G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Kutokana na kuzembea kupita kiasi kwa serikali ya awamu ya tano kupambana na Dengue mwaka huu, na athari kubwa tulizoona kutokana na homa hiyo. Huenda tukaenda kukumbwa na Ebola. Je wizara imejiandaa?
Kusema kweli wizara ya afya sasa sijui ni woga au nini wamekuwa hawajishughulishi na mapambano ya homa za milipuko kama dengue na zile zenye hatari kubwa ya kulipuka kama Ebola.
Je tumeandaa mazingira ya kupambana na ugonjwa huo au itakuwa kama dengue? Inasikitisha sana mathalan wakati watanzania kadhaa wa Dar es Salaam walikuwa wakiteswa na dengue, kipimo cha homa hiyo kwenye hospitali kadhaa kilikuwa kikipatikana kwa bei ya ghali sana ikilinganishwa na udharura wa ugonjwa huo hali inayoonyesha kuwa ni kama wizara haikujishughulisha kikamilifu na homa hiyo.
Niiombe serikali ya awamu hii iache kuwaachia wananchi kujipambania na majanga yao. Hii ni dhana iliyojengeka na inaonyesha ni kama imekuwa. Tumeshuhudia majanga ya njaa, tetemeko, uharibifu wa mazao na kukosekana kwa masoko ya mazao ni mifano tosha inayotuonyesha kuwa serikali ya awamu ya tano imeaumua kujiweka mbali na shughuli za dharura zinazotokea kwenye jamii. Kwa maana hiyo basi jitihada za kupambana na Ebola ambayo inaonyesha viashiria vingi kutua nchini ziwekwe ili lisijekugeuka tena kuwa janga litakalotafuna maelfu ya watanzania na kuwaweka vitandani kama ilivyokuwa kwa homa ya dengue.