Ninadaiwa Tala, Branch na M-pawa. Nisipowalipa watanifanya nini?

Kilichonichosha kulipa ni riba kubwa yaani nilikopa 10,000 me niliyotumia ni 9000 tu baada ya makato ya pesa ya kutolea ila wao niwalipe 13,080

Wapi na wapi hawapati kitu, silipi deni lao yaani wapate faida ya 4080 kweli??
 
Hili ni janga lingine chini ya jua, yaani mtu kukopa unaomba tena kwa kubembeleza halafu kulipa hutaki tena maksudi kabisa.
Si ajabu mtu huyu anamuomba Mungu abariki maisha yake wakati yeye anabomoa ya wengine.

Ndugu ni vyema ukalipa tu deni lako ni ishara ya uungwana na ustaarabu katika jamii. Vinginevyo unajitafutia laana tu kwenye maisha yako.
 
Kama nilivyoelekeza hapo juu, nimekuwa mfanyabiashara mdogo muda mwaka sasa tangia nijiunge na mikopo ya tala na kufikia mkopo wa laki 3 na nusu nikachukua biashara nikapeleka Morogoro.

Nikakuta soko sio zuri hivyo mtaji ukayumba.

Nlivyowaelekeza TALA wakasema hawanielewi tulishakubaliana hiyo pesa irudi kwa muda wa mwezi. Mpaka sasa nimezidisha siku 15 wameongeza riba asilimia 10.

Najuta mpaka sasa nimeomba wanifahamishe ofisi zao zilipo labda niende nikakutane na mkuu wao nimueleze yaliyonikuta wanasema niwasiliane kupitia facebook au sms za kawaida.

Hivyo naomba kama kuna yeyote anajua ofisi zao zilipo anielekeze niwafuate.
 
Mi wananidai na nina mpango wa kuwalipa ila nimekuwa nimelazwa hospital wiki mbili na wanaendelea kunitisha na hawaelewi ,sijui nife ili wafurahi na tuone watalipwaje! Hata pole hakuna wakati mm ni mteja wao wa muda mrefu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza pole na homa ndugu. Mimi Mpaka hapa nlipo katika laki tatu na nusu nmepunguza elfu 50 lkn riba imeongezwa na kua deni lile lile aisee.. hivi hawana ofisi hawa watu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom