Predigo son. Kiwanja kipo wilaya kilindi, kina hekta 10 au ekari 25, madini ni ya dhahabu. Then n - handsome. Nipe adress ya kanada ili nitume cv mtu wangu.
Maelezo hayajitoshelezi hata kidogo, Mf madini ya aina gani?ukubwa wa kitalu?kiko wapi?. nahdani ungeweka hayo maelezo wenye nia wanaweza shawishika/QUOTE]
Makola tatizo lako ni zaidi ya kiwanja ndugu yangu. Kwanza nina wasi wasi na unavyoweza ku market! Mwekezaji anahitaji detail nyingi sana kabla hajaamua kuonana na wewe. Sasa unaposema nina kiwanja, hatujui ukubwa wake, madini gani, leseni ya daraja gani, kadirio la madini,leseni inakwisha lini n.k sijui unategemea nini. Kwa ushauri wangu, hapa Tanzania wapo watu wa madini na project management, hawa ni wazuri sana kabla hujaingia mikataba mikubwa au huja market bidhaa au mali yako. Watakusaidia maana ninaona hata akipatikana uwezekanao wa kutapeliwa ni asilimia 1000%
Hii ni sawa na ile ya mheshimiwa kitomari wa JF anatangaza nyumba za kupanga haweki hata picha,! wapo watu wako nje ya nchi mathalani wanataka kukodi nyumba kwa sababu mbali mbali, sasa kama hakuna picha na details utawapata wapi wateja. Jana kuna mtu kanipigia simu toka ireland eti niende nikaangalie apartment zinafanana vipi hiko kimara! kazi hii Kitomari angeshaimaliza kama angeweka picha na kuwa makini.
Please Watanzania, amkeni na mjue mbinu za kuuza na kujiuuza, ikiwa ni pamoja na buisness plan and management. Tusifanye kazi kwa kubabaisha, that time is over, now is competition from north to south, east to west!
Mheshimiwa Makola, hata ungeenda UDSM wapo watu wangekusaidia bure kuliko kukurupuka,'' nina kiwanja na leseni .....'' fanya mambo kisayansi my brother, unaweza uza eneo la bilion 30 kwa milion 3! simply because you don't ask!