Ninachokiona ni vita Baridi baina ya Masikini na Matajiri hapa Tanzania

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
NINACHOKIONA NI VITA BARIDI BAINA YA MASIKINI NA MATAJIRI HAPA TANZANIA

Na, Robert Heriel

Nimejikuta sipendi kuzungumzia siasa za nchi hii. Hii ni baada ya kugundua kuwa siasa za nchi hii ni Vita Baridi Kali inayohusisha makundi makuu mawili; nayo ni masikini na Matajiri.

Kwa kweli Mwanzoni nilipoanza kujihusisha na Siasa za maandishi mitandaoni sikuwa na muono Kama nilionao hivi sasa. Mwanzoni nilikuwa nadhani Siasa ni Uwanja wa watu kupigania maslahi ya nchi bila kujali ni Masikini au ni matajiri. Nilifikiri Siasa ni mchezo WA kijamii, wakitamaduni ambao watu hushiriki kuongoza watu katika maendeleo ya taifa. Lakini kumbe sikuwa Sawa, nasisitiza; Sikuwa Sahihi kudhania hivyo.

Nimegundua kuwa kujiingiza kwenye Siasa ni kukubali kuingia katika vita baridi itakayoweza kuharibu mapafu na kuyajaza maji.

Siasa ni urafiki wa kimaslahi, kuyapigania na kuyatetea Kwa gharama yoyote Ile.

Mimi sio mwanachama wa chama chochote, kusema hivi wanasiasa na Wafuasi wao hawapendi kusikia kauli hii. Sijajua ni Kwa nini lakini kama nikijaribu kuyaona mawazo yao, hunifikiria Mimi ni kama "Kinyuki Maua" wengine huniona Kama Mnafiki niliyebobea.

Hata hivyo siwalaumu Kwa mtazamo huo wanaonifikiria, nafahamu kwenye vita sharti uwe na upande. Lakini wasichojua ni kuwa wengine hatuipendi vita hiyo.

Siasa za nchi hii huenda ni zile za Kupe na Kondoo. Au pengine ni zile Siasa za Paka na Panya ndani ya nyumba.

Hakuna atakayeongoza Kwa raha kwenye Siasa za TANZANIA vita baridi hii ikiendelea. Hata hivyo Jambo la kutisha ni kuwa Mwanasiasa yeyote anapaswa kuchagua upande aidha upande wa matajiri au upande wa masikini.

Kama Rais akiwapenda Wanyonge basi wanyonge watampenda.
Halikadhalika Kama Rais akiwa upande wa MATAJIRI basi matajiri watampenda.

Vyovyote iwavyo, hujuma lazima ziwepo katika siasa.

Hakuna Rais atakayekumbukwa Kama yule atakayeweza kuwaleta pamoja matajiri na Masikini. Jambo ambalo haliwezekani na Kama litawezekana basi hicho ndicho kitafanya Rais huyo akumbukwe.

Rais wa Masikini hukumbukwa na Masikini na wanyonge aliowapambania.
Rais wa matajiri hukumbukwa na Matajiri aliowapigania.


Jambo moja nililolikariri na ambalo nafikiri litadumu Kwa Karne nyingi Kwa Rais wa upande wa masikini ni hili;

Ili masikini afurahi na ampende Rais husika basi anapaswa afanye Jambo moja kuu la lazima nalo ni kuwanyanyasa, kuwakandamiza, kuwakamuua Matajiri. Masikini hupenda Sana akisikia tajiri kahenyeshwa mavi, kakamuliwa au kafilisiwa.

Masikini hata usipomletea maendeleo Ila ukamfilisi Tajiri na kumzonga zonga basi atafurahi Sana. Ataona wewe ndiye Rais wao.

Masikini hupenda kifo cha wengi ambacho kwao hukiita Harusi au sherehe ya makabwela.

Ni bahati mbaya ilioje nchi yetu kuwa na masikini wengi wenye kuzidi mzani. Hivyo yeyote unayefikiria kuongoza nchi hii Kama unampango wa kupendwa na wengi ambao ni masikini basi usijisumbue kuwa namna ya kuleta maendeleo. Bali sugua kichwa namna gani utawasumbua matajiri wasiishi Kwa Raha kwani hayo ndio mapenzi kwa watu Masikini.

Masikini huenda ikawa istilahi jumuishi Sana kiasi kwamba wengi wakabaki hewani wasielewe.
Masikini Kwa mujibu WA andiko hilo nimemuweka katika daraja hizi;
1. Masikini wa kipato
2. Masikini wa makazi
3. Masikini wa chakula na mavazi
4. Masikini wa Fikra, elimu na Ujuzi,

Tajiri katika andiko hili nimemchora Kama ifuatavyo;
1. Tajiri WA kipato
2. Tajiri wa makazi na makazi
3. Tajiri WA chakula na mavazi
4. Tajiri WA Fikra, elimu na Ujuzi.

Kwa taifa letu vita baridi ipo baina ya makundi hayo hapo juu. Ukitaka kuingia kwenye Siasa basi jua kabisa unaingia katika Uwanja wenye timu hizo mbili zilizohasimiana Kwa kiwango cha juu kabisa.

Ukisikia kelele zinapigwa cha Kwanza sharti ujue kelele hizo zinatokea Red Corner au Blue Corner?
Je zinatokea Kwa makabwela au matajiri?
Kisha fanya tathmini penye faida zaidi.

Ukiona Rais hapendwi na masikini na wajinga basi jua atakuwa anapendwa na Matajiri na werevu. Na ukiona Rais hapendwi na Matajiri na werevu basi jua anapendwa na masikini na wajinga.

Hizo ndizo Siasa na mambo yake Kwa ufupi Kwa nchi yangu ya TANZANIA. Wakati mwingine nitakuja kuelezea sifa za makundi hayo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Bagamoyo, Pwani.
 
Wakati Magufuli anawashughulikia matajiri masikini waliingana kuwatetea. Ajabu matajiri hawaungani kuwatetea masikini kipindi hiki cha Samia!!!

Wakati Masikini walifurahia mno.

Walioungana ni matajiri wa Fikra, Ujuzi na elimu kuwapigania matajiri wa vipato

Kelele sasa hivi zinatoka Kwa masikini OG.

Ingia mitaani, vijiweni na mitandaoni angalia masikini wanavyoishutumu serikali.
 
Tanzania ni kama wote tu ni maskini. Hakuna hivyo vita ya matajiri na maskini Tanzania. Nafikiri kwa nchi za chini ya jangwa la Sahara, Tanzania ndiyo kuna tofauti ndogo kati ya maskini na tajiri.

Vita kubwa nchi yetu ni kati ya mwananchi wa kawaida na Apparachtiks. Hasa hasa wale waliopachikwa serikalini. Hiyo ndiyo vita baridi kubwa nchini mwetu. Hao ndiyo wanafanya tutaabike na kuendelea kuwa maskini.
 
Mimi mwenyewe nikiona tajiri anafirisika nafurahi Sana ,tena hata Kama sijala njaa inaisha ...

Yaani wengine watembelee kwenye v8 sis tunapigwa na jua tunashindia mihogo ya Jero na pepsi bigii moja .....
 
Tajari akifilisika ni rahaa Sana ,kwan watoto wake tutakuwa tunashindia mihogo wote ,shule tunatembea kwa miguu wote ,kila kitu tunakuwa sawa Hadi rahaaa.

Magufuli aliona mbali sanaa
 
Na mama ameamua kuwa upande wa matajiri kaamua kuachana na masikini tunatakiwa kuwanyoosha wakati wa uchaguzi
 
Tanzania ni kama wote tu ni maskini. Hakuna hivyo vita ya matajiri na maskini Tanzania. Nafikiri kwa nchi za chini ya jangwa la Sahara, Tanzania ndiyo kuna tofauti ndogo kati ya maskini na tajiri.

Vita kubwa nchi yetu ni kati ya mwananchi wa kawaida na Apparachtiks. Hasa hasa wale waliopachikwa serikalini. Hiyo ndiyo vita baridi kubwa nchini mwetu. Hao ndiyo wanafanya tutaabike na kuendelea kuwa maskini.


Karibu Sana
 
Back
Top Bottom