SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,803
- 1,863
Sasa huyu anataka treasury registrar aajiri inamaana serikali kwenye Mashirika ya reli, umeme, maji, Mawasiliano, matibabu, viwanda muajiri awe mmoja hivi huyo muajiri anakua na utaalamu gani wa kujua sifa na vigezo vya watu wote hao wakati fani yake ni uchumi?
Gawa majukumu kwa kila mtu ili kuwe na ufanisi waziri sio mjumbe wa nyumba 10/10
Lakini unaweza kushangaa watu wanaona anaongea points kumbe pumba tu, nimejua yaani kama utakua unapinga tu masuala Bungeni ndio nyumbu wanakuona wa maana bila kujali kipi unapinga na uhalali wake
Kaka REDEEMER,
Afadhali umeiona. Unajua Bashe anawazidi wengi bungeni na humu JF kwa kigezokwamba ameshiriki mfumo wa biashara kabla hajaenda bungeni. Kumbuka amekuwa Director wa Media moja kwa muda mrefu na akiongea inabidi uwe umeenda shule kwelikweli kupangua hoja yake.
Ona hata wanaochangia wanaishia tu kusifia bila kwenda ndani.
Wewe umeona hiyo point na mimi naongezea kwambaBashe haja-study vitu vingine katika business system. Hukohuko kwenye private sekta bado kuna ugomvi mkubwa kwamba nani awe mwajiri hasa kama institution ina discipline nyingi.
Tatizo la appointment liko kote na linatokana na utata kwamba ni nani anapaswa kutoa appointments. Kampuni nyingi zilipoingia hapo nchini zilikuwa zinaweka director wa kila department anakuwa executive director na anakuwa na decision kwenye board. Baadaye Chief Executive (CEO) wakaona hiyo inawapunguzia nguvu maana Managing Director (MD) anajidhani ni mkuu wa kampuni lakini akiingia kwenye board na executive directors wenzake anaweza kuzidiwa hoja na finance director au operations director.
Wapo wanaoamini kwamba kwa sababu fedha ndiyo inayoendesha kampuni au taasisi basi mkuu wa fedha ndiye anayepaswa kuajiri. Hii ndiyo concept ya Bashe. Wapo wanaoamini kwamba Operations Director ndiye anatakiwa kuajiri watu wake na hasa kama kampuni kama TTCL ina section ya professional duties.
Mzozo huu umekuw ani mkubwa kiasi kwamba ma-director wamekuwa wakitunishiana misuli kwenye board na ilipofikia hatua hii wakaona mbinu ni kuvuja kampuni kidogokidogo kuifanya iwe na “outsource”.
Yaani department inavunjwa na kuwa kampuni binafsi na huko inakuw ana director wake. Department ya Sales nayo inageuzwa kwa kampuni binafsi inakuw ana director wake. Department ya Marketing inafanyw ahivyohivyo na inakuwa kampuni na director wake.
Hivyo, kwa nje unaona kwamba ni kampuni moja lakini kumbe ukweli ni kwamba ndani yake kuna “outsurce” nyingi tu. Hii ni “outsource” usichanganye na “subsidiary”. Maana “subsidiary” ni kampuni ndogo bado inamilikiwa na kampuni mama.
“Outsource” ni kampuni nyingine kabisa. Natoa mfano mdogo unielewe. Zamani kampuni zote zilikuwa zina section ya ulinzi au usafi. Siku hizi ulinzi siyo section au department bali ni kampuni kabisa inajitegemea na ina director wake. Ndiyo hizi security companies.
Usafi nao ni kampuni inajitegemea ndiyo hawa akina “Global Trotters” na ndiyo inayoajiri hawa mabinti wanaopiga kelele ovyo kwenye lift za majengo mengi marefu. Hawa ni wafanya usafi wameajiriwa na kampuni ya usafi.
Hivi ndivyo ilivyo sasa hivi.
Inaelekea TTCL bado imelala na mfumo ule wa “monolith company” yaani Managig Director anasimami kila kitu na board inamsimamia na kuna kamouni moja tu.
Dunia sasa hivi haiku hivyo. Ule ugomvi wa madaraka niliousema umeifikisha dunia hapa. Na isingekuwa ku-split katika “outsource” ni wazi kungekuw ana ugomvi ni nani mkubwa na ni nani aajiri.
Mkurugenzi wa fedha ana idara yake na watu wake wa fedha ataambiwa ajiri watu wa idara yako tuachie mambo mengine sisi. Hivyo huwezi kusema per se kwamba mhusika na fedha kama “Treasury Registrar” ndiye awe mwajiri kwa sababu ni msimami kama anavyosema Bashe.
“Treasury Registrar” anaweza kuona “financial position” ya kampuni . Lakini “financial position” inatokana na vitu vingi. Unahitaji professional experts wazuri na yeye hawajui anawajua wallet waliomaliza mambo ya accounts. Hajui customer care wazuri au hajui kabisa hata customer care ni nini na hawa ndiyo wanaokutana na wateja.
In fact mimi kama mteja wa TTCL au kampuni yoyote mtu wa muhimu kwangu ni Customer Care maana ndiye ninayemalizana naye kwa mambo mengi.
Hivyo, kampuni haiendeshwi kwa kuzingatia mtaalamu wa pesa vinginevyo mtu ambaye hakusoma accounts asingeweza kuanzisha kampuni au kuendesha kampuni.
Ninakubaliana na Bashe kwamba ni tatizo kumuweka Waziri awe appointing officer lakini ninakataa solutionyake kwamba appointing officer awe “Treasury Registrar”.
Kuna option ameiweka lakii hakuisema sana. Kwamba hizi position ziwe competitive yaani zitangazwe na zigombaniwe. Naposema hivyo anamaanisha position za board members. Ukitaka kuwa board member basi nafasi itangazwe na tugomee mimi na wewe.
Unaweza kudhani ni sahihi na rahisi lakini tuuchambue mfumo huu. Hivi kweli hapo Tanzania watu wanajua na kufuatilia mambo yanayofanywa na bodi zetu? Bashe kasema vizuri kwamba kuwe na quarterly report yaani ya miezi mitatu na si ya miezi sita kama inavyopendekezwa kwa TTCL.
Lakini hata kama kungekuwa na monthy report turejee kwenye swali la mwanzoni, je kazi za bodi nyingi ni nini? Swali hili jibu lake ni moja kote seikalini na kwenye private sekta kwamba kazi za board mara nyingi ni kama hakuna. Inawezekana kabisa kuendesha kampuni yoyote ya sekta binafsi au sekta umma bila hata kuwepo na bodi ya wakurugenzi.
Bodi ni kikao kinachokaa sanasana wiki nzima wakati kampuni huendesha shughuli zake kila siku. Wengi huwa hawana uelewa wa shughuli za kampuni wakati biashara inahitaji ubuinifu wa kila dakika.
Hivyo mwenye kuelewa mambo mengi ya kampuni ni executive director yaani Managing Director na executive director wenzake. Hawa wanaokuja kucnywa chai kwenye kikao cha bodi ni vigumu kupinga hoja za Executive Director labda tu awe si mwadilifu na fisadi. Lakini kama ni muadilifu board members watakuwa wanapiga usingizi kama bungeni hawana la kumpinga maana yeye ndiye anayeendesha na anajua challenge zinazozaliwa kila leo katika sekat tena challenge zingine hazikuonekana mapema na bodi.
Hivyo mfumo huu ndiyo ubovu wake, bado tunaamini sana uwepo wa bodi. Ni mfumo huuhuu umefanya bodi zifukuzwe na zitaendelea kufukuzwa au kutumbuliwa kila leo kwa sababu biashara ya kampuni ukweli ni kwmaba haimo mikononi mwa bodi bali imo mikononi mwa executive directors yaani Managing Director na executive directors wake.
Tena hata nawa wamechoka siku hizi na nimesema kwamba wame-split kampuni na kugawa kazi katika vikampuni vidogovidogo vinavyoitwa “outsource”. Ndiyo hawa akina EROLINK, HUAWEI nk.
TTCL au hata TANESCO ikubali na iendane na hali ya sasa. HUwezi kuwa na kampuni kubwa imesamba anchi nzima ukaweza kui-manage hata kama inasimamiwa na Waziri anachokipinga Bashe au hata ikisimamiwa na “tresures registrar” anavyopendekeza Bashe.
TTCL na TANESCO zinatakiwa kuwa split na kampuni ndogondogo zifanye kazi kama makampni makubwa yote yanavyofanya kwa miaka zaidi ya kumi sasa.
Kingine alichojisahau Mheshimiwa Bashe ni pale anaposema nafasi za bodi au hata ukurugenzi ziache kuwa appointment ziwe zinatangazwa. Nimeshasema ni wazo zuri lakini anakosea kusema eti “private sector” wanafanya hivyo.
Ndugu zangu JF, hebu niambien ni kampuni gani ya binafsi ilishawahi kutangaza nafasi za “u-director” au nafasi za “board members”? Mimi binafsi sijawahi kusikia na kama ni uzembe wangu nikumbusheni.
Ninachojua watanzania wengi hawajawahi kuwa na cheo hiki cha “director” hukohujo kwenye “private sector”. Chagua kampuni kubwa za wawekezaji nchini na uniambie ni kampuni ngapi zina “Managing Director” mtanzania. Hakuna.
Lakini kampuni hizohizo utakuta zimeweka “Board Chairman” mtanzania, tena mwanasiasa, kitu anachokikataa Bashe. Spika mmoja wa Bunge aliwahi kuwa “Board Chairman” kampuni moja kubwa hapo nchini hadi aliposakamwa kuhusu "u-board member wake" akawajibu wanaomsakama kwamba “wana wivu wa kike”.
Huyu ni mwanasiasa na nafasi yake huko haikutangazwa kwala ugombewa bali aliitwa na kupewa kwa vigezo viijuavyo hiyo kampuni na kampuni kubwa sana hadi leo ipo. Na iliendelea na mtindo huohuo wa kupata wanasiasa kuwa "ma-Board Chairman".
Lakini tujiulize. kkwa nini hawa kampuni binafsi kwenye Board wanaweka watanzania lakini executive director hawathubutu kuweka mtanzania?
Mtokeo yake hakuna mtanzania unayemsikia kuwa ni “Managing Director” kwenye hizi kampuni binafsi.
Sababu nimeshaisema nayo ni kwmaba bodi nyingi ni kama rubber stamp tu ni kama hazina kazi kwani kazi kubwa wanafanya executive directors yaani Managing Director, Finace Director au Operations Director.
Na siku hizi kazi zinafanywa na "oustsource companies" wanawekeana KPI agreement maisha yanakwenda.
Hivyo ukiwadanganya watu kwamba kwenye bodi za kampuni biafsi kuna watanzania wenzenu na sisi tunapofuka kama wajinga tukijidhani eti watanzania nao tuna maamuzi katika kampuni binafsi kumbe ni change la macho.
Hivyo, hata huko private sekta anakokusifia Bashe bado kuna uozo uleule kwamba appointments bado ni za kuteuliwa kama serikalini wala hakuna interview au tangazo lolote.
Ongezeeni mnayoyajua tukijua tunajadili hatima ya shirika letu TTCL na mengine
-------------------
Kitendo cha kuifanya TTCL-PESA kuwa kampuni tanzu ni kifo kwa ttcl,Celtel ilianza hivyo na mwishoni wakajitenga!!!! na mwishoni wakalipwa bila kuwekeza chochote!! Bashe keep it up!! TTCL-PESA imilikiwe na TTCL 100%
Huyu jamaa akili yake iko mbali sana kulinganisha na yule wa "mipasho"
keep it up Bashe
TTCL isijekurudi kuwa Shirika la Umma tena. Kila mtu anafanya anachotaka na hakuna kuwajibishwa. Mara nyingine tuangalie mambo gani yatasaidia tufike tunapotaka kwenda