Ninafanya biashara ya kuchoma nyama, ila nyama leo imeharibika ushauri tafadhali nifanye nini?

wakwatito

Member
Apr 15, 2018
30
49
Mie nahusika na ujasiriamali mdogo mdogo na genge la nyama choma kila siku nimekuwa nachukua nyama jioni na kwenda nayo nyumbani na kuweka katika chombo kikubwa cha wazi nimekuwa nafanya hivi mara kwa mara.

Ila leo nimekuta nyama inatoa wadudu nimemweleza anayenipaga nyama now kaniruka hataki hata kuona hasara nayo pata naombeni ushauri nichukue maamuzi yaapi maana hata pesa ya kufanyia leo kazi sina jana yote nimempa.

Ahsante
 
Ndo changamoto za biashara huna jinsi lazima uzikabili tu...sasa anza kufikiria kununua kifriji kidogo cha kuhifadhia.
 
Mie nahusika na ujasiriamali mdogo mdogo na genge la nyama choma kila siku nimekuwa nachukua nyama jioni na kwenda nayo nyumbani na kuweka katika chombo kikubwa cha wazi nimekuwa nafanya hivi mara kwa mara....
Mwambie akukopeshe nyama nyingine nzuri alafu utamrejeshea kidogokidogo maana kila kazi ina hasara zake.

Hapo huna la kufanya maana nyama ulichukua mwenyewe na uliridhia wakati ukichukua
 
Mwambie akukopeshe nyama nyingine nzuri alafu utamrejeshea kidogokidogo maana kila kazi ina hasara zake.

Hapo huna la kufanya maana nyama ulichukua mwenyewe na uliridhia wakati ukichukua
Fuata huu ushauri utakusaidia kama muuzaji atakubali kukukopesha.
 
Kama huna friji si uwe unanunua siku hiyo hiyo kuliko kuiacha wazi mpaka kesho yake.
 
Mwambie akukopeshe nyama nyingine nzuri alafu utamrejeshea kidogokidogo maana kila kazi ina hasara zake.

Hapo huna la kufanya maana nyama ulichukua mwenyewe na uliridhia wakati ukichukua

Fuata huu ushauri utakusaidia kama muuzaji atakubali kukukopesha.

Hawezi kukubali kumkopesha, kwa kuwa naamini wakati huyu jamaa anamwambia nyama imeharibika ni lazima kutakuwa na kauli ambazo pengine zitakuwa si za kiungwana zitakuwa zilitumika na mmoja wao!

Hili la kukopeshwa lingewezekana tu endapo huyu aliyenunua nyama angeamua kuvunga bila kumwambia nyama imeharibika!

Angemuambia tu kuwa amuongezee nyama kisha akimaliza kuuza atamlipa! Kwa sasa huyo muuza nyama atahisi kuwa endapo atamkopesha basi hatolipwa kwani huyu mnunuaji anaweza akamgeuka na kumwambia kuwa anafidia!
 
Hii sio code kweli?

Nyama hauwezi kuiweka kwenye fridge na ikatoa wadudu, joto haliruhusu kabisa.

Kijana umetumia code ngumu mnoo
 
Nunua vinegar ioshe kwa vinegar.

Mimina ndimu kwa wingi kwenye nyama na uwe kama unaisuuza kwa ndimu.

Osha kwa vinega tena.

Kisha endelea na maandalizi yake ya siku zote.

NB. Hii niliona kwenye nyama ya mbuzi sijui wewe unadeal na nyama gani. Pia nunua friji.
 
Hiyo ni ya kutupa hakuna namna. Hasara kwenye biashara ni kawaida, ndio inayokupa akili ya ujiongeza. Nunua friji na ongeza maarifa namna ya kuhifadhi chakula kisiharibike haraka.

Usithubutu kulisha wateja nyama iliyooza. Hasara zitakuandama mpaka ujute, maana utajijengea sifa mbaya hutoendelea. Usiwalishe watu kitu ambacho ingekuwa ni wewe mwenyewe usingefurahia.
 
Back
Top Bottom