Ninakosea wapi? Au biashara ni kipaji?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
Hbarini wafanyabiashara.

Binafsi ni kijana nimeingia 31, ni muajiriwa seikalini shirika flani, Nilikuwa navutiwa sana na ujasriamali hivyo na mimi nikaona nisijivunge.

Nikaona nifungue steshonari nimweke dada wa kazi awe ananisaidia, sikutaka kukopa hivyo nikafikiria nifungue biashara ambayo mshara wangu unaweza kuwa mtaji, Basi nikakusanya mshahara, viposho na balance ya benki nikafanikiwa kununua photocopy machine, printe ya rangi, lamination, computer, madaftari, peni,n.k niligharamika milioni 3 na kitu hivi

Gharama za kila mwezi huwa ni chumba - 100,000, Mshahara wa binti- 100,000, chakula+choo+taka+usafiri wa binti - 90,000, umeme+ulinzi - 20,000, hivyo matumizi jumla huwa ni kama 310,000. Mauzo yote kwa mwezi huwa yanacheza kwenye laki 4 hadi laki 4 na nusu na kuna muda anakuwa pungufu kwa hio kama unavyoona hapo faida ipo ila ya kawaida kuifanya tu biashara isiwe na hasara

hio faida kiukweli inaniumiza maana hata nikizidisha mara 20 bado haifikii msharawangu baada ya makato, yani hata kazini huko watu baki wanaoniulizaga steshinari inaendeleaje huwa inabidi niwadanganye faida ili kuepuka aibu

sasa sijui nijiongeze vp wadau
 
Hbarini wafanyabiashara.

chumba nlipata cha laki, binti nikawa nampa laki mshahara na alowance ya elf 3 kila siku kwajili ya usafiri, msosi, choo, maji, n.k,

kusema kweli naona biashara hainilipi, kwa mwezi nikitoa kila gharama nabaki na elf 80 au laki...

sasa sijui nijiongeze vp wadau

Hiyo 80/100K unaipata baada ya kufanya haya yote?hiyo biashara ina muda gani?

Nijuavyo biashara kama bado ni changa hatutegemei profit iwe kubwa mapema so kama ni ya muda mfupi una nafasi ya kufanya vizuri bado,pia inawezekana hujajitosheleza bado kivifaa that's why unaona faida ni ndogo so cha kufanya weka nguvu zaidi pia ongeza M-pesa Tigopesa etc unaweza kwenda vizuri zaidi.
 
Hii biashara ya kitambo mkuu ni miaka mitatu sasa, huwa najipa matumaini ipo siku itakuwa ila wapi,

Gharama nlizotumia kuanziha biashara,

photocopy 1,800,000
printer ya rangi yenye scanner - 450,000
computer 400,000
lamination 100,000
kalamu, bahasha, madaftari, n.k - milioni 1

Gharama za kila mwezi

chumba - 100,000
Mshahara - 100,000
chakula, choo, taka, usafiri - 90,000
Umeme - 20,000

Jumla ya mapato yanacheza kwenye laki 4 na kitu, mara chache inazidi
 
Hii biashara ya kitambo mkuu ni miaka mitatu sasa, huwa najipa matumaini ipo siku itakuwa ila wapi,

chumba - 100,000
Mshahara - 100,000
chakula, choo, taka, usafiri - 90,000
Umeme - 20,000

Jumla inacheza kwenye laki 3

mapato kwa mwezi unakuta ni kama laki 4 ama pungufu, ikizidi ni mara chache sana
Kwa biashara inayoweza kulipa hivyo vitu kwa muda wote huo naamini kuna ziada zaidi inapatikana hapo ni vile wewe hujajua bado,haiwezekani mwaka wa kwanza mpaka wa tatu faida zifanane hiyo hali ipo planned na anayefanya hivyo ni huyo uliyemwamini.

Umesema anakaa mtu...right?em kabla hujawaza kuifunga vizia likizo moja shinda hapo asubuhi mpaka jioni utajua kama pana hasara au lah.
 
kwa mwezi nikitoa kila gharama nabaki na elf 80 au laki...
Kama ukitoa kila kitu kuanzia mshahara/matumizi yote unabakiwa na faida ya 80,000 to 100,000

sikushauri uache hiyo biashara hata kidogo,wewe kilio chako ni faida ndogo ila si kwamba hupati kbsa

wenzako wanaliaga hawapati kabisa,80k usiichukulie poa kwa biashara, hebu jiulize biashara yako hiyo

ukiendaga fata mzigo wa 80k unachukua vitu kiasi gani?! assume huitumiii hiyo hela iache usiiguse kwa

miezi 10 tu Utakuta kibubu kina 800k hivi ukijikaza ndani ya 10month ukichukua ile 800k ukairudisha yote

kwenye hiyo biashara yako unahisi utakua na stationary ya ukubwa gani? Shida yenu watu mliozoea ajira

mnapenda mahela mengi mengi yanayokuja kwa mara moja kama mishahara yenu ilivyo, Biashara/ujasiriamali haupo hivyo.

Huku tunakusanya sh 200 tu sh 100 tu sh 50 tu sh 500 then total tunakuja ipata baada ya miezi kadhaa SO mkuu nikwambie tu kitu, Biashara yako iko vizuri sana komaa hapohapo Punguza matumizi yasio na lazima

graph yako ya income kwa mwezi itaongezeka,Kingine akili yako iruhusu kufanya kazi zaidi unapoona biashara inakupa income ndogo usifikirie kuiacha "utaacha biashara ngapi"?

jifunze kuweka akiba na kujiona kama huna biashara ongeza biashara nyingine na nyingine kupitia hicho kidogo unachokipata kwa mwezi "biashara za mitaji ya laki zipo kibao" zifanye.

kuwa na biashara nyingi ndogo ndogo unapofika mwisho wa mwezi ukikusanya kote Utajikutaa mfukoni una not less ya 3 to 4m (depends na vibiashara vyako) Acha kupasuka kichwa na biashara kubwa kubwa.

Umeingia ktk ujasiriamali Cheza namba zote cheza miguu yote Kuwa kiraka kama mcheza mpira anaetumia left n right...

Mwisho : Usifunge wala usiache hiyo biashara bali itumie kama sehemu ya kupatia mitaji ya vibiashara vyako vingine... Go ahead Champion...
 
Kwa biashara inayoweza kulipa hivyo vitu kwa muda wote huo naamini kuna ziada zaidi inapatikana hapo ni vile wewe hujajua bado!

Umesema anakaa mtu...right?em kabla hujawaza kuifunga vizia likizo moja shinda hapo asubuhi mpaka jioni utajua kama pana hasara au lah.
Mkuu kuna muda niliwahi kudhani hivi na nilishajaribu kukaa dukani na ziara za kustukiza, kama ni kuibiwa itakuwa ni kwenye lamination ya vyeti huku maana mashine yake haiesabu kazi, anyway kwenye lamination wateja sio wengi sana, wateja wengi ni kwenye copy huku na printing, na hizi huwa zinahesabika kabisa hata ukiwa hushindi hapo
 
Kama ukitoa kila kitu kuanzia mshahara/matumizi yote unabakiwa na faida ya 80,000 to 100,000

sikushauri uache hiyo biashara hata kidogo,wewe kilio chako ni faida ndogo ila si kwamba hupati kbsa

wenzako wanaliaga hawapati kabisa,80k usiichukulie poa kwa biashara, hebu jiulize biashara yako hiyo

ukiendaga fata mzigo wa 80k unachukua vitu kiasi gani?! assume huitumiii hiyo hela iache usiiguse kwa

miezi 10 tu Utakuta kibubu kina 800k hivi ukijikaza ndani ya 10month ukichukua ile 800k ukairudisha yote

kwenye hiyo biashara yako unahisi utakua na stationary ya ukubwa gani? Shida yenu watu mliozoea ajira

mnapenda mahela mengi mengi yanayokuja kwa mara moja kama mishahara yenu ilivyo, Biashara/ujasiriamali haupo hivyo.

Huku tunakusanya sh 200 tu sh 100 tu sh 50 tu sh 500 then total tunakuja ipata baada ya miezi kadhaa SO mkuu nikwambie tu kitu, Biashara yako iko vizuri sana komaa hapohapo Punguza matumizi yasio na lazima

graph yako ya income kwa mwezi itaongezeka,Kingine akili yako iruhusu kufanya kazi zaidi unapoona biashara inakupa income ndogo usifikirie kuiacha "utaacha biashara ngapi"?

jifunze kuweka akiba na kujiona kama huna biashara ongeza biashara nyingine na nyingine kupitia hicho kidogo unachokipata kwa mwezi "biashara za mitaji ya laki zipo kibao" zifanye.

kuwa na biashara nyingi ndogo ndogo unapofika mwisho wa mwezi ukikusanya kote Utajikutaa mfukoni una not less ya 3 to 4m (depends na vibiashara vyako) Acha kupasuka kichwa na biashara kubwa kubwa.

Umeingia ktk ujasiriamali Cheza namba zote cheza miguu yote Kuwa kiraka kama mcheza mpira anaetumia left n right...

Mwisho : Usifunge wala usiache hiyo biashara bali itumie kama sehemu ya kupatia mitaji ya vibiashara vyako vingine... Go ahead Champion...
Watu Kama nyinyi ndo mnahitajika hongera sana

Na karibu jf maana nakuona kama mgeni kwa nondo ulizotapika
 
Kama unapata 80,000 kwa mwezi faida, niamini mimi huyo mfanyakaz wako anakuibia faida sio chini ya 100,000
Experience ya hio biashara ya stationary wengi wanao faidika nayo, ni wale waliojiajiri na kushinda nayo asubuh hadi jioni. Pia ni wale wanaoweka wake zao.

Inshort kwa miaka hio 3 huyo dada ndio unae mtajirisha, biashara ingekua mbaya angekukimbia. Stationary ni kama duka tu la rejareja anekuuzia ndio anajua namna ya kukupiga pesa.
 
Dah mkuu, ukilinganisha pesa nliyoweka na ninayoipata ni asilimia ndogo, yote kwa yote naombeni mbinu za kitaalam kuikuza, kuna kipindi mtu alikuja na ofa ya milioni 3 ila nilimtolea mbali apo kwa sasa naanza kutamani nngeikubali ile ofa
 
Mkuu hapa nimekwisha badili mabinti wa kazi kama watatu hyu wa sasa ni wanne, vigezo vyangu inabidi wawe mabinti wadogo, Moj aliondoka alipopata ajira wengine waliondoka kwajili ya mimba ila nashukuru hawakukimbiwa :):) ,
 
Dah mkuu, ukilinganisha pesa nliyoweka na ninayoipata ni asilimia ndogo, yote kwa yote naombeni mbinu za kitaalam kuikuza, kuna kipindi mtu alikuja na ofa ya milioni 3 ila nilimtolea mbali apo kwa sasa naanza kutamani nngeikubali ile ofa
Biashara zipo nying ndugu chakata ubongo huo...na hapo ndo kwenye kaz nzito...nna ka chemba kangu ka1 mtaj wake ni 1m ila kwa mwez kananipa 160k...na nnaweza nisiende kukazungukia kuangalia hata miez miwil..ila kanajiendesha kenyew tu

Ni lazima uumize akil kwelkwel kupata idea hiz za biashara...msome sana huyo jamaa controla nyuz zake utapata kitu

Mim miaka miwil au mitatu nyuma huyo jamaa alibadil life langu kwenye upande huo wa ujasiriamali...so komaa nae
 
Yani ubinifu ndio siri kiukweli, japo inabidi usiingie kichwa kichwa, kusoma wazo ama kuliongelea ni rahisi sana ila kwenye utekelezaji hata hatua ya kutia tu mtaji ni kimbembe
 
Tatizo Lako Pesa nyingi inatoka nje.

Binafsi huwa natumia principle Hii,
1.Mshahara wa mfanyakazi/wafanyakaz kwa mwezi,
haitakiwi kuzidi 10% ya mauzo yangu kwa sikU.

Mfano: Ili nimlipe mfanyakazi laki 100,000, natakiwa kua na uhakika wa mauzo yasiyopungua million 1 kwa sikU.

2. Fremu ya biashara inatakiwa iendane na faida ya biashara husika,
Biashara ili inilipe, Lazima faida inayoingia ndani ya sikU 7 za mwanzo iwe na uwezo wa kulipia Kodi ya pango kwa mwezi mzima.
Kama Kuna ishu za vibali, tra,manispaa n.k, hapo faida ya sikU 10 itapaswa kucover vyote hivyo.
 
Hbarini wafanyabiashara.

Binafsi ni kijana nimeingia 31, ni muajiriwa seikalini shirika flani, Nilikuwa navutiwa sana na ujasriamali hivyo na mimi nikaona nisijivunge.
Sijaelewa hapo unamaanisha ukitoa pamoja na gharama za kununulia hizo stationaries zote unazoziuza au? lakini pia uwe unaweka akiba itakayo kusaidia ku fanya replacement ya hivyo vifaa, fotocopier pamoja na printer.maana zikichoka huwa matengenezo ni ghali sana
 
Yani ubinifu ndio siri kiukweli, japo inabidi usiingie kichwa kichwa, kusoma wazo ama kuliongelea ni rahisi sana ila kwenye utekelezaji hata hatua ya kutia tu mtaji ni kimbembe
Confidence ya kutia mtaj huja ukiwa tayar umesha cheza sana na biashara na idea ushazipractice ukaona zinatoa..hapo lazima uwe na confidence..na hyo inajengwa na kuanza biashara tuu no bla bla..unaanza unajikwaa unainuka..unajifunza.zunguka mitaan masokon angalia watu wanafanya nin.soma mazingira fata sheria za biashara zote zinataka nin...kama research fanya..anza mtaj mdogo..huku unakua..

Ndivyo kila mtu anaanza hvyo na watu wanatoboa...mim sasa hiv nna magol meng tu ya kutosha...nna confidence ya kuanzisha kitu..tatzo langu ni management tu ndo nahangaika nayo...so kama nilivyokwambia msome huyo jamaa..hata sis tulikua kama wew mwanzo
 
Funga camera,
zitasaidia kupunguza wizi. Tafuta hata za laki 3 tu. hesabu itaongezeka kidogo mpaka 150-200/month

Then ndo uje uongeze mtaji
 
Tatizo Lako Pesa nyingi inatoka nje.

Binafsi huwa natumia principle Hii,
1.Mshahara wa mfanyakazi/wafanyakaz kwa mwezi,
haitakiwi kuzidi 10% ya mauzo yangu kwa sikU.

Mfano: Ili nimlipe mfanyakazi laki 100,000, natakiwa kua na uhakika wa mauzo yasiyopungua million 1 kwa sikU.

2. Fremu ya biashara inatakiwa iendane na faida ya biashara husika,
Biashara ili inilipe, Lazima faida inayoingia ndani ya sikU 7 za mwanzo iwe na uwezo wa kulipia Kodi ya pango kwa mwezi mzima.
Kama Kuna ishu za vibali, tra,manispaa n.k, hapo faida ya sikU 10 itapaswa kucover vyote hivyo.
Mzee hii model yako si mchezo...biashara zako lazima ni za mitaj mikubwa sana....mauzo milion kwa siku si mchezo
 
Back
Top Bottom