Ninakerwa na watanzania wanaokiharibu kiswahili chetu kwa uzembe tu

ESPIRIT

JF-Expert Member
Jul 3, 2014
665
524
Sijui bado ni kwanini baadhi watanzania wenzangu mpaka sasa wameshindwa kutofautisha kati ya r na l. Hiyo huwa inanikera sana.

Nikiri hata girlfriend wangu ana huo uzembe. "Jamani laha sana" badala ya raha sana au saruni badala ya saluni.

Pia baadhi ya wana JF wanachangia sana kukiharibu kiswahili chetu. Mfano Magufuri badala ya Magufuli.

Tubadilike. Mimi ni Mwalimu wa hesabu nakipenda Kiswahili. Kenya isionekane ndio bingwa wa Kiswahili kwa uzembe wa baadhi yetu.
 
Kifimbo cheza wa tatu sasa baada ya yule wa gazeti la sani na yule dada wa jf.
 
Sijui bado ni kwanini baadhi watanzania wenzangu mpaka sasa wameshindwa kutofautisha kati ya r na l. Hiyo huwa inanikera sana. Nikiri hata girlfriend wangu ana huo uzembe. "Jamani laha sana" badala ya raha sana au saruni badala ya saluni. Pia baadhi ya wana jf wanachangia sana kukiharibu kiswahili chetu. Mfano Magufuri badala ya Magufuli. Tubadilike. Mimi ni Mwalim wa hesabu nakupenda Kiswahili. Kenya isionekane ndio bingwa wa Kiswahili kwa uzembe wa baadhi yetu.

Aisee sidhani kama unanishinda kwa kukereka na hao watu.
 
Sijui bado ni kwanini baadhi watanzania wenzangu mpaka sasa wameshindwa kutofautisha kati ya r na l. Hiyo huwa inanikera sana. Nikiri hata girlfriend wangu ana huo uzembe. "Jamani laha sana" badala ya raha sana au saruni badala ya saluni. Pia baadhi ya wana jf wanachangia sana kukiharibu kiswahili chetu. Mfano Magufuri badala ya Magufuli. Tubadilike. Mimi ni Mwalim wa hesabu nakupenda Kiswahili. Kenya isionekane ndio bingwa wa Kiswahili kwa uzembe wa baadhi yetu.
Hili ni tatizo la ngeli za kiarifa na matamshi kwenye ulimi kama ilivyo kigugumizi au kithembe
Wengine wanakosea kwa kuzungumza/kusoma tu na wengine wanakosea kwenye kuandika tu na wengine wanakosea kotekote
Pia kuna ambao ni tatizo la makuzi na mazoea jaribu kumwambia mchina atamke R uone atakavyopata shida
 
Watangazaji wa clouds na wasanii wa bongo fleva. Yaani wanaona sifa kuongea Kiswahili cha kijinga. Kwa kweli watanzania tunahitaji maombi maana wengi wetu wamekuwa wajinga wa kujitakia.
 
Kudhibitisha badala ya kuthibitisha. Hapa napo panahitaji marekebisho
 
Tatizo jingine ni wale wasiojua tofauti ya H na A. Unakuta mtu anaandika Akuna badala ya Hakuna; Amna badala ya Hamna; Ajaja badala ya Hajaja. Tatizo jingine ni neno Sio badala ya Siyo. Hii imenikera hadi kwenye bango la Mchepuko Sio dili la Kibonde badala ya kuandika Mchepuko Siyo dili. Ndio badala ya Ndiyo. Nina wasiwasi hata kwenye mitihani huwa wanaandika hivi hivi. Inakera sana.
 
Sijui bado ni kwanini baadhi watanzania wenzangu mpaka sasa wameshindwa kutofautisha kati ya r na l. Hiyo huwa inanikera sana. Nikiri hata girlfriend wangu ana huo uzembe. "Jamani laha sana" badala ya raha sana au saruni badala ya saluni. Pia baadhi ya wana jf wanachangia sana kukiharibu kiswahili chetu. Mfano Magufuri badala ya Magufuli. Tubadilike. Mimi ni Mwalim wa hesabu nakupenda Kiswahili. Kenya isionekane ndio bingwa wa Kiswahili kwa uzembe wa baadhi yetu.
Vipi umeona ilivyoshida hata kwako..."girlfriend" siyo kiswahili ndugu
 
Wewe mwenyewe una uhaba wa misamiati ya Kiswahili.

Neno "uzembe" umelitumia mahali pasipo stahiki.
Makosa uliyobainisha ni makosa ya kisarufi hukupaswa kutumia neno uzembe hapo.

Ushanikera.
 
Sijui bado ni kwanini baadhi watanzania wenzangu mpaka sasa wameshindwa kutofautisha kati ya r na l. Hiyo huwa inanikera sana. Nikiri hata girlfriend wangu ana huo uzembe. "Jamani laha sana" badala ya raha sana au saruni badala ya saluni. Pia baadhi ya wana jf wanachangia sana kukiharibu kiswahili chetu. Mfano Magufuri badala ya Magufuli. Tubadilike. Mimi ni Mwalim wa hesabu nakupenda Kiswahili. Kenya isionekane ndio bingwa wa Kiswahili kwa uzembe wa baadhi yetu.

Wakati mwingine siyo kosa letu.Kiswahili ni lugha ya Pili ya watanzania wengi.Kiswahili tumekikuta shuleni.Ndiyo maana kuna Pidgin inasaidia kuongea lugha ya kigeni katika lafudhi yako,mfano Nigerian English,Solomon Islands Pidgin.Hata kuna wasomi makini ila kiswahili chao kibovu.Wale ambao kiswahili ni lugha yao ya kwanza haiwapi shida.
 
Wewe mwenyewe una uhaba wa misamiati ya Kiswahili.

Neno "uzembe" umelitumia mahali pasipo stahiki.
Makosa uliyobainisha ni makosa ya kisarufi hukupaswa kutumia neno uzembe hapo.

Ushanikera.
Asante, nitajirekebisha. Hilo ni kosa la ndani zaidi
 
Msikereke kiasi hicho wakuu msichoke kutusahihisha makosa maana kiswahili fasaha ni kigumu kuriko pure mathematics au additional mathematics...
 
Back
Top Bottom