Ninajiandaa kwenda kumshauri IGP afanye haya ili kudumisha Amani huko Mkuranga

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,545
22,050
Wadau habari zenu!
Mimi ni miongoni mwa watu wenye mipango ya kuishi maeneo ya mkuranga siku za usoni!
Nasikitishwa sana na matukio hayo yanayotokea maeneo ya pembezoni.
Kwa kifupi nimedhamilia kumtembelea IGP ofisini kwake ili nikamshauri haya machache!
1. Akae chini na viongozi Wa dini zote mbili (Islamic & Christian) ili wapange namna gani awaombe wafanye mikutano ya hadhara kuhusu mafundisho ya imani na upendo (ikiwezekana watoe ruzuku serikalini kufanikisha mikutano) hili litawajumuisha waumini wote pamoja na kutibu mioyo ya watu iliyoanza kujaa hofu, ( pia waombaji na wachungaji mahili sampuli ya kinagwajima watahubiri na kuombea waliovunjika moyo waponywe).
2. Waandae makongamano ya michezo na miziki ambapo vijiji vyote vishiriki kupata kombe la aman pamoja na kitita cha Pesa kuanzia washindi pamoja nawashiriki wasiachwe kupewa chochote! Na itapendeza zaidi jeshi la police/jkt/jwtz na magereza nao wakaingiza timu zao kushiriki hata kama wataazima baadhi wachezaji raia! Michezo hiyo isiwasahau makundi mengine kama miziki, ngoma na ile ya wakuu Wa vikosi angalau hata washiriki Kwa kuvuta kamba.
3. Wakati hayo yakiendelea kikosi kazi cha Interijensia wajichanganye humo humo kufanya yao talatibu.
4. Waalike mabenk na taasis zingine zitakazoleta fursa Kwa wanachi.
*************************
Hayo pamoja na mawazo yenu mtakayochangia na mengine mengi niliyo nayo natarajia kwenda kumshauri IGP rafiki yetu/ mzee wetu MANGU naimani atayafanyia kazi!
Kulaumu tu hakutasaidia chochote!
Wacha nijitose na hizi nondo mbali na hapo inabidi nikachukue Tunguri kijijini.
 
Mwambie pia aiombe serkali ktk ngaz husika,wafungue kambi ya jeshi..
kuna mapori ya kutosha huko.
 
Andaa Watu wa kukuwekea dhamana kabla hujaenda kushauri!

Pia iandae Familia Yako kisaikolojia kwa Upekuzi wa kustukiza Nyumbani
 
Sirikali imeshindwa kudukua ila mie nimejua tatizo hadi sasa ni ardhi . Kama mnabisha mtaona
 
Mleta mada ana hoja , nami naamini ubabe hautasidia Bali utaumiza wasiohusika kabisa.

Hapo kwenye viongozi wa dini ni mahali pake na wasiwe wanafki wa kuhubiri amani majukwaani huku kwa waumini wao wanahimiza jihad, hatutafanikiwa kwa unafki.
 
haujui ila najua ndio hilo la ardhi serikali ilipokonya mashamba na viwanja tena huko kuna watu wanachimba dhahabu uongo ukweli ?
Mimi ni mkazi wa huku na ndugu zangu washauwawa katika sakata hili mmoja wao alikuwa mwenyekiti .... Hakuna dhahabu around here
 
kuwakusanyia watu wengi ni kuwarahisishia mauaji ya watu wengi..

serikali ianzishe kambi za jeshi Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mafia kuthibiti mapori kutumia na majambazi
 
Sirikali imeshindwa kudukua ila mie nimejua tatizo hadi sasa ni ardhi . Kama mnabisha mtaona
Wala sio ardhi,,, kule kuna tatizo zaidi ya ilo Mkuu, ,,,police inatakiwa wasitumie panic,, Tiss inatakiwa wajichimbie kule ili wajue kiini,,,ila nahisi kuna jambo wamefanyiwa au huwa wanafanyiwa watu wa huko sasa wanalipiza,,,au kuna kitu kikubwa zaidi,au kuna watu wenye itikadi Kali tofauti na dini inavyosema,kwaiyo wanataka kulazimisha umma wa huko ufuate itikadi yao kali tofauti na misingi ya imani ilivyo, ,
 
Mawazo yako ni mazuri lkn hiyo ya kuweka music au kumwita gwajima sidhani kama utawapata raia wa kuhudhuria kwa kiasi ulichofikiri!! Hapo labda hizo semina ziwahusishe masheikh wenye ilmu kubwa ya dini kama vile Kassim mafuta,khamis Ame,Juma pori,Abuu Hatim,sheikh mujahid hawa wana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuelezea uzushi wa haya makundi ya fikra potovu yanayojinasibisha na uislam!! Kule hata ukiwapeleka bakwata hawatasikilizwa chochote maana ndani ya bakwata wenye ilmu ya dini kwa uwezo wa kujenga hoja ni wachache sana na wengi wao hata kusoma qurani shida je unategemea wataongea nini mbele ya baadhi ya watu ambao wameathirika na fikra khawarij (_ugaidi)!!
Tatizo linalopelekea baadhi ya vijana wa kiislam kujiunga na haya makundi ni ukosefu wa elimu ya dini nowadays vijana wengi wakiislamu hawasomi dini yao na wamebaki kukumbatia ushabiki tu ndo maana ilikuwa ukisikia maandamano tu frontline utakuta vijana wamejazana kwa akili zao walikuwa wakidhani wanaitetea dini kumbe wanaichafua dini (kwa hakika uislamu haukubali maandamano na maandamano si ktk mila za kiislamu) sasa vijana wa type hii wakishawishiwa kujiunga na kuanzisha hivi vikundi inakuwa rahisi kwao kukubali kujiunga kutokana na kukosa (tamayyuz-upembanuzi wa kujua kuwa hili linafaa au halifai ktk dini) Na ili mtu awe na huo upembanuzi ni lzm asome dini....
Uislamu hauruhusu mauaji ya aina yeyote, uislamu unatutaka waislamu kuheshimu mamlaka (serikali),uislamu unatutaka waislamu kwa wanyenyekevu ,uislamu unatutaka waislamu kuwa na subra haya yote Leo hii hayazingatiwi
SERIKALI IFANYE NINI?
1:Ishirikishe viongozi wa dini ktk kuifundisha jamii kuhusu uhatari,athari na uharamu wa haya makundi......Hapa kunahitaji masheikh wenye elimu hasa ya dini na wenye uwezo wa kujenga hoja maana inabidi watu wapewe nafasi ya kuwauliza maswali hawa masheikh na kujibiwa papo hapo--Njia hii imesaidia sana kuondoa fikra hizi potofu kwa baadhi ya vijana ambao mpk sasa wanasoma dini na wanavipinga hivi vikundi na Kubota had garish a mitaani hivi vikundi
2:serikali itumie intellejensia yake ktk kubaini wahusika wa haya matukio (Ni vizuri mkawatumia waislamu ktk kubaini..nadhani hapa inaeleweka! sio lzm kila mtu aelewe point hii) Waislamu wako tyar kuipa support serikali maana wao ndo wahanga wakubwa wa hili tatizo na hata ukifatilia wengi wa wenyeviti na wajumbe waliokufa kule ni waislamu tena kuna mpk maimamu wameuwawa na hivi vikundi
3:ukiona kuna vijana wa hapo hapo mkuranga wamekuwa trained na wamekuwa na uwezo wa kufanya haya matukio basi jua hapo kuna kiongozi wa hilo kundi,kuna walimu wa hilo kundi hivyo sasa serikali inahtaji kuwakamata baadhi ya hao wahusika wakiwa hai ili kuweza kumaliza mtandao mzima wa haya makundi
4:Nimeangalia clip ya mahojiano ya mama mzazi wa kijana mdogo (24years) alouwawa na Polisi akipambana na Polisi.......Katika Yale mahojiano mtangazaji alimuuliza mama mzazi kama ana taarifa kuwa mwanae alienda somalia (note it) Mama akajibu mi sijui maana hata Mimi mzazi wake alinipiga marufuku nisifike kwake kwa kuwa Mimi natembea uchi!!
 
Wala sio ardhi,,, kule kuna tatizo zaidi ya ilo Mkuu, ,,,police inatakiwa wasitumie panic,, Tiss inatakiwa wajichimbie kule ili wajue kiini,,,ila nahisi kuna jambo wamefanyiwa au huwa wanafanyiwa watu wa huko sasa wanalipiza,,,au kuna kitu kikubwa zaidi,au kuna watu wenye itikadi Kali tofauti na dini inavyosema,kwaiyo wanataka kulazimisha umma wa huko ufuate itikadi yao kali tofauti na misingi ya imani ilivyo, ,
We umeongea kweli ila kuna kaukweli kwenye bandiko lako
Mmenyanyasa watu huko kisa ardhi .
 
Back
Top Bottom