Nina Woga(fear),stress(msongo)nifan yeje kupata tiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina Woga(fear),stress(msongo)nifan yeje kupata tiba

Discussion in 'JF Doctor' started by rakeyescarl, Sep 17, 2012.

 1. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 400
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wakuu nawasalimia na naomba msaada.
  Umri miaka 50.Nina watoto 5 na mke,naishi DSM.Niliachishwa kazi mwaka 1 uliopita na nikawa nabangaiza mpaka siku kama 14 zilizopita nilipopata kazi upya ya kipato cha wastani,ndio likanitokea tatizo hili.
  Naogopa kutoka ndani ya nyumba najisikia -feelings kama kuna kitu kinanifanya nisitake kutoka ndani ya nyumba.
  Ndg zangu wamenishauri nipime ukimwi,cancer na malaria(FBP) vyote vimekuwa negative.Najisikia kwa mbali kama tumbo linauma nimeangaliwa ulcers sina.
  Wengi wamenishauri kuwa hii ni stress,je nifanyeje kupaa tiba hata kama si stress,hata kama ni hospitali ya kulipia naweza kulipiwa,natanguliza shukurani. naomba mwenye msaada anisaidie niache kuteseka kwa kuni PM au rakeyescarl@yahoo.ie.
   
 2. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,320
  Likes Received: 2,944
  Trophy Points: 280
  kwa uwelewa wangu mdogo...muone daktar wa maswala hayo. Pia kutokana na imani yako mtangulze Mungu mbele..pia jtaid kufanya mazoez mara kwa mara na pia tembele ndugu na marafkr..pole sana. GOD Z GOOD!
   
 3. REX

  REX JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tres inatiba ya asili.kwa tafit zilizofanywa zinaonesha kuwa royal jelly ni dawa nzuri sana kwa tatizo hilo.siku hiz wameaza kuiweka hata grand malt wakiwa na lengo la kupunguza msongo wa mawazo jambo ambalo limekuwa tatizo kwa watu wengi.lakin grand malt ina kiwango kidogo sana cha royal jelly ukipata ya vidonge ni nzuri zaid.kwa msaada zaid ntafute 0715720276
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,022
  Trophy Points: 280
  Pole Sana mkuu kwa hayo matatizo yako ya Ugonjwa wa wasiwasi tumia Dawa yangu ya Mbadala itakusaidia hii inshallah uwe unakula hii Lozi kila siku kwa kipimo cha gao la mkono wako. Angalia faida yake hapo chini.


  Lozi (Almond):

  [​IMG]  Lozi inajulikana kama ni King katika jamii ya njugu, ina elements karibia ya zote zinazohitajika katika mwili wa mwanadam. Ni chakula chenye kutia nishati mwili na akili.
  Kuna aina mbili za Lozi, kuna lozi zile tamu na kuna lozi chungu kuna zenye ngozi nyembamba (thin-skinned) na kuna zenye ngozi nene(thick-skinned) hii ni katika aina ya lozi tamu ambazo ndio tunazozitumia na tunahitajika kutumia ama zile lozi chungu zina prussic acid ambayo ni sumu hata hivo hizo lozi chungu zinatumika katika mambo ya kutengenezea cosmetics, mafuta ya lozi (almond oil) pia na perfumes.


  Nchi mashuhuri yenye Lozi ni Morocco, pia lozi zilionekana katika miaka mingi nyuma katika nchi ya Syria na Palastine inasemekana katika zama za Nabii Issa A.S. Hata hivo sasa hivi lozi zinazalishwa sehemu nyingi duniani kama Italy,California,Australia,Sou th Africa,Kashmir na sehemu nyingi za Asia.


  Food Value: Minerals and Vitamins
  Moisture 5.2% Calcium 230 mg
  Protein 20.8% Phosphorus 490 mg
  Fat 58.9% Iron 4.5 mg
  Minerals 2.9% Niacin 4.4 mg
  Fibre 1.7%
  Carbohydrates 10.5%


  Ndani ya lozi pia kuna upatikanaji wa copper, iron phosphorus na Vitamin B, vitu hivi vinasaidia katika upatikanaji wa new blood cells, haemoglobin pia inasaidia ubongo, mishipa, mifupa, moyo na ini kufanya kazi kwa wepesi kabisa. Lozi insaidia kupanua na kutia nguvu muscles za ubongo katika kuongeza fahamu.


  Old ages:Utu uzima wa kiumri.
  Chukua lozi kiasi na uziroweka katika maji na baadae utoe ngozi yake ikisha uzisage na kufanya paste kwa kutumia kama siagi, hii huongeza proteins ndani ya mwili na hasa kwa watu wazima, pia unaweza kutia katika maziwa na ukanywa hii nzuri kwa watoto.


  Anaemia: upungufu wa damu
  Kuna upatikanaji wa copper katika lozi katika rate 1.15mg per 100 grams, copper pamoja na iron na vitamins hizi zinatumika kama ni catalyst katika mfumo wa blood haemoglobin. Kwa hiyo wenye maradhi ya upungufu wa damu ni vizuri mtu kutumia lozi kwa sana.


  Constipation:kupata choo
  Kwa wale wenye matatizo ya kupata choo, ni uzuri kula lozi wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala.


  Impotency:upunguvu wa nguvu za kiume
  Kwa wale wenye upunguvu wa nguvu za kiume na za kike, wale lozi kwa wingi.


  Skin Disorder:maradhi ya ukoma
  Kwa wale wenye maradhi ya ukoma, wasage lozi iwe laini ikisha wajipake pale palipoathirika, na pia kwa wale wenye pimples.

  Tumia kisha unipe Feedback rakeyescarl
   

  Attached Files:

  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huko Dar nitazipataje? Lozi ni kiswahili au kiingereza?
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,022
  Trophy Points: 280
  Nenda katika Ma Super Market utazikuta nenda Sokoni Kariakoo ndani uliza Lozi ni Kiswahili utazikuta kwa kiingereza inaitwa (Almond) distazo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,220
  Likes Received: 1,625
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu. Kuna depression uliiweka ndani kwa muda mrefu, sasa umepata kazi ndio stress zinajiachia. Kwanza kuwa na attitude chanya kwa maisha. Kuna watu wamekaa 5 years bila kazi, wengine kwa ugonjwa hawaamki kitandani na hawajui wanapona lini. Count your blessings. Una mke, watoto wanaokupa support na sasa kazi. Jivike ujasiri, utazoea tena maisha ya mikiki ya barabarani. Mungu aliekutunza toka utoto wako, magumu uliyopitia hata sasa, bado atakutunza. Kila la kheri. Mungu wako atarudisha kila kilichoibwa na Ibilisi.
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,220
  Likes Received: 1,625
  Trophy Points: 280
  Halafu umepotea muda mrefu wewe! Nafurahi kukuona tena. Karibu.
   
 9. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 9,579
  Likes Received: 1,646
  Trophy Points: 280
  kuna clubu ya watu wenye msongo wa mawazo, wavutaji sigara waliokubuhu, wanywa pombe walipitiliza na watu wenye matatizo mbalimbali. Huwa wnakutana hapo mitaa ya Muhimbili, wanachokifanya ni kuhadithiana life style zao, wanakunywa kahawa pamoja na wanashiriki mazoezi madogomadogo. kupitia stories, unajikuta matatizo uliyonayo ni robo ya mwenzio, hivyo unaingiwa na faraja, unatabasamu unafurahi na wenzio.

  Namna ya kufika, nenda muhimbili hospital, onana na psychotherapist, naamini atakuwa anafaham wapi hao jamaa wanakutana lini na mda gani.

  Pole sana, lakini kumbuka raha mtu hujipa mwenyewe, usingoje kupewa raha. Mshukuru Mungu una mke na watoto, naamini kama tatizo lako halihusiani na kipato na hvyo kuona familia ni mzigo kuitunza, basi familia ndiyo faraja yako tosha.

  Mungu akupe nguvu brother
   
 10. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 13,797
  Likes Received: 1,529
  Trophy Points: 280
  pole sana mkuu,lakini issue yako zaidi ya kutumia dawa inatibika pia kwa kupata ushauri,mara nyingi ukifika hiyo age watu huwa na hofu ya maisha hasa kama yale mengi aliyoyatarajia kuyatimiza kwenye umri huo hayajatimia
  pengine watoto ulionao ni wadogo na wanakutegemea bado hivyo ukichanganya na kuwa imekuchukua muda kupata ajira tena na pia hiyo ajira kipato ni cha wastani ,i bet ni kidogo zaid ya ulichokuwa nacho wakati unafanya kazi!
  huna sababu ya kujiumiza kwa tafakari ,relax!tayari umefanya lililo ndani ya uwezo wako kwa ajili ya familia yako!jitune kukubali mabadiliko na kujikubali since bila hivyo hata ukinywa dawa bado litakuwa ni tatizo!pia zungumza na ulio karibu nao hasa mkeo na watoto ili wakubali kuwa maisha yanaweza kuwa ya tofauti!
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,228
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  pole mkuu. Yawezekana una fear of the unknown. Kwenye subconscious mind yako kuna mambo ambayo yamejizika huko na yanahitaji kufukuliwa. Mtafute mwanasaikolojia mmoja wa hapahapa bongo anaitwa chris mauki anaweza kukusaidia. Uki google utapata taarifa zake.
   
 12. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 400
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nawashukuru sana tena sana kwa waliosadia kwenye hii habari. Na wote walionitumia kwa PM. Sina njia ya kuelezea furaha na shukurani zangu,najua ingekuwa gharama kubwa sana,kupata hizi habari.
  Asanteni kwa kusoma kwenu na mbarikiwe sana.
  RE.

  FYI:Nilikwenda sana ma hospitali mengi-DAR na huyu ndg yangu,lakini ukifika pale que na matatizo waliyonayo wengine -unajikuta mmeondoka.Hii nchi tuombe sana mungu atujalie hospitali kamilifu na zenye ma Dr.wa kutosha kwenye kila fani.
   
Loading...