GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,544
- 108,869
Unakuta Kipindi fulani ni cha ama dakika 30 au Saa Moja tu lakini Watangazaji wake wote Watano wanataka Kuonesha Umahiri wao katika Kupiga Stori na hapo hapo tena Matangazo ya Biashara yanafululiza na Content husika iliyokufanya usikilize hicho Kipindi unakuja kuipata ndani ya dakika 5 tu.
Halafu namtafuta sana huyu Mtu aliyebuni kuwa kwa Siku hizi ili Redio yako ipendwe na Vipindi pia vivutie Wasikilizaji basi ni lazima kiwe na Watangazaji kuanzia Watano mpaka hata Saba tena wote wakiwa Hewani Wanabwabwaja tu Pumba zao.
Enyi Wamiliki na Watangazaji wa Redio na Vipindi mbalimbali vya nchini Tanzania Sisi Wasikilizaji wenu tunataka kusikia ' Content ' husika tu na siyo huu ' Upuuzi ' wenu wa kutupigia ' Mikelele ' ya Stori zenu zisizo na Miguu wala Kichwa kwani si tu mnaharibu bali mnatukera mno.
Kuhusu Upigaji wa Matangazo (ambayo najua ndiyo yanawalipeni sana) tafuteni utaratibu wa kuyapiga lakini siyo Kuyafululiza mpaka yanakula muda mrefu wa Kipindi na hatimaye 'Content' husika inakuja kusikika kwa dakika 5 pekee.
Halafu acheni Umbwiga (Ushamba) wenu yaani unakuta Tangazo la Biashara linapochezwa Hewani linajieleza vyema tu mwanzo mwisho kwa Sisi Wasikilizaji na likiisha tu utasikia Watangazaji wote waliojazana Studioni nao wanaanza tena Kulizungumzia. Hivi mliambiwa akina GENTAMYCINE ni Viziwi na hawakulisikia au Kulielewa?
Nina uhakika kuwa kwa Kero hii Kubwa kukifanyika Audience Research ya kuhusu Media za Tanzania na Contents zake ' Findings ' zitaonyesha kuwa Wasikilizaji wengi wamepungua na sasa tumekimbilia huku katika Mitandao ya Kijamii (JamiiForums) ambako binafsi kama GENTAMYCINE naona ' Kumenoga ' kuliko huko kwenye ' Upuuzi ' wenu.
Unaacha Kutangaza ' Content ' ya Kipindi unaanza Kutuambia Mambo yako ya Nyumbani na Mkeo pamoja na Wanao huku ' Ukijisifu ' tu Kipopoma (Kipumbavu) utadhani tumekuuliza.
Na wengine mlivyo Waongo mkiwa ' Vipindini ' huwa ' mnajimwambafai ' kweli kweli kuwa mna Maisha Bora wakati baadhi yenu ( kama si wengi wenu) tunawajua jinsi mlivyo Mafukara kama nilivyo Rais wa Mafukara JamiiForums GENTAMYCINE Mimi.
Ujumbe huu uzifikie 'Redio' zote nchini.