Ninahoji UMAKINI na UADILIFU wa Dr Slaa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ninahoji UMAKINI na UADILIFU wa Dr Slaa!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMARADE, Oct 28, 2010.

 1. K

  KAMARADE Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Kamarade wa Kamarade

  Katika mazingira ya sasa ambapo dunia imelazimishwa kuamini kuwa kuna tofauti ndogo sana kati ya Uislamu na Ugaidi, ninaingiwa na wasiwasi sana na hatua ya Dr Slaa kumuita Kikwete ni gaidi na kuwa chama chake ni cha magaidi.

  Wasiwasi wangu unatilia maanani pia kuwa uchaguzi wa wiki hii unaenda katika historia kuwa ni uchaguzi ulionyesha dalili zote za mgawanyiko wa ufuasi wa wagombea katika misingi ya udini zaidi ya misingi ya uchama kama ambavyo tulizoea hapo kabla.

  Kauli mbiu ya mgombea wa CHADEMA mwaka huu, yaani Dr Wilboard Slaa ni UADILIFU, UMAKINI na UWAJIBIKAJI.

  Kauli ya Dr Slaa ya siku ya Jumanne tarehe 26 Oktoba katika viwanja vya Temeke Mwembe Yanga, ambapo safari yake ya kugombea urais ilianza isivyo rasmi miaka mitatu iliyopita, pamoja na kauli nyingine alizotoa tangia kampeni hizi zianze, zinanifanya nijiulize maswali magumu ambayo wangi wetu tulishindwa kufanya hapo kabla kutokana na sababu mbalimbali.

  Ni jana tu katika gazeti la Majira iliripotiwa kuwa Dr Slaa alidai kuwa yeye siye aliyeanzisha udini isipokuwa ni mgombea wa CCM Jakaya Kikwete. Amedai kuwa Kikwete amekuwa akitumia nafasi yake kupendelea Waislamu. Na pia amedai kuwa hata timu yake ya kampeni ya Kikwete ni ya waislamu watupu na pia mgombea mwenza wake naye pia ni Muislamu.

  Lakini mbali na kauli hizi, Dr Slaa amewahi kukaririwa huko Iringa akidai kuwa karibu nusu ya maafisa wa usalama wa taifa wanaripoti kwake. Tamko ambalo ukichukulia historia yake ya kufanya kazi katika ikulu yetu na dhana iliyojengeneka kuwa kashfa mbalimbali ambazo amekuwa akiibua amekuwa anazipata kutoka kwa watu wake katika Idara hiyo nyeti ya Usalama wa taifa letu, ni wazi halikupaswa kutolewa jukwaani kama alivyofanya Dr Slaa.

  Hatari ya tamko hilo ni kuwa mara baada ya uchaguzi hali haitakuwa shwari huko katika vyombo vyetu nyeti. Ni wazi matamko kama haya yameshaleta mgawanyiko mkubwa na hali ya kutokuaminiana kati yao kwa kiasi kikubwa. Hali ambayo inaweza kuleta madhara makubwa kwa usalama wa taifa letu. Tumeyaona hayo huko Zanzibar, hatupaswi kuwa wahanga wa madhara ya hali hiyo na upande huu wa nchi yetu.

  Siku hiyo alipotoa madai hayo pia alitoa madai kuwa lile tamko la kuwataka watanzania kuwa makini na watu wanaotishia kumwaga damu wakati wa uchaguzi lilikuwa ni tamko la Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo yeye kama binafsi.

  Aliendelea kudai kuwa alifanya Afande Shimbo alifanya hivyo ili kutetea maslahi yake binafasi. Dr Slaa alidai kuwa ana ushahidi kuwa Shimbo kama alivyomwita, amepewa kile alichoita dili la kifisadi la kuingiza matrekta madogomadogo nchini.

  Kuanzia hili la kuwa tamko lile lilikuwa ni la Jeshi na sio la vyombo vya ulinzi na uslama ni wazi Dr Slaa ameonyesha dalili za kukosa umakini kama rais mtarajiwa. Nasema hivi kwa sababu najua kuwa kwa uzoefu wake wa masuala ya usalama na utawala katika nchi yetu, alijua wazi kuwa lile halikuwa ni tamko la jeshi bali ni tamko la Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa ambayo Dr Slaa anaijua na anajua utendaji wake na majukumu yake.

  Lakini pia Dr Slaa kama rais mtarajiwa naamini anajua wazi kuwa Luteni Jenerali Shimbo katika taratibu za majeshi yetu ndiye alikuwa mkubwa kati ya wasemaji wa vyombo vingine vya ulinzi na usalama waliokuwepo naye siku ile. Hawa ni pamoja na Kamishina Venance Tosi wa Jeshi la Polisi na Afande Kivuyo ambaye ndiye msemaji wa masuala ya intelijensia ya jeshi la Polisi.

  Ni wazi kiutaratibu ni Jenerali Shimbo ambaye kwa muda sasa ndiye amekuwa msemaji wa Jeshi la Ulinzi akiwa kama afisa wa ngazi ya juu miongoni mwa watatu hao ndiye alipaswa kulisoma tamko liloandaliwa na kupitishwa na wakuu wa majeshi yetu pamoja na wale wa vyombo vingine vya usalama na sio kuwa tamko lilikuwa ni tamko lake.

  Lakini kitendo cha Dr Slaa kuanza kudai kuwa Jenerali Shimbo ana biashara ya kifisadi ya matrekta ilikuwa ni upotoshaji wa hali ya juu kwani ni wazi anajua kuwa katika jeshi letu kuna kitengo cha biashara kinajulikana kama SUMA JKT. Na kwa kushirikiana na Jeshi letu la Ulinzi ambao ndio waliwezeshwa na serikali kusimamia mradi wa matrekta hayo zaidi ya elfu moja, SUMA JKT ndiyo yenye utaalamu wa kutekeleza jukumu la kuyafikisha kwa walengwa na pia kuangalia uwezekano wa kujifundisha teknolojia yake ili hapo baadae jeshi letu kupitia kiwanda chake cha Nyumbu kuweza kuyatengeneza hapa hapa nchini.

  Ni wazi kuwa Dr Slaa hakuwa makini ama kwa kutofuatilia ukweli kuhusu madai kwamba kazi hiyo ni kwa manufaa ya Jenerali Shimbo, lakini pia haingii akilini kwa mtu yeyote mwenye chembe ya umakini kuanza kuanzisha uhasama na vyombo vya ulinzi na haswa jeshi letu akiwa safarini kuelekea Ikulu.

  Kuhusiana na matamshi yake kuwa Jakaya Kikwete amekuwa akiwapendelea Waislamu, maneno ambayo pia yamekuwa yakiongelewa kichinichini katika vibaraza mbalimbali na hata katika nyumba za ibada, ni wazi Dr Slaa kama mgombea wa nafasi nyeti ya Urais hakupaswa hata kuthubutu kuyafikiria ukiachilia mbali kuyasema hadharani. Alichofanya Dr Slaa ni kuyafikisha manung’aniko hayo yasiyo na chembe ya ukweli katika majukwaa ya kisiasa.

  Dr Slaa ametangaza rasmi kuwa mapambano ya chinichini kwa chini kati ya maslahi ya Watanzania wafuasi wa dini ya kiislamu kwa upande mmoja na Watanzania wafuasi wa dini ya Kikristo kwa upande mwengine ni mapambano ya kisasa na sio kijamii kama tulivyozoea hapo kabla.

  Lakini pia kwa mujibu wa taarifa zilizokuwa zikizunguka katika radio mbao za jiji letu ni kuwa Dr Slaa kwa kutumia nafasi yake kama Katibu Mkuu wa chama chake, amewashauri na kukubaliwa na Meneja wa Kampeni wake Prof Baregu kuwaamuru wagombea wao kuwasiliana na Maaskofu wa Kanisa la Katoliki katika majimbo yao ili waweze kutumia “mtandao wa kanisa” kulinda kura zao dhidi ya “hujuma za CCM”.

  Ukichukulia hayo na hili la leo, ni wazi kuwa ama Dr Slaa ana mapungufu makubwa katika Umakini anaoupigia kauli mbiu ama basi zile dalili za kuwa anaweza kushinda na kuukwa urais siku chache zijazo zimemchanganya kiasi cha kumfanya kuwa tayari kufanya lolote lile ili kuhakikisha kuwa anapata kila kura anayoweza. Hata kama itabidi kuigawa nchi katika mapande mapande.

  Zaidi ya matamshi hayo, Dr Slaa ambaye amekuwa akiahidi uendeshaji wa serikali makini pindi atakapochaguliwa, huko nyuma amekuwa akifanya makosa mbalimbali ambayo nayo pia yanaibua maswali na hoja kadhaa kuhusiana na umakini wake kama Rais Mtarajiwa.

  Moja ya matendo hayo ni jinsi gani alivyolishughulikia suala la mahusiano yake na mwanamama mmoja ambaye yasemekana ni mke halali wa mtu mwengine. Kati ya mambo ambayo amekuwa akidai kama utetezi wake ni lile la kuwe eti hakujua kuwa mwanamama yule ni mke wa mtu na hivyo hana kosa kisheria wala kimaadili.

  Kwa mtu yeyote anayethamini heshima ya Urais, changamoto na majukumu yake, ni wazi atajiuliza maswali mengi zaidi kutokana na utetezi kama huu.

  Hivi kweli yawezekana kabisa mtu ambaye hata kabla hajatangazwa kuwa mgombea Urais kupitia chama chake ilikuwa ni siri ya wazi kuwa ndiye alikuwa na nafasi kubwa kama sio pekee ya kugombea urais wa nchi kujiingiza katika mahusiano na mwanamke na hata kufikia kuishi naye pamoja na watoto wa mwanamke huyo bila ya kuhoji hali halisi ya mahusiano ya mwanamke huyo na baba watoto wake. Hili linaleta maswali pia kuhusiana na uthabiti na umakini wa chama chake kwa ujumla.

  Lakini je historia inatufundisha nini jinsi ya wale kina mama na kina baba ambao wanaonyesha dalili za kuwa watu wakubwa kidunia ambao hubambikiwa wenza ambao ama wana nia ya kuhakikisha wanafikia kiti cha enzi wakiwa nao ili kuhakikisha maslahi yao ama kikundi Fulani nyuma yake ama wale ambao hupenyezwa kwao pengine hata na vyombo vya dola ama makundi ambayo yana nia ya kukudhuru huko mbeleni, iwe kisiasa ama maisha.

  Na kama ni kweli kuwa Dr Slaa amekuja kujua ukweli huo na hivyo kuthibitishia umma kuwa mwanamke huyo hakuwa mkweli kwake katika karibia mwaka na zaidi waliokuwa wakiishi pamoja, iweje aendelee kuwa na imani na mtu kama huyo na zaidi kupanda naye na kumuweka mbele katika majukwaa ya kisiasa.

  Lakini hili pia linaleta maswali mengine. Suala la Uadilifu analolitumia kama kauli mbiu ama dira ya utawala wake kama akishinda.

  Hivi katika dunia yetu hii ambayo wazee tumekuwa tukipigia makelele sana janga la kushuka kwa maadili kwa vijana wetu, ni mfano gani ambao Dr Slaa anauonyesha mbele ya vijana na watoto zetu. Ni maadili gani anayo halalisha kwa makeke kiasi hicho kama ambavyo wale anaowaita kuwa ni maifsadi wafanyavyo?

  Lakini pia hili la Uadilifu linakwenda zaidi ya hapo.

  Dr Slaa akiwa kama Katibu Mkuu wa CHADEMA na kwa mujibu wa katiba yao ndiye anayepaswa kuwa msimamizi mkuu wa masuala yote ya kifedha. Lakini pia ndiye anayepaswa kusimamia na kuripoti ipasavyo matumizi yote ya fedha yakiwemo yale ya ruzuku ambayo ni kodi yetu anayotuahidi kuwa anaenda kuiokoa mikononi mwa wale tuwaitao mafisadi.

  Kwa mujibu wa Mkaguzi Mkuu wa mahesabu ya serikali hivi karibuni, alitaarifu kuwa tangia miaka miwili iliyopita baada ya sheria ya kumpa wajibu wa kukagua matumizi ya fedha za ruzuku ziendazo katika vyama vya siasa, ni CCM tu ndiyo waliowahi kuwasilisha mahesabu yao kwake. Akiwa na maana hakuna chama kingine chochote kikwemo CHADEMA ambacho kimetekeleza jukumu hilo la kiuadilifu. Hili linaleta swali kubwa kuhusu Uadilifu wa Dr Slaa na pia chama chake.

  Lakini pia wakati wa mapambano makali kati ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA marehemu Chacha Wangwe, kulikuwa na taarifa ama tuhuma kuwa Dr Slaa aliamuru vijana wake akiwemo John Mnyika na mwengine aliyetajwa kama Mtemelwa, kukusanya risiti bandia ili ziweze kuwakilishwa kwa wafadhili wa chama hicho huko ughaibuni. Kwa mujibu wa madai hayo, mambo hayo yalifanyika mara baadaya Uchaguzi wa mwaka 2005. Hili nalo linaleta maswali magumu kuhusu uadilifu anaoahidi Dr Slaa na CHADEMA kama chama.

  Zaidi ya hayo, kumekuwa na madai miongoni mwa viongozi wa CHADEMA kulumbana kutokana na Dr Slaa kama Katibu Mkuu na Mkuu wa Sekretariat ya chama hicho kushindwa kuwasilisha mahesabu ya mapato na matumizi ya chama hicho kwa miaka takribani mitano sasa katika Baraza Kuu la chama kama ambavyo katiba ya chama hicho inavyotaka.

  Mbaya zaidi hata sasa wakati kukiwa na sheria kali ya Matumizi ya Fedha katika Uchaguzi ambayo Dr Slaa alikuwa mmoja wa vinara wa kuipigia kelele kupelekwa bungeni na kupitishwa, yapo malalamiko kuwa kiasi kikubwa cha fedha ambazo wafadhili mbalimbali wa chama hicho wamekuwa wakizitoa kabla na baada ya kuanza kwa kampeni hazijawakilishwa kwa mhazini wa kamati ya kampeni anayetajwa kwa jina la Sussan.

  Hii ni pamoja na zile shilingi milioni 100 ambazo miezi kadhaa iliyopita zilitolewa kwa mbwembwe na mfanyabiashara machachari Mzee Sabodo. Fedha ambazo inadaiwa kuwa tangia Mwenyekiti Mbowe apokee cheki yake, amekataa kuziwasilisha kwa mweka hazina wa kampeni wala Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho na kuamua kuenda nazo huko Uchina ambako yasemekeana alifanya manunuzi ya vifaa vya kampeni bila ya kuwahusisha wahusika. Na hadi sasa hakuna mahesabu aliyoripoti ama kukabidhi kwa chama.

  Na hili sio mara ya kwanza kutokea na mbaya zaidi ni mambo ambayo yamezoeleka ndani ya CHADEMA yakiwa na baraka za Dr Slaa kama katibu mkuu na msimamizi mkuu wa fedha wa chama.

  Kauli mbiu hii ya Uadilifu huu pia inatikiswa na madai ya kuwepo kwa jitihada za Mwenyekiti wa CHADEMA Bwana Mbowe, alikuwa akijaribu kulazimisha wale wanao daiwa ni watu wake kuwekwa katika nafasi za juu za wateule wa viti maalumu bungeni wa chama hicho tofauti na alama na vigezo vyao halisi. Taarifa hizo zilidai kuwa katika hili Dr Slaa aliungana mkono na Mwenyekiti wake na hivyo kuwalazimisha wazee wa chama hicho kuja juu na kumpinga Mwenyekiti wao hadharani kwa mara ya kwanza.

  Hayo yamefanyika sasa baada ya miaka mitano ya chama hicho kutikiswa na madai kama hayo katika uteuzi wa wabunge wa viti maalumu waliokiwakilisha chama hicho miaka mitano iliyopita.

  Mambo kama haya siyo tu yanahoji uthabiti wa hoja ya Uadilifu na Umakini ambayo Dr Slaa na CHADEMA wamekuwa wakiitumia kuikosoa CCM na kuwaahidi watanzania kuwa wataisimamia ipasavyo lakini pia linazua maswali dhidi ya umakini wa Dr Slaa kama kiongozi ambaye anaweza kupewa ridhaa ya watanzania kuliongoza taifa katika jitihada za kurudisha umakini, uadilifu na uwajibikaji.

  Nimeamua kuhoji haya sasa kwa kuwa hapo mwanzo wengi tulidhani kuwa Dr Slaa hataweza kushinda na CHADEMA wataweza tu kuongeza viti bungeni, jambo ambalo wengi tungependa kuona likitokea.

  Lakini ukweli ni kuwa hivi sasa kumejengeka hisia ya kuwa kuna uwezekano wa Dr Slaa kushinda uchaguzi na kuwa Rais wetu atakeyekabidhiwa mamlaka ya kuongoza taifa letu lakini zaidi vyombo vyetu vya dola. Jukumu ambalo hata kama tumezoea kuona likiwa mikononi mwa watu wenye UADILIFU wa kutia mashaka lakini kamwe hatujawahi kuona na hivyo kuzoea kukabidhiwa mtu aliyekosa UMAKINI.

  Na hivyo ni wajibu wetu kuhoji ili hata kama tutakuwa tumechelewa kuepusha gharika la kuwa na Amiri Jeshi Mkuu mwenye UMAKINI unaotia shaka, basi angalao hoja hizi zikawepo katika makarabsha ya historia ya nchi yetu.
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Nadhani muda wa kuhoji umeisha sasa ni vitendo na jamaa ndio huyooo kwa IKULU
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ccm ni chama cha kigsidi, kimeunda genge la wahuni , genge la wanamgambo genge hilo linaitwa green Guard
  ni magaidi ndio , hawafai kabisa.
   
 4. T

  The King JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabongo wameamka ndugu si wale wa kichwa cha mwendawazimu. Kwanza mlianza kwamba kaiba mke wa mtu mkapiga chini Rais Mtarajiwa akaendelea kupeta tu na kuvuta umati mkubwa wa Watanzania kila alipopita. Mkasema kwamba ana ukabila na usini lakini bado wabongo wakapangua porojo zenu, mkadai kwamba anataka kusababisha umwagaji damu nchini hizo porojo nazo zikapigwa chini na Watanzania sasa kiwewe kimewazidi na matumbo joto. Mjiandae tu kuondoka kwa amani na kuiacha nchi salama salmini. Bye bye thithiem na mafisadi wenu.
   
 5. Catagena

  Catagena Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angalia safu za uongozi ya Mheshimiwa JK
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Makala ndefu namna hiyo?

  Hiyo kasome wewe na mkeo/mumeo tu mama.
   
 7. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kamarade< Hoja yako ni too late. Huwezi kuwabadilisha, nenda jiunge nao kumpigia Kura Dr. Slaa
   
 8. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Unahoji....Wakati Upigi...Kula....!!!Utakuta wewe na makamba hampigi Kula.Mwanachama wa JF..Mchanga kama wewe....Tunaweza hoji uadilifu na uzoefu wako...ambao tunamashaka nao....Hujachangia hata kwa thumuni...
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Chapisha vijalida gawa nchi nzima au mpelekee RIZ 1 kama huna pesa akusaidie!
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wewe ni katika wanafiki tulionao katika nchi yetu.kama kweli unaipenda familia yako unanunua shuka wakati wa baridi halafu unawaletea asubuhi.umechelewa kaka.kwa vigezo tofauti wote si wakamilifu hata kikwete aliwahi kusema kwamba hajui matatizo yetu yanatokana na nini na bado tulijaribu kumwamini na yaliyotokea wote tumeshuhudia.kwa kauli yake ametamka kama si kwenda ughaibuni kuomba msaada wote tungekufa njaa.
  sasa kwa kauli kama hizo je hapo tuna mtu makini kweli?suala la uadilifu kwa kikwete tusilijadili kwa sababu ni 0.suala la unyumba kwa tanzania naweza kumtetea dr shein peke yake wengine wote ni vimeo.
  huyo unayetaka kumpigia debe ndiye hovyo kabisa kwa suala la nyumba ndogo.ukiwa ikulu heri ndoa moja yenye mgogoro kuliko vimada kumi waliotulia.kauli kama hizi naomba uzitolee ufafanuzi kwa maslahi ya nchi,wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni ni vihererhere vyao,ukitaka kula lazima uliwe,nisingeenda kuomba mngekufa njaa,rostam,lowasa,mramba,mwakalebela ni watu safi.
  kwa hoja zako na jinsi tunavyomfahamu kikwete ni kwamba hapo hakuna mtu anayefaa wote ni pumba.sasa kama pumba moja nia ya mchele na nyingine ni ya mahindi tuchague moja.moja tuionja kwa mika mitano tumevimbiwa sasa hiyo nyingine hatujaionja na tuionje.
  aliye kutuma kamwambie sijawakuta watanzania.
   
 11. rennychiwa

  rennychiwa Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ndugu yangu imefikia hatua watu wanasema Hapana, hatutaki kudanganywa tena, tunataka mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu. Tumechoshwa na propaganda ambazo hazina kichwa wala miguu.

  Kazi ya green guard unaijua vizuli? Mfumo wa uongozi ndani ya CCM unauelewa? Maisha yao binafsi yaani wana wake wangapi, vimada, watoto nje ya ndoa? Sizani kama unaelewa vizuri jaribu kuwachambua wagombea wote kwa kina afu utaona wapi utapiga kura yako. Dhamira yako itakusuta.

  CCM kimekosa mwelekeo, kimeshindwa kuwavuna vijana makini, kimeshindwa kulinda maslai ya wengi, hakitaki kukosolewa, kimekosa washauri wazuri sasa kimezeeka kinataka kurudi ujana watu wanasema hapana. Ndio maana hata nyinyi mnaoandika hizo mada hamjui hili na kama mnalijua basi mnaogopa kusema ukweli kwa maslai yenu binafsi.

  Hata mwalimu Nyerere (Hayati) aliwakosoa wana CCM waziwazi hata kudiriki kuwaita wengine wahuni na walafi. CCM ya leo ni ya kupokezana vijiti bila ya kujua anayekipokea anauwezo wa kukimbia ama la. Someni alama za nyakati, watu wameamka watu wameijua nchi yao, watu wamejua thamani ya kura yao. Nyie endeleeni na propaganda, nguvu ya umma ndiyo itakayo amua kama si leo basi kesho.

  Mabadiliko chanya Tanzania yanawezekana. Tumia kura yako vizuri.
   
 12. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu huu si wakati wa kuhoji bali kuamua mustakabali wa maisha ya taifa hili kwa sasa na vizazi vijavyo.
   
 13. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ndiyo Thesis yako? Subiri Phd kama ya JK.
   
 14. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata kama kamarade angeandika kurasa kumi kumtetea jk wake,hataweza kuyabadili mawazo na maamuzi ya watanzania ambao wameshaamua mabadiliko.pole bwana kamarade
   
 15. P

  Preacher JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  YAANI THREAD HII IMENIBOA SANA - UNYUMBA WA DR. SLAA HATUUHUSU - MBONA RAISI Mk........... ALICHANGIA MKE NA WAZIRI Mr.......???NA HAMJASEMA LOLOTE???? UMEMKALIA KOONI DR. SLAA WA WATU.... MSHINDWE NA MLEGEE............. SIE TUNATAKA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA - HIYO MICHANGANUO INAKUFAA WEWE NA VIBARAKA WALIOKUTUMA - KWANZA UNAPATA FAIDA GANI KUMCHANGANUA DR. SLAA???????????????????????? MWENZIO ANAKUBALIKA NA WATANZANIA - NA WENYE WIVU WAJINYONGE ........ WATU WAMEJIPANGA KUMPA KURA YA "NDIO"

  SO....................AMUA ....... ILA USHAURI WA BURE - UKIENDA KUPIGA KURA - CHAGUA DR. SLAA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU
   
 16. T

  Thadeus JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 24, 2007
  Messages: 267
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  kALAGHABAHO!!!!!
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  [​IMG]
   
 18. B

  Bwassa Member

  #18
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Jamani,

  Tusidanganyane hapa kwenye Forum kuwa eti Dk. Wilbrod Slaa atashinda kiti cha Rais! Hakuna vigezo vyovyote vya kisayansi vinavyoashiria jambo hilo, labda hii "Opinion Poll" ya Jamii Forum, ambayo imethibitika dhahiri kuwa ni ya kuchakachua!

  Fikiria yafuatayo:-
  · Dk. Slaa hana uzoefu wowote wa uongozi wa Kiserikali;
  · Uongozi wa Kanisa umemshinda;
  · Uadilifu wake unatia shaka (kuiba mke wa mtu, kuishi na mwanamama muda mrefu bila ya kumuoa rasmi, kuchukua pesa za walemavu mpaka wakamuondoa uongozi wa Kanisa);
  · Katika Bunge (alikokimbilia kufanya kazi ya Siasa baada ya kushindwa kabisa, tena kwa aibu, kumtumikia Bwana!) kazi yake ni kuvurumisha "mabomu" tu, hana jipya (kama "mabomu" yanampeleka mtu Ikulu, Augustine Lyatonga Mrema angekuwa Rais wetu mwaka 1995!).
  Mtakuja kuabika humu katika JamiiForum baada ya Oktoba 31! Mtaishia kusema "CCM, imeiba kura" (wimbo wa wanasiasa wa upinzani Tanzania, uliochosha masikioni)! Isitoshe, Urais si wa kumjaribu mtu, ukitaka waulize Waganda walivyomjaribu Iddi Amin aliyempindua Rais Milton Obote au Wazambia walivyomjaribu Chiluba (aliyekuwa anapasua "mabomu" dhidi ya UNIP hadi akamtia ndani Rais Kenneth Kaunda)!

  Chagua CCM iliyotimiza ahadi zake:-

  · Barabara za lami zimejengwa (ya Kigoma Kaskazini kwenda Burundi, Zito Kabwe anadai sasa katika kampeni zake za Chadema, kuwa eti anajenga yeye!);
  · Kwenda Mwanza tulikuwa tunapitia Nairobi, sasa tunakwenda moja kwa moja tu, kwa siku moja;
  · Vijana wetu, tena watoto wa masikini, wanaofaulu Shule ya Msingi sasa wanaingia Sekondari kwa wingi kwa kuwa kila Kata ina Sekondari;
  · Tuna Vyuo Vikuu 33 sasa na kikubwa cha umma cha Dodoma kitakachochukua wanafunzi 40,000 kwa mkupuo, kimeanza kazi;
  · Tuna chakula cha kutosha hivi sasa nchini (Kenya sasa wanahemea na kuponea Tanzania!) mpaka Serikali imerusu tuuze nje kwa wenye njaa wa huko;
  · Zanzibar sasa shwari, baada ya Rais Kikwete kutimiza ahadi yake ya kulipatia ufumbuzi suala la uhasama wa kisiasa (tumesuluhishana wenyewe na hatukumhitaji Kofi Annan!).

  Tusidanyike!

  Bwassa
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Iyo article ukiipeleka habari leo au RAI naona unaweza ambulia mshiko
  Ambatana na wanaompigia Kura ya ndio Slaa bse upepo wa ushindo ndo unako elekea
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  well done Kamaharage...

  You have effectively used your citizen's rights

  clap...clap!!!
   
Loading...