Nina wazo la kuanzisha kikundi cha vijana kwa ajili ya kulima na kufuga

igihumbi

JF-Expert Member
Feb 20, 2017
441
350
Habari za kutwa mwana jf mwenzangu?.
Leo nimefikiria jambo nikaona sio mbaya kama tukilijadili kwa pamoja. Tatizo la watu wengi ni kutokuwa na ujuzi katika jambo fulani hasa katika ukulima au ufugaji unakuta mtu anamtaji ila ni namna gani ataweza kuendesha swala zima la kilimo au ufugaji inakuwa ngumu kufikia muafaka.
KWA MTAZAMO WANGU.(kila mtu atakuwa na mtaji wake ila tutalima katika eneo moja ila kupeana uzoefu)
Tuunde kikundi ambacho baadae tutakisajili tutajadili ni kilimo gani tukiendeshe.
mfano tupo watu 7 na tumechagua kilimo cha mpunga tutatafuta eneo la heka 21 kila mtu pata heka 3. Safari itaanzia hapo tutalima hadi mavuno kwa pamoja itatusaidia kupata uzoefu zaidi na hata badae tunaweza kuchukua mikopo kwa ajili ya kilimo maana tiyari tutakuwa tumesha fahamiana.
Karibuni kwa mawazo.
nb: Hakuna mtu atakae shika pesa za mwenzake bali kufanya kila kitu kwa pamoja kama ni kulipia shamba basi tutamtafuta muhusika baada ya hpo tutalipia kwa pamoja kila mtu akiwa anaona..

Link ya kujiunga na group la whatsapp
Kilimo kwanza
 
Ni wazo zuri sana kama wote mtakua na mtazamo sawa, kulikua na Jamaa anaitwa Jordan Rugimbana walianzisha kikundi chao, wakalima, wakafuga, wakajenga nyumba zinazofanana na kisha wakaoa wanawake ambao nasikia walikua wafanyakazi wao (hili sina uhakika nalo) Jirdan Rugimbana alikuja kuwa DC then RC sijui akatoweka wapi huko...na hata kuonekana kwake kwenye siasa ilikua throiugh huo mradi
 
Kuna jamaa namjua ni member wa JF. Na pia alikua mstari wa mbele sana kwenye suala la FOREX humu jukwaani. Alikusanya vijana kwa wazee mtaani kwetu pande za Temeke Buza kwa wazo kama lako. Mwisho wa siku amekimbia na zaidi ya milioni 5 za watu hajulikani alipo.
Imefika kipindi nikiona mada kama hizi nashindwa kuamini nahisi kabisa moja ya lengo kubwa ni upigaji. nasisitiza tena huyo jamaa namjua na ni member mkubwa na muda mrefu JF. Ila yeye hatambui kwamba nafahamu hadi id yake humu.
 
Kuna jamaa namjua ni member wa JF. Na pia alikua mstari wa mbele sana kwenye suala la FOREX humu jukwaani. Alikusanya vijana kwa wazee mtaani kwetu pande za Temeke Buza kwa wazo kama lako. Mwisho wa siku amekimbia na zaidi ya milioni 5 za watu hajulikani alipo.
kipindi nikiona mada kama hizi nashindwa kuamini nahisi kabisa moja ya lengo kubwa ni upigaji. nasisitiza tena huyo jamaa namjua na ni member mkubwa na muda mrefu JF. Ila yeye hatambui kwamba nafahamu hadi id yake humu.
nikweli mkuu huwa inatokea ila hii ni tofauti hakuna mtu atakae shika pesa za mwenzake.
 
kwasababu hujawahi kuwa karibu nao ukitaka kujua level za maisha yako angalia marafiki ulionao

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisaa marafiki zangu mostly wako kwny financial institutions,accounting firms,hustlers(madeal) etc

Labda nianze kutafuta marafiki ambao ni wakulima wa matikiti ntawaona walio matajiri pande hizo.
 
Nimependa hilo wazo maana na mimi ni kijana ninaependa sana kilimo ila uzoefu sina naona tukiwa hata watano tutaweza kupeana ushauri na motisha zaidi
 
Ushirika nchi hii ulishashindikana , hatofika mbali alafu zao la mpunga linalipa sana changamoto mnalima kwa means hipi? Umwagiliaji? Mvua? Mechanization? Au mnatumia vibarua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom