Ninahisi nimebugi, nataka tuandikishiane nimpe milioni 5 ya msingi. Anipe mwanangu atakapofikisha umri

Habari, Nimesoma maelezo yako na kuyaelewa ifuatavyo:-

Mosi, Ulifiwa na mke/mpenzi wako akiwa na kichanga tumboni hivyo kwa sasa huna mtoto lakini unahitaji mtoto kwa hali yoyote ukizingatia umri unakwenda na wenzio wenye umri kama wako wana watoto.

Pili, Uwezo wako kiuchumi siyo mbaya (uchumi wa kati) hivyo pesa ya mambo madogo madogo haikupigi chenga ikiwepo na ya kutuma nyumbani ambapo unauguza mama yako.

Tatu, Umepata mpenzi wa kijaluo mwenye mtoto wa umri wa miaka tisa (9) na yeye ana hamu ya kuolewa na kwa kuwa umeonyesha uwezo wa kumlea mwanae anataka umuoe haraka bila kujali unayoyapitia kwa sasa.

Ushauri wangu, Kwanza nakushukuru kwa kukiri kuwa umebugi (umekosea) Sasa unatakiwa kurekebisha makosa kwa kufanya ifuatavyo. Kuoa siyo jambo la kukurupuka, subiri kwanza ajifungue wakati mkiendelea kumuuguza mama yenu mzazi, pili tumia muda mrefu kumchunguza unayetaka kumuoa maana kwa mujibu wa maelezo yako (kama haumsingizii) inaonyesha hajali shida zako.

Wanawake wa Vyuoni (hasa vyuo vikuu) wanapitia mengi na wanajua mengi, sasa huyo wako amegundua una udhaifu hivyo anatumia udhaifu huo kukuendesha anavyotaka yeye. Simama kama Mwanaume unatakiwa kuwa mpangaji na muamuzi wa mwisho yeye abakie kuwa mshauri na asikupangie (au unaogopa digree yake!!:D:D).

Kwa maoni ya mmoja wa wadau ni kuwa Mwanamke mwenye mtoto (Single mother) aliyepata mtu wa kumlelea mwanae na kumuahidi ndoa si rahisi kumuacha na ukijaribu unaweza kulishwa hata vyura na mijusi na sisi wote ukatuona mmbwa. Hivyo hata ukitaka kumuacha ujipange usikurupuke anaweza kuuuwa au kukufanya kichaa.

Na ninavyohisi ameshawaambia ndugu zake kuhusu udhaifu wako hivyo nao wanakupelekesha tu. Kuhusu fedha hiyo milioni 5 usimpe maana atatumia itaisha kisha atakuja tena kwa ukali (maana ameshakuona poyoyo). KWA UJUMLA UNATAKIWA KUSIMAMA KIUME TENA KWA KUMAANISHA SIYO KUIGIZA.
Ushauri mzuri sana huu.
 
Naungana na mdau mmoja hapo juu alipotoa ushauri wa kukutaka kusimama kama mwanaume,kimaamuzi na kimwenendo.Pia jitahidi sana kuwa msiri na mipango na mambo yako,usimwamini sana mwanamke na kumpa siri za mambo yako hasa kifedha.Naamini huyo mrembo anajua detail zako nyingi za kifedha( kwa wewe kujianika kwake) ndio maana anatumia nafasi ya kukuendesha awezavyo.Pia jitathmini kwenye maamuzi yako,kama baba na kama mwanaume aliye kiongozi wa familia.
 
Suala la kuoa,nakushauri liahirishe kwanza,ili upate muda wa kuutathmini huo uhusiano wenu na kuiona kesho yenu itakuwa vp,pia upate muda wa kumuuguza mama mzazi.Huo muda wa kujitathmini ningeshauri kila mmoja angeishi kivyake ili umsome vyema huyo mtarajiwa wako,msiihi pamoja,aende hata kwao kwa muda kidogo.Hapo ndio utajipa nafasi ya kumjua vyema.Kumbuka " Usiongozwe na hisia(mapenzi),ongozwa na akili zaidi katika maamuzi!!!
 
Wanawake wa Makabila ya mkoa wa Mara ni pasua kichwa Sana kwenye ndoa. Hawajali kuvuruga ndoa kwa uzinzi au kubambikia mimba,kuzaa watoto wa baba tofauti,mdomo na ukorofi.

Chunguza kwa nini aliachika au aliachwa baada ya kuzalishwa
 
Eehe hicho ndo cha Muhimu...!! Hakuna Mahari utaenda uambiwe pesa ndogoo labda mashehee ambapo mwanamkw wako anataja.

Mwanamke amesoma ana Degreee amini utatajiwa Mil kwenda mbelee sema shida ni single maza so pesa inapungua sanaaa kwa asilimi 90... na hapo Baba wa mtoto akiwa amefariki kama yupo Hai bhasi hata laki 2 unabebaa matatizo yako ukafie nayo mbelee..

Aisee
 
Kwanza hapo ulipo nakuona tuu hauko sawa mkuu.

Umefiwa na mke tena mwenye ujauzito lakini hujapitisha hata miaka 2 umeenda kuangukia kwa mwanamke ambaye ni wazi kabisa yuko desperate na ndoa.

Nakushauri huyo mwanamke endelea kukaa naye umsome tabia vizuri.

Mchane wazi kwamba wewe hauna uwezo wa kumlea huyo mwanaye mwingine hivyo asikupe mzigo.

Mchane wazi kwamba kwa sasa haupo kwenye position ya kufanya process zozote za kuoa asubiri mpaka mama ako atakapopona.

Mchane wazi kwamba yeye kuwa na mimba yako kisiwe kigezo cha kukupelekesha. Mwambie wewe ndiye mwamuzi wa mwisho hivyo atulize boli.

Yani uanaume wako sio unafanya mipango kwa kupelekeshwa pelekeshwa na kukurupuka.

Unforgetable
 
Subiri ya mama yapite..hayo ya mimba baadaye..ila pole sana
 
Nazidi pata mwangaza ila mimi nilitaka kumnawa siku hio hio ambayo yeye ndio anaona inafaa kama alivypanga ndio nitoe hio statement na nimpe pesa akafie mbele imagine iko hivi,.
Baba mkubwa anasema yeye awekewe laki tatu kwa bahasha yake, Mama laki tatu na vikorokoro kibao, kaka nae anatak laki 2 , Mzee anatamka kua lazima apate ngombe wawili wa kisasa wa maziwa na mengine mengi, ninaona bora nikae single sio kwa uoaji huu aisee
Huyo aliemzalisha mbona hajatoa mahari,unaoa familia inapepo la umaskini...utailea hiyo familia mpka uote mvi
 
Unakosa Mil 2 ya shughuli ya Mahari lakini Unapata Mil 5 ya kumkabidhi binti muweke mkataba????? Serious mkuu???? Wewe kama ulikuwa na nia ya kumuoa bhasi ungeenda kwao wakaongee na ndugu hiyo hela itapungua sana Tu mahari sio kitu fixed mzee unaweza toa hata 1.5 au Moja kabisa.

Kingine mama yako anaumwa bhasi mwambie Mkeo msubiri kwanza apone alafu usikie atasemaje maana haya hujampa hilo wazo uone mwenzio atajibu nini ushamuhukumu...serious??? Hatuishi kwa hisia mkuu wewe ongea nae ataelewa tu tayari ana mimba unadhani anaenda wapi sasa???? May b useme hukumpenda alafu pia ni SINGLE MAZA TAYARI ANA MTOTO...!! So unaona mahari kubwa hivyoo haifaiiiKweli kwa single maza Mil Inatoshaa sanaaaaaa....
Mwanamke akiwa anakupenda na kujua hali yenu kiuchumi,anamalizana na familia yake kwa kuwaambia hali ni mbaya mahari yangu isizidi labda laki 5...wewe umeona wapi mahari kila mtu na kiwango chake...hiyo familia inaroho y kimasikini sana,wazazi wenye utu na busara wanaweza kumuoza binti yao kwa kumsikiliza yeye anataka nini
 
Jamaa afunguke Asema ana laki 5.. Iwe sababu tosha familia inaweza sema toa laki 6 bhasi
Mimi wakati nachumbia mke aliwaambia wazazi wake mahari yake isizidi laki 5,mana hesabu ilikua 2m...uwezo nlikua nao mkubwa tu ila mke ndio alisema na familia ikamsikiliza
 
Kuna mchizi wangu job! Alitia mimba dem wa kichaga mwaka jana, lkn alikua ashaona hawawezi kukaa pamoja kwa sababu demu mzito sana kwenye mipango ya maisha. Yaani ni yule dem akija getto hawezi kugusa chombo aoshe au apike, yy akija anataka waagize chips kuku wacheki movie, na kumpa mtonyo wa kusuka, dem alikua kamaliza chuo mwaka huo huo. Maza ake alivyogundua dem anamimba, na aliyempa mimba ana ka kazi ka maana, akaanza kumsumbua mchizi aende kujitambulisha. Akapiga chenga sana hadi akaenda. Kufika wakapanga na mahari kabisa mil 2.

Dogo alipojifungua tarehe za mahari zikawa zishafika, jamaa akawa anatia kalenda, ooh hali mbaya, nivumilieni bado najipanga, hahaha: ilifikia hatua maza ake na dem kamtia dem kwenye gari kampigia simu jamaa kumtaarifu mkeo na mwanao Wanakuja huko mlee pamoja kama ni kujipanga mtajipanga mkiwa wote. Mkitaka kuleta mahari ni nyie.

Ko kiufupi hii mambo ya kujipanga inategemea na mtazamo wa wazazi wa dem. Vinginevyo mzigo utakomaaa nao hadi uchoke.
Huyu ndio mwanaume,sio huyu anapelekwa kama gari bovu na single maza
 
Ay
Yuko kwenye usimamizi mzuri kiongozi tumekaa hospital zote bongo na kujirizisha kwa kile anachosumbuliwa nacho, ila imagine mtu aliekuleta dunian anasikia kua dogo umetoa posa /mahari ilhali yeye yuko hoi huu ni umaku, nimetiwa kidole matakon na kuambiwa ninuse nimekubali na kwa kua nishajua kua kuna nuka acha nichambe mavi haya maisha yaende, huruma zangu za kisukuma zitaniponza nisipokaza pu mb
Umepata demu mweupee jamaa languuu
 
2 million mahari kwa single mother ?, ilitakiwa wewe ndo ulipwe kwa kumpa Nusra huyo bidada ,kimbia haraka sana.
 
Una pesa za kuchezea, MTU ana mtoto wa miaka 9 unajua baba mtoto alipo!! Kila siku mnaambiwa kuoa single mother ni kama kujitega mwenyewe kwa Bomu ila hampati somo....

Ukiona hafai jitenge naye
 
Usimuamini mwanamke kuwa mkoloni kwa mwanamke ww ni mwanaume fanya mamuzi magumu...
 
Back
Top Bottom