanza kubonyeza wenyewe, pesa ina maliza kila kitu.

  CCM ni kitega uchumi kizuri sana, kwa kuwa hapo zamani ilikuwa automatic kuwa ukipata nafasi ya kuombea ubunge kupitia CCM tayari wewe ni mbunge, kwa hiyo kama uki-invest vya kutosha kwenye kutaka kupata nafasi ya kugombea ubunge maana yake ni kuwa jiandae kurudisha pesa zako na kuvuna zaidi. Na ukichangia zaidi ulaji ndio unakuwa mkubwa zaidi, unaweza kukumbuka kuwa kuna baadhi ya waheshimiwa waliotoa hela nyingi 2005 walichaguliwa kuwa mawaziri.

  Wanaoichangia CCM si wajinga, they know another EPA another Kagoda will come, kwa hiyo mtu akiinvest milioni 500 ana uhakika kuwa zitarudi na atapata faida zaidi, sasa mkuu anauliza hizo pesa zitaurudi vipi, sijui maana yake ni nini hakuna asiyejua kuwa CCM haina biashara ya kurudisha mabilioni ya pesa.
   
 6. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe mwananchi ndiye utakaye lipa hilo deni.
   
Loading...