Nina wazo la kuuza vyakula vya asili kwa ajili ya kuboresha afya kwa wakazi wa mjini. Ushauri wenu tafadhali

Rwaz

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,964
3,311
Naweza kukosea kichwa cha habari mniwie radhi.

Nina wazo la kuwarudisha wakazi wa mjini kwenye vyakula vya asili vilivyowapa bibi na babu nguvu na afya njema. Corona imekuwa alarm ya kujitafakari kuhusu kula kwa afya.

Watu wengi mjini hula chakula kisafi na si chakula kizuri, kwa tafsiri ya kiafya. Naomba mawazo nikifungua eneo maalum (au deliveries) la kila mtanzania kula kikwao, vyakula vya kuufanya mwili imara zaid.

Pia ni ufahari kula kikwenu ukiwa mjini. Bila kusahau elimu kubwa ya kujitenga na vyakula vizuri kwa macho lakini kiafya ni bomu.

Wengine wameoa tofauti na kabila zao wanakosa kula kikwao. nitakusanya wapishi toka huko kwa makabila husika. Ukweli mchungu ni kuwa watu wengi mjini wana hela zao lakini wanakula ovyo kwa sababu hakuna namna au chaguzi za kutosha.

Mf. menu inaweza kuwa ndefu lakini vyakula vyote ni kundi moja la mafuta ndo mana matatizo kama nguvu za kiume hayako vijijini, wengi wanakula mapishi mazuri lakini si chakula bora. (Nategemea wateja wengi wa ndizi za kiasili na order kadhaa za kichuri)
 
Unamaanisha ugari wa muhogo, togwa, bunyongwe, chambishi...ukauze pale Kariakoo.

Kila la kheri
 
Unamaanisha ugari wa muhogo, togwa, bunyongwe, chambishi...ukauze pale kariakoo.

kila la kheri
Togwa! Kampun za soda na juice zitaandamana. nalenga vyakula.
 
Ukihitaji mtaalamu wakupika

Kiburu
Shiro
Ng'ande
Ngararimo
Kizeri
Kitawa
Mahindi ya kukaanga

Usisite kunishtua boss
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom