Ninaekereka au Kuchoshwa na hili linaloendelea sasa katika Redio nyingi za Tanzania nipo peke yangu au?

Safi! Japo siyo redio tu bali hata tv mambo ni hayo hayo...

Jamaa wana makelele mengi balaa tena saa zingine wanafanya kama wanashindana sijui tuite kujibizana yaani huyu anaongea yule nae anakuja juu anaongea kwa kupaza sauti ya juu ili amfunike (amnyamazishe) mwenzake
 
Hawa unawaonea Mkuu ' Uozo ' mkubwa uko Clouds FM, EFM, Magic FM na Wasafi FM.

Kidogo Radio One na RFA kuna Nidhamu na Kujielewa fulani ila siyo kwa hawa niliowataja.
Bila kuisahau Efm mkuu hizi redio unakuta kila kipindi wameweka na mchekeshaji mmoja au wawili kazi yake hapo ni kutema pumba tu.
Kwa mfano Efm kuna Manganje na Mpoki
 
Au unakuta kunakitu Cha muhimu na Cha msingi mtangazaji anakizungumza alafu mtangazaji kiongozi anamwambia mda imeisha au tunadakika chache dakika zenyewe Sasa kumbe ni kupiga mziki lisaa lizima
 
Tatizo kubwa la watangazaji wa sasa hatwajiandai wala kufanyia tafiti wanachokirusha hewani tofauti na watayarishaji vipindi na watangazaji wakongwe

Sikiliza kwa mfano vipindi vinavyotayarishwa na Masoud Masoud utaona jinsi anavyoiheshimu kazi yake na kuwaheshimu wasikilizaja wake. Masoud anatafiti content zake na kuziweka katika mpangilio wa kuelimisha na pia kuvutia

Watangazaji wa sasa anaweza akaongea hewani kitu asichokijua au hana uhakika nacho au ni cha uongo na akataka wote muamini anavyojua yeye!

Ni vyema kila Radio ikawa na timu ya wadhibiti ubora kuanzi kwenye lugha, uwasilishaji wa content mpaka nidhamu za presentation ili vipindi viwe both entertaing and educating
 
Hata magazeti pia hakuna habari za kiuchunguzi ni kuripoti tu matukio.

Habari itasema Waziri Mkuu kafungua mkutano, tena hiyo ni headline.
Hapo miaka michache iliyopita yalikuwepo magazeti yenye habari za kiuchunguzi,nadhani yalitengenezewa mazingira ya kupotea na ' secret hash '.
 
Back
Top Bottom