Ninakerwa na mabango ya waganga wa jadi jijini

Sinkala

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
1,773
683
Kumekuwepo na wimbi la uchafuzi wa jiji la Dar es Salaam kunakofanywa na masangoma ambao huwa hawachagui mahali pa kuyaweka matangazo ya shughuli zao, wanaweka popote tu hadi Airport kuna vitambaa vya matangazo. Sasa mimi ninauliza, ni mamlaka gani inayodhibiti uwekaji wa mabango? Hivi zile billboards za makampuni ya simu et al, si huwa zina utaratibu wa kulipia matangazo; hawa sangoma wanalipia? Nilitaka niweke picha mbili hapa, lakini nimeogopa kwani bado familia inanihitaji.
 
AK usimpe huyu bwana hadhi hiyo, mpambanaji ni yle anayekerwa na hali halisi na ku-act,chukua hatua!
Tulikuwa tunasema hivyo wakati wa enzi zetu kule kwnye ile organization machacharii kwenyebelimu na rushwa

Lakini unaju nchi hii haina mwenyewe! Unaweka bango, wakikwambia toa, unaingia ndani na kutoka na mapnga, mishale na marungu na kwaambia,
Anayethubutu kutoa bangi langu na afanye hivyo!
Ona pale kwa kakobe! Kama serikali ngangari mm ngunguri! Ndo mtindo wa kisasa....siipendi hali hii! And I will play my part
 
Kwa hiyo unakerwa kwa sababu yametapakaa kila sehemu au kwa sababu unafikiri hawalipi kodi?
 
Kwa hiyo unakerwa kwa sababu yametapakaa kila sehemu au kwa sababu unafikiri hawalipi kodi?
Yametapakaa na yanachafua mandhari ya mji. Unakuta mtu ameweka kitambaa, amekitoboa toboa halafu anakiweka kando ya barabara. Sipendi kabisa!
 
mabango yote hutangaza , Mganga toka Sumbawanga, Mganga toka Nigeria
dawa zinazouzwa, ni za nguvu za Kiume, mvuto wa kimapenzi, kutanua Hips, kuondoa nuksi na kusaidia kumvuta aliembali nawe.
 
Back
Top Bottom