Kama huna utulivu wa moyo hata unyanyue nyumba mbili huku na huku mwili hutauona,unanyanyua vyuma huku ukiwaza ile 10K yako uliyoipata itakutosha kula ugali samaki na juice na nauli kesho?
Hapo mwili utaupata vipi,tafuta kwanza hela ili ukitoka gym ukiamua kula mbuzi unakula ukiamua kula samaki unakula yaani unapata kitu roho inapenda sometimes unaweza jisikia kutokula ila unajisikia uko vizuri.
hakikisha huna stress..kula mimboga ya majani..misupu..mfani kongoro ..samaki..maji kunywa sana...cabs kwa wingi..protini ndo izidi sana..lazima ukipga vyuma ujae..n.b..ukienda gym vaa sweta ata kama joto ni kali
Kama unataka kujazia sana kuna vyakula maalum vya makopo,ni unga hivi,japo sikushauri ksbb nahisi vina machemical kibao,ila ndio unaboost. Huo unga unapatikana kwenye masuper market ya vyakula nafikiri. Mimi nimejazia japo sio sana,ksbb sipendi kuwa much. Lakini vyakula ninavyotumia ni vya kawaida tu. Asubuhi supu ya samaki na mihogo,siku nisipofanya mazoezi asubuhi nakula matunda mchanganyiko,papai,tikit,parachichi hivyo lazima viwepo. Mchana wali au ugali+samaki+mboga za majani zimeungwa karanga. Usiku lazima matunda mengi sinia zima nafuta taratibu. Lakini mazoezi yangu sitaki kuongezea kitu cha ziada kuboost. Nataka niwe asili tu. Ningekushauri pia fanya mazoezi tu ndio yakupe matokea,ukijituma sana kila siku utatanuka tu,huku ukila vyakula vya kawaida. Usile saaaana,utakuwa na tumbo kubwa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.