Ninamiliki kituo Cha mafuta, mshindani wangu anauza Sana kuliko mimi. Nini nikifanye kuongeza mauzo na wateja

Wakuu Kama nilivoelezea hapo hapo juu namiliki kituo Cha mafuta. Nina changamoto yakushuka mauzo kulinganisha nahapo awali mauzo yamepungua baada yakuongezeka vituo viwili vingne vya mafuta. Nini nifanye kuongeza mauzo au kuvuta wateja Zaid ukizingatia washindani wangu wana nguvu zaid yangu maana hawakodi magari Bali wana magari yao yakuwabebea mafuta pindi waendapo nunua mafuta katika madepot ya jumla. Sasa wakuu nin nifanye kuongeza mauzo ktk Hali hii
Shell yako ikoje?iko wapi?ina nini zaidi ya kuuza mafuta.Unauza lita ngapi kwa siku?target yako ni lita ngapi kwa siku?
 
Yawezekana jamaa wamekupiga pin kwenye suala la location tu.
Ukiwa na chombo cha usafiri kuna upande ni rahisi sana kuweka mafuta kuliko upande mwingine.
Note: kama uko mjini, hakikisha unakuwa na change nyingi, madereva wa bajaji, bodaboda na daladala wakija wapate change bure.
Utanishukuru.
 
Chief, msikilize vizuri Karucee yupo sahihi sana.
Kuna issue pia ya dereva anaeleta mafuta kituoni kucheza mingo na meneja anaesimamia kituo.

Wewe kila siku unachezea shoti tu.

Usikae home miguu juu ukijitapa una kituo. Nenda kituoni mida ya wanga, kaa siti ya nyuma angalia mchezo.

Utakuja kuwakuta pump attendant wanafanya 'basdei' hapo hapo wamelewa na kuna chupa cha pombe changing room.
 
Hakika hii field waijua vizuri, mbongo mpe mgongo unapigwaa😂
 
Kuna issue pia ya dereva anaeleta mafuta kituoni kucheza mingo na meneja anaesimamia kituo.

Wewe kila siku unachezea shoti tu.

Usikae home miguu juu ukijitapa una kituo. Nenda kituoni mida ya wanga, kaa siti ya nyuma angalia mchezo.

Utakuja kuwakuta pump attendant wanafanya 'basdei' hapo hapo wamelewa na kuna chupa cha pombe changing room.
Unayosema ni sahihi kabisa, hayo mambo yapo sana. Kimsingi ni mambo madogo madogo, lakini yana impact kubwa katika "afya ya biashara" hiyo.
 
Pole sana...

Kama mwenzako anauza 2450 wewe uza 2448 it makes a difference...

Kuna na wafanyakazi shapu na wenye kauli nzuri Kwa wateja...
 
Wakuu Kama nilivoelezea hapo hapo juu namiliki kituo Cha mafuta. Nina changamoto yakushuka mauzo kulinganisha nahapo awali mauzo yamepungua baada yakuongezeka vituo viwili vingne vya mafuta. Nini nifanye kuongeza mauzo au kuvuta wateja Zaid ukizingatia washindani wangu wana nguvu zaid yangu maana hawakodi magari Bali wana magari yao yakuwabebea mafuta pindi waendapo nunua mafuta katika madepot ya jumla. Sasa wakuu nin nifanye kuongeza mauzo ktk Hali hii

Piga Kazi na sala mkuu

Wakati mwingine wateja hawafati bei wanafata huduma. Mungu akupe macho na maskio ya kuwasikiliza wateja

Utakua juu tuu😎😎
 
Anazingua.
Huenda hujamuelewa mkuu wala hakukubishia alieleza anachokifahamu yeye. Ulichosema ww pia ni sahihi ndiyo practice.

Nitoe mfano labda. Last week kuna sehemu pump iligoma kutoa receipt alichofanya pump attendant alicheki na mwenzie akamuuliza kama ameuza mafuta ya bei hiyo siku hiyo akacheck kwenye recepts zake akaipata moja nikapewa hiyo kureplace hiyo ambayo pump imegoma kutoa same amount same date. Hayo yanawezekana sbb receipts zina mapungufu mengi likiwemo la kutokuwa na na reg no ya gari husika. So receipt kuuzwa ni very possible kwa mazingira yaliyopo kwa sasa.
 
Chief, msikilize vizuri Karucee yupo sahihi sana.
Mkuu akija mteja anataka mafuta 150000 Kisha ww umpatie risiti ya 200000 haiwezekani unless uwe narisiti ya 200000 ambayo mtu alinunua mafuta akaiacha..maana unaporudisha tu mkono kwenye pampu risiti hutoka hapo hapo inamaana ukikatia mafuta anayochukua ya 150000 itaishia hapo hapo narisiti itatoka yahiyo hiyo hela..hakuna namna utafanya utoe rosti ya Zaid bila kuuza mafuta mafuta yakiwango hicho hicho Cha risti anayotaka
 
Kuna issue pia ya dereva anaeleta mafuta kituoni kucheza mingo na meneja anaesimamia kituo.

Wewe kila siku unachezea shoti tu.

Usikae home miguu juu ukijitapa una kituo. Nenda kituoni mida ya wanga, kaa siti ya nyuma angalia mchezo.

Utakuja kuwakuta pump attendant wanafanya 'basdei' hapo hapo wamelewa na kuna chupa cha pombe changing room.
Mkuu nipo anytime kituoni nahesabu mwenyewe ndio manger
 
Wakuu Kama nilivoelezea hapo hapo juu namiliki kituo Cha mafuta. Nina changamoto yakushuka mauzo kulinganisha nahapo awali mauzo yamepungua baada yakuongezeka vituo viwili vingne vya mafuta.

Nini nifanye kuongeza mauzo au kuvuta wateja Zaid ukizingatia washindani wangu wana nguvu zaid yangu maana hawakodi magari Bali wana magari yao yakuwabebea mafuta pindi waendapo nunua mafuta katika madepot ya jumla. Sasa wakuu nin nifanye kuongeza mauzo ktk Hali hii

Kuna kitu kinaitwa “Ongezeko la thamani “ ,hichi ni kitu pekee katika biashara yeyote inayoanza ni lazima kuwa nayo_Ongezeko la thamani huonesha ni kitu gani cha kipekee katika biashara yako kinakutofautisha na biashara zingine zinazotoa huduma au kuuza bidhaa kama yako.Mfano kama wewe wa kituo cha mafuta unaweza kuweka offer kwa wateja wako kwamba kwa mtu atakae nunua mafuta kwako na kutunza risiti zake kutoka kwako pale anapofikisha risiti zenye thamani ya lita 200 za mafuta utampa lita mbili bure pale atakapo kuja na risiti zote zenye thamani hiyo kutoka kwako.Hii inaweza kuchukuliwa poa lakini hata mimi binafsi ningekuja kwako kama ubora wa mafuta yako ni sawa na vituo vingine vilivyopo jirani,huu ni mfano tu lakini unaweza kucreate vingine vingi na ukavutia wateja zaidi.
 
Hapo kuna vitu vingi,

Sheli nyingi zinauza mafuta machafu,kuna sheli nilikua naweka mafuta then taa ya check engine inawaka,ikabidi niachane na hicho kituo na ninawaambia na watu wengine wasiende hapo,just imagine ni kituo chako huoni umepoteza wateja wengi?

Ushauli wangu ni uweke box la maoni, na wewe pia ukae hapo kama week moja hivi ufuatilie ubora wa huduma na bidhaa zako.
 
Kuna jamaa ana kituo kimoja tu pale luguruni anauza sana weka competitive price punguza hata 5sh. Tu unaona mafanikio
 
Back
Top Bottom