Nina wiki ya pili kazini, ila nataka kuacha kazi

Sasa kwa akili hizo ataweza kazi za kukaa camp porini kuudumia wazungu wanaokuja kuwinda kwa miezi 6 bila kurudi nyumbani?
Ataweza ndugu.....
Huu ni mhemko wa ugeni pia inawezekana hii ni kazi yake kwanza ya kuajiriwa na pirika pirika za ujana ndio vinavyomyumbisha.....kama anafanya kazi kwa ajili ya kesho yake njema atastahimili na kuingia katika ulimwengu mpya.......akiizoea hali hiyo hata kaa tena fanye kazi za mijini........Kuna mpwa wangu mmoja aliwahi kupata huko machakani alikuwa kila siku vilio, lakini alivyoyazoea mazingira ya huko.....huu ni mwaka wa nne yupo huko na ameoa huko huko na kimaendeleo sio haba ukilinganisha na alivyokuwa hapa mjini.....
 
Niunganishe kwenye goli lako kaka.. nakupa asilimia 60 ya faida. Mimi nachukua asilimia 40. Na kuna msingi wangu ntaongezea
Hizi ni lugha za watu waliokuwa desperate na kutafuta kazi......btn the line hakuna mtu mwenye ofisi yake anayeweza kukuachia ofisi yake kwa kauli kama hizi......vijana wajifunze kujikuza kimawazo yenye uzalishaji na sio kuwa desperate
 
Kama ni mazingira ya bush basi huko ndio nafuu sana kwa uzoefu wangu mimi wa kutembelea hii nchi yetu.

Hapo ongea na mwenye guest umlipe kwa mwezi na atakufanyia nafuu sana hilo linawezekana kabisa vinginevyo ni wewe umezoea mambo ya mjini huko unayakosa ndio unaona hapakufai, ila kwa mshahara huo na mazingira hayo na wewe ni msela unanafasi nzuri sana ya kujipanga kimaisha kwa sasa.
Yaani bushi sana utakuta huko chumba ni elfu 10 kwa mwezi na guest haizidi elfu 6.

Chai hii huyu anatunywesha
 
Kula tu per day ni 10k, usafiri mpaka ofisi ilipo kwenda na kurudi 3k.bado sijapata ghetto hivyo naishi Lodge,per day ni 12k.

Ulipokuwa unapiga winga na kupata 300k kwa mwezi, hukuwa ukila , safiri na kupanga chumba?

Iweje matumizi yaongezeke baada ya kuanza kupata 850k?
 
Yaani bushi sana utakuta huko chumba ni elfu 10 kwa mwezi na guest haizidi elfu 6.

Chai hii huyu anatunywesha
Hujafika alipopataja wewe,tena hiyo guest aliyotaja elf 12 ni nafuu mi nilienda lodge ilikuwa 15 na hakuna kupunguziwa na hakuna vyumba vya kupanga,huko inyonga paskie tu kuna sehem hata huwatumii simu wanatumiana barua na gari iko moja tu inaondoka asbh na kurud jion. Mtoa mada nimemwelewa sana sema avumilie tu atazoea.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mazingira ya hii kampuni tu hayajanivutia. Ni kazi ya mkataba wa mwaka mmoja(renewable). So naona siwezi kuendelea nao mbele.

Ndio kwanza nina week ya pili kazini ila nataka kuacha.

Mnanishaurije?

Bila kusema sababu tubakushaurije? Akili iliyoandika Hii ni dhahiri Ina matatizo; kwa maana ya kigezo cha akili yako ya kutegemea ushauriwe na ujaeleza kitu nakushauri endelea na kazi maana judgement yako itakuwa Sio nzuri....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom