Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Usokwe

JF-Expert Member
Mar 4, 2019
523
1,000
Ndugu wasomaji,

Nimeamua sasa kuachana CRDB bank kutokana na makato yasiokuwa na Tija yoyote. Najiuliza, hivi ndio kusema kuweka fedha bank ni utajiti?

Makato yao yanaumiza sana na hayana uhalali wa aina yoyote, haisadi sekta ya bank kukua, mitaji kukua, kukopesha nk.

Nadhani ni wakati wa BoT kuangalia hizi sera za mabank pamoja na huduma zao.

Kwahivyo naona ni bora kutafuta mbadala. Nachoomba ushauri ni bank gani ambayo inatoa online services, mastercard, visa, account activities etc.

Maana kwakweli CRDB wamenishinda. Kupata card, online access ilikuwa ngumu kama kitu gani. Toka Kimei ameondoka naona imekuwa bank ya hovyo sana.
 

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
10,107
2,000
Nachoomba ushauri ni bank gani ambayo inatoa online services, mastercard, visa, account activities etc.
Maana kwakweli CRDB wamenishinda. Kupata card, online access ilikuwa ngumu kama kitu gani.
Umezungumzia mambo mawili.
  • Makato
  • Uharaka wa kuhudumiwa /Online Service

Nakushauri fungua account yako na benki ya FNB, kama benki mbadala
  • Account type chagua ile yenye makato fixed kwa mwezi, ni kiasi kidogo, then chochote utakachofanya kwenye account yako hakuna makato.
  • Online Banking wako vizuri, waweza login kwenye account yako kwa simu au PC na kufanya miamala wakati wowote..
 

aker2011

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
756
1,000
Juzi nilitoa kiasi flan salio likabaki vzuri tuu, Jana nmeenda kutoa tena nakuta kiasi Cha elf 20 hakipo, Sasa najiuliza iyo elf 20 imepotelea wap? Ni moja kati ya bank ya ajabu Sana na wanakata pesa bila sababu yoyote nasubiri apa wakanipe maelezo vizuri kabla sijaama iyo bank
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,723
2,000
Bank yenye tabia za kipekee ni Equity tu kwa sasa! Hawana ujinga wa kuchezea hela zako ukiweka mle ni kama kibubu😅

Drawback:
Ikitokea Emergency kuipata hela yako utachora chini maana kwa Dar ATM yao iko Mikocheni tu😅! Usipompata wakala unaweza lia na mawakala wake sio wengi.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,723
2,000
Umezungumzia mambo mawili.
  • Makato
  • Uharaka wa kuhudumiwa /Online Service

Nakushauri fungua account yako na benki ya FNB, kama benki mbadala
  • Account type chagua ile yenye makato fixed kwa mwezi, ni kiasi kidogo, then chochote utakachofanya kwenye account yako hakuna makato.
  • Online Banking wako vizuri.
FNB sijawajaribu ila Ecobank ndio wahuni wakubwa 😅 usijaribu yani maana ATM yao huwa mbovu siku zote kupata kadi tu ni mbinde, makato ndio biashara yao kama serikali ya maza😅
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom