Ninaekereka au Kuchoshwa na hili linaloendelea sasa katika Redio nyingi za Tanzania nipo peke yangu au?

Unakuta Kipindi fulani ni cha ama dakika 30 au Saa Moja tu lakini Watangazaji wake wote Watano wanataka Kuonesha Umahiri wao katika Kupiga Stori na hapo hapo tena Matangazo ya Biashara yanafululiza na Content husika iliyokufanya usikilize hicho Kipindi unakuja kuipata ndani ya dakika 5 tu.

Halafu namtafuta sana huyu Mtu aliyebuni kuwa kwa Siku hizi ili Redio yako ipendwe na Vipindi pia vivutie Wasikilizaji basi ni lazima kiwe na Watangazaji kuanzia Watano mpaka hata Saba tena wote wakiwa Hewani Wanabwabwaja tu Pumba zao.

Enyi Wamiliki na Watangazaji wa Redio na Vipindi mbalimbali vya nchini Tanzania Sisi Wasikilizaji wenu tunataka kusikia ' Content ' husika tu na siyo huu ' Upuuzi ' wenu wa kutupigia ' Mikelele ' ya Stori zenu zisizo na Miguu wala Kichwa kwani si tu mnaharibu bali mnatukera mno.

Kuhusu Upigaji wa Matangazo (ambayo najua ndiyo yanawalipeni sana) tafuteni utaratibu wa kuyapiga lakini siyo Kuyafululiza mpaka yanakula muda mrefu wa Kipindi na hatimaye 'Content' husika inakuja kusikika kwa dakika 5 pekee.

Halafu acheni Umbwiga (Ushamba) wenu yaani unakuta Tangazo la Biashara linapochezwa Hewani linajieleza vyema tu mwanzo mwisho kwa Sisi Wasikilizaji na likiisha tu utasikia Watangazaji wote waliojazana Studioni nao wanaanza tena Kulizungumzia. Hivi mliambiwa akina GENTAMYCINE ni Viziwi na hawakulisikia au Kulielewa?

Nina uhakika kuwa kwa Kero hii Kubwa kukifanyika Audience Research ya kuhusu Media za Tanzania na Contents zake ' Findings ' zitaonyesha kuwa Wasikilizaji wengi wamepungua na sasa tumekimbilia huku katika Mitandao ya Kijamii (JamiiForums) ambako binafsi kama GENTAMYCINE naona ' Kumenoga ' kuliko huko kwenye ' Upuuzi ' wenu.

Unaacha Kutangaza ' Content ' ya Kipindi unaanza Kutuambia Mambo yako ya Nyumbani na Mkeo pamoja na Wanao huku ' Ukijisifu ' tu Kipopoma (Kipumbavu) utadhani tumekuuliza.

Na wengine mlivyo Waongo mkiwa ' Vipindini ' huwa ' mnajimwambafai ' kweli kweli kuwa mna Maisha Bora wakati baadhi yenu ( kama si wengi wenu) tunawajua jinsi mlivyo Mafukara kama nilivyo Rais wa Mafukara JamiiForums GENTAMYCINE Mimi.

Ujumbe huu uzifikie 'Redio' zote nchini.
Ni kweli kabisa sasa hivi kuna hivi vipindi vya michezo sasa unakuta hao wachambuzi wako kibao na matangazo ndio usiseme.Naunga mkono hoja.
 
Ni kweli kabisa pia hao watu hawajasomea uandishi wa habari ni WAHUNI TU, serikali inatazama tu na kulaumu kwamba hakuna maadili
 
Kwanza redio nyingi hazifuati muda, kipindi cha kuanza saa 3kamili huanza na dk 10 kabisa......nadhani ni TBC pekee wanaofuata ratiba za vipindi..........
 
Siku hizi redio chenga watangazaji wanapiga stori zisizokuwa na maana ndio maana mm nasikilizaga matangazo ya dura ya dunia tu.
 
Acha kelele wewe mwenyewe kwa jinsi unavyojitukuza kila senstensi lazima ujitaje jina lako.
 
Acha kelele wewe mwenyewe kwa jinsi unavyojitukuza kila senstensi lazima ujitaje jina lako.
Kwani GENTAMYCINE nikijitaja kila mara Wewe inakupunguzia au inakuongezea nini? Pumbavu.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE ( alias ) Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer sawa? Mnanichukia lakini 24/7 kila muingiapo tu hapa JamiiForums lazima mtakodoa nimeandika nini au nimeanzisha Uzi gani.

Na GENTAMYCINE nitaendelea Kujipaisha sana tu hadi mkome na mkiona mnachukizwa kuliko na hii ID yangu 'Brand' kabisa tafuteni haraka Sumu ya Panya na Dawa ya Kuulia Kunguni korogeni katika Kikombe kisha mnywe Mfe kabisa sawa?

Cc: adriz
 
Mimi mara chache nawasikiliza, bora siku hizi kuna options kibao mitandaoni. Watu wanapiga stori kama wapo kijiweni then matangazo alafu wakianza kuongea tena wanaanza na matangazo

Pengine waandaaji wa vipindi ndio tatizo au waandaaji wanakosa vipaji vinavyojitosheleza. Hadi vipindi vya burudani unakuta team ya watu watano na madj si chini ya 2! Zamani mtu mmoja au wawili tu walikuwa wanaweza kukimbiza. Hii inampa mtu jukumu kubwa la ubunifu tofauti na sasa na huo mlundikano.
Enzi za kina Misanya Bingi rip radio one, Fredwaa rip rfa. Na DJs wao ndani ya nyumba. Matangazo yapo but very controlled na contents za vipindi. Full enjoyment ya kusikiliza radio

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Vipindi vingi siku hizi ni vijiwe tu, redio station zinaajiri watu wasio na taaluma ya uandishi wa habari na utangazaji

Kuwe na bodi inayosimamia taaluma ya utangazaji na uandishi wa habari kama vile NBAA
 
Back
Top Bottom