Ninadaiwa benki nne, BOA, CRDB, AKIBA, STANBIC BANK, naombeni msaada wenu

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wana JF...

Ndugu yenu nipo kwenye wakati mgumu hakuna kipindi kigumu kwenye maisha yangu kama iki...

Hizo benki zote zinanidai jumla ya milioni 80

Kila benki nilikopa milioni 20 nimetapeliwa zaidi ya milioni 50 na wazaire...

Milioni 10 niliingiza kwenye biashara ya dagaa nayo ikakata..

Milioni 20 nilinunua Costa kwa muhindi nayo imekufa gear box ipo garage..

Mke wangu nae kakimbia naombeni msaada wana JF wenzangu..

Nifanyaje niokoeni jamani
 
pole sana...hata sijui nikushauri nini kiasi unachodaiwa ni kikubwa mno...
 
Kama nyumba yako haina ceiling board, si umalizane tu na shingo **** mkuu. Chukua ujasiri wa mkwawa uondokane na hayo madhila ya dunia
 
Ulipokopa uliweka dhamana ya vitu gani? Kama zipo hizo dhamana uza ujiokoe na madeni japo hakuna mwanadamu asiyedaiwa kama hayakusumbui kulipa yavumilie tu yataisha
 
Mbona haupo makini. Umesema unadaiwa na benki nne @mil 20. Hiyo hesabu ya mil 80,000/= umeipataje?

Naomba unieleweshe kabla ya kukupa ushauri.
 
Pagumu kama ulinunua ardhi ipige bei,ungejua ungenunua mapori uyafyeke baada ya mwaka thaman inaongezeka.gari kitu gani tena kwa muhindi bora mwarabu.ni sawa na mchaga akuachie sehemu alpokuwa anafanya biashara yeye arudi nyumban kupunzika elewa hapa akuna biashara ndo maana anakupa wewe.
 
Hawezi kuuza chochote kilichowekwa dhamana, especially immovable collaterals ambazo zinakuwa chini ya mabenki baada ya perfection.
Angalia makosa ya kisheria yaliyopo kwenye offer letter pamoja na terms and conditions ulizokubali.
 
Mbona haupo makini. Umesema unadaiwa na benki nne @mil 20. Hiyo hesabu ya mil 80,000/= umeipataje?

Naomba unieleweshe kabla ya kukupa ushauri.

Hesabu wito, kunawatu hawawezi soma 2 hadi uandike mbili.
Hata hivyo yuko kwenye taharuki
 
Mbona haupo makini. Umesema unadaiwa na benki nne @mil 20. Hiyo hesabu ya mil 80,000/= umeipataje?

Naomba unieleweshe kabla ya kukupa ushauri.

Ndungu yangu nadhani ujanisoma vizuri, nimesema nadaiwa na benki nne, kila benk moja nilikopeshwa milioni 20 jumla nadaiwa milioni 80 umenipata kaka
 
Kwa kweli matatizo yana tabia ya kuja yanafatana! mwezi ujao tena kodi ya nyumba..
Mwezi wa kwanza tena watoto shule ehee mwaka huu takuwa mgeni wa nani!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom