Annina
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 437
- 57
Wapendwa,
Nipo kwenye serious mahusiano na kwa mapenzi ya Mungu tunaweza kufunga ndoa. Tatizo nina wivu kupita maelezo, yaani saa zote nahisi kuibiwa...kwa mfano kuna siku nilikuta amempa lift zilipendwa wake na alikuwa amekaa kwenye siti ya mbele ya abiria, niliumia kupitiliza nikaacha kuitumia ile siti, kuanzia siku ile nikawa nakaa siti ya nyuma kama balozi! Baada ya muda akabadili gari -thanx God sasa nakalia siti yangu!
Nyumba anayoishi nimebadili karibu kila kitu kwani nahisi vina uhusiano na mpenzi wake aliyepita na vinaweza kumkumbusha waliyokuwa wakifanya - siwezi kuvumilia, nimembadili hata yeye - mavazi, perfume, sehemu za kutembelea nk nk yote hii ni kuhakikisha mimi ndio natawala mawazo yake na si vinginevyo, lengo ni kwamba kila kitu kinachomzunguka kiwe kinamkumbusha mimi! Akisafiri tunakesha kwa PC na simu... kuhakikisha yupo peke yake nitamtaka afanye mambo kadhaa ili nijiridhishe siibiwi... msg zikiingia kwenye simu yake mapigo ya moyo yanabadilika...huwa najitahidi kujizuia kusoma msg hizo lakini asiponiambia nani ametuma na kuniruhusu kusoma naweza kukosa usingizi siku kadhaa!
Jamani nisaidieni, ni mimi tu au na wengine wako hivi? Nina wasiwasi atachoka, kuna wakati naona namnyima uhuru, najaribu kujizuia lakini nashindwa, nifanyeje?