Nina wasiwasi Waziri Muhongo na Katibu wake, wanaweza kuumbuka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina wasiwasi Waziri Muhongo na Katibu wake, wanaweza kuumbuka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtz-halisi, Jul 29, 2012.

 1. Mtz-halisi

  Mtz-halisi Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimefuatilia sana hoja za wabunge na waziri na naibu wake juu ya TANESCO, ninaona siasa zaidi kuliko hali halisi, hapo ndipo naungana na Zitto kabwe. Sakata la Jairo lilipita bila kutajwa wabunge walio hongwa watanzania tukafurahi sana kwa sababu mtu mmoja kasimamishwa kazi kwa taratibu zilizokuwa zinafanywa na wizara zote huko nyuma.

  Waziri pamoja na katibu wake walifanya lobbying kwa wabunge wasimamie hoja za kijinga ili budget yao mbaya ipite, Kwa sababu tuna wabunge wajinga na wapenda sifa kila mmoja alisimamia wala rushwa, hapo ndipo prof alishinda; ukitaka kumshinda mjinga hapo ndipo panafaa; Mjinga yeyote anasimamia sehemu nyepesi iliaonekane ana uchungu.

  Kwa jicho langu la Mbali muheshimiwa Lowassa kawashinda wote washindani wake na kwa hili anasitahili kupewa uwaziri Mkuu walio mpokonya. Kwa sababu inaonekana ni hawa wabunge wala rushwa ndio walitunga ule uongo. Katika hili wengi wataingia hata ambao hatuzanii kama Mwakyembe, Makamba junior etc.

  Kibaya zaidi wanasema wabunge, hawasemi Fulani na Fulani mbona Kafulila alisema kipindi kile Zambi, na yule aliyekamatwa na Rushwa wamefanya abc, lakini leo hatuambiwi majina; Wabunge wa CCM ukiona wamesimama hivyo amini usiamini wamekomaa wakiamini Zitto kala hizo pesa, lakini kwa Siasa za Zitto naamini hawezi fanya ujinga kama huo.

  Siku si nyingi tutaanza mgao wa Umeme, ndipo uongo na Ukweli wa Waziri wetu tutaujua.

  Naomba niishie hapa
   
 2. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,247
  Likes Received: 10,423
  Trophy Points: 280
  naona zogo lenu linaishia katika kuwakatia wananchi umeme.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,412
  Likes Received: 81,450
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu Wabunge waliochukua rushwa mwaka jana toka Madini na Nishati ili wapitishe kinyemela bajeti ya Wizara ile lazima majina yao yote yaanikwe hadharani na wapandishwe kizimbani kujibu mashtaka ya kupokea rushwa na hatimaye wote wafukuzwe bungeni kama watakutwa na hatia ya kupokea rushwa.

  Na hawa wanaodaiwa kuchukua rushwa toka Tanesco's board of directors & Management team nao pia wapandishwe kizimbani na wakionekana wana hatia basi wahusika wote hawastahili kuwa wawakilishi wa Watanzania kule Bungeni.
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wanaotetea wabunge walarushwa ni wanafiki wakubwa
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,412
  Likes Received: 81,450
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Wabunge wapokea rushwa wakamatwe

  Tanzania Daima


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]TUHUMA za rushwa zilizotolewa na baadhi ya wabunge dhidi ya wenzao katika Wizara ya Nishati na Madini, zimemfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuridhia kuvunjwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

  Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wajumbe wake kukumbwa na tuhuma za kupokea hongo kutoka kwa baadhi ya kampuni za mafuta ili kuficha ufisadi wa vigogo ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Sisi Tanzania Daima Jumapili, tunaungana na Watanzania wote kukemea vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya wawakilishi hao ambao wameamua kwa makusudi kuuacha uaminifu na kusimamia haki kwa masilahi ya watu wachache.

  Kitendo hicho si cha kuvumilika, pamoja na Spika Makinda kuamua kuvunja kamati hiyo, ipo haja ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwachunguza wabunge hao na ikibainika walihusika na kuchukua rushwa basi sheria ikuchukue mkondo wake na wakamatwe.

  Wabunge hao si kuwa wamelidhalilisha Bunge na taifa kwa ujumla, lakini pia kumdhihaki Mungu, hasa kupitia sala inayoombwa wakati wa kufanyika kwa vikao hivyo.
  Tunaamini kuwa wanaomba sala hiyo huku ndani ya mioyo yao wakiwa hawana nia thabiti, bali ni kutaka kuonekana wema mbele ya jamii.

  Tulitegemea wabunge hao ndio wawe mfano wa kuigwa katika kukemea vitendo hivyo, lakini badala yake wao ndio wameongoza kufanya jambo ambalo linaashiria kuwa kuna mikataba mingi isiyo na tija ambayo inaingiwa kutokana na wabunge kupewa fedha.

  Tunaelewa kuwa pamoja na wabunge hao kuongezewa posho bado wamekiuka uadilifu, uwajibikaji na kuweka tamaa mbele kwa masilahi yao binafsi.

  Kamwe jambo hilo si la kuachwa lipite, kuna umuhimu wa kuangalia upya viongozi tunaowachagua ili kutuwakilisha, maana hili linatoa picha kuwa kuna baadhi wanaweza kuingia mikataba mibovu hata ya kuiweka nchi rehani.

  Kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la wabunge kupigiwa kelele za kupokea rushwa ni wazi kuwa viongozi hao inaonesha waliingia madarakani kwa njia hiyo, hali inayowafanya wasahau wajibu wao unaowakabili.

  Tunaona kuna haja ya kuhakikisha viongozi wetu wanapatikana kutoka katika vyuo vya kiuongozi ili kuwa na maadili kwa kuwa sasa inaonekana kuwa maadili yameporomoka na bungeni kumekuwa kama sehemu ya eneo la kujificha.

  Pia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) inatakiwa kuacha kukalia majadala ya vigogo wanaotuhumiwa kwa rushwa, kwani wapo baadhi wanashindwa kufikishwa mahakamani kwa kisingizio cha kuwa na kinga.

  Hatuwaoni watuhumiwa wakubwa nchini kwa mfano wa kesi ya rada wakifikishwa mahakamani. Bila shaka ni kutokana na mfumo huo unaotoa nafasi ya kulindana ndiyo maana imefikia mahali mbunge haoni aibu kupokea rushwa.

  Tunaamini kuwa umefika wakati taasisi zinazohusika zishirikiane kwa pamoja ili kuondoa aibu hii ndani ya Bunge letu tukufu na taifa kwa ujumla, maana kama mwakilishi wa wananchi anachukua rushwa ni wapi tunaelekea? Hii ni wazi hakuna utawala bora!


  [​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 6. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,948
  Likes Received: 37,461
  Trophy Points: 280
  Mtz-halisi

  Mkuu unajua watu hawako makini.Kuna kauli moja alitoa waziri wakati anafanya majumuisho kuwa hata hizo fedha za kulipia mafuta hayo ya PUMA bado hazijalipwa.Sasa jiulize kama wanashindwa kulipia hayo mafuta tutarajie nini siku za usoni.Huyu waziri maskini naona kaingia choo cha kike na haya mambo ya wanasiasa yatamshinda siku si nyingi.Na ajue kabisa ni hao hao ndio watamgeuka maana hapo alipo ndipo penye ulaji na yeye anaonekana amejipanga kuwadhibiti.

  Na kwa kushindwa kulipia mafuta huenda ikawa ni sababu nyingine iliyopelekea kununua mafuta kwa mkopo kutoka PUMA.Tukumbuke kuwa PUMA iko chini ya serikali kwani serikali ina hisa.Kwahiyo ni rahisi hata kuwakopa kuliko makampuni mengine.Hatari ninayoiona hapa itafika hatua hata hawa PUMA watashindwa kutoa hiyo huduma na hapo ndipo mgao utaibuka tena.

  Serikali yetu imekuwa na tabia ya kukopa kutoka makampuni ya ndani na kushindwa kulipa. Mfano ni NSSF,PPF n.k.Kumbuka hata TANESCO wanaidai serikali fedha za bili ya umeme.

  Hii kauli kuwa mgao wa umeme ni wa kutengeneza umekaa kisiasa zaidi.Siamini kama kila mgao ulikuwa wa kutengeneza.Kweli serikali ingekubali kuandamwa na kusemwa kwasababu tu ya mgao feki wa umeme?Kweli serikali ingekubali kukopa mabilioni ya hela ili kuondokana na mgao feki?Siamini kama serikali siku zote ilikuwa haiijui kwa kuna hujuma kama hii.

  Tutapata majibu siku si nyingi.Kuficha ukweli ni kazi ngumu sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ni kwamba kutakuwa na mgawo hivi karibuni?

  Mimi naamini Wizara ya Nishati na Madini imepata watendaji wazuri ambao si wanasiasa bali wachapakazi. Eliackim Chacha Maswi ni kiongozi thabiti sana tangia akiwa shule huko SHYCOM pamoja na UDSM sina shaka naye. Prof. Muhongo naye ni kiongozi thabiti mtendaji asiyejua manbo ya siasa bali utendaji. Hakuna shaka kwamba hawa watu wamekata mirija pale TANESCO na kwa hakika wataandamwa kwa hila nyingi ili kama alivyosema Rais waondoke kwa kuwa wengi walikuja na kupita. Ni juu ya viongozi wao wakuu yaani Waziri Mkuu na Rais kuwalinda na kuwasaidia wasiingiliwe na wanasiasa ili waliokoe taifa hili kutokana na madhira ambayo limekuwa likipata kwa mali zake kupokwa.
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Huyu alieanzisha thread hii kama siyo Zitto mwenyewe basi ni yule mwandishi wa Gazeti lake Zitto la Mwananchi analolitumia kwa Propaganda zake. ila kwahili Zitto umenasa na huna pa kutokea, only time will tell, huwezi kutufanya wote wapumbavu kwa maslahi yako, nenda peleka ujinga wako kwa wale watoto wa Kigoma All Stars.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jul 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Salary slip;

  Mkuu nakuomba unihakikishie kwamba serikali yetu ina hisa asilimia 50 ya PUMA ENERGY International - Bofya Au tuna own kiasi hicho kwa franchize ya Bongo tu..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Ni suala la muda tu,Zito sio mjinga kiasi hicho!
   
 11. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,948
  Likes Received: 37,461
  Trophy Points: 280
  Mkuu sioni hata dalili ya hili jambo.Ni jambo la kushangaza sana.Inabidi wabunge wahoji kauli hii.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Jul 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nimesoma mahala ya kwamba BP shell Tanzania walipoondoka ndio waliwauza share zake kwa hawa PUMA energy wakati huo tukiwa na ubia nao 50%. Sasa Sielewi kilitokea nini hadi serikali yetu isichuke kila kitu.. Na yalikuwepo makubaliana gani ya kimkataba na BP Shell ikiwa mmoja atashindwa kuendelea na biashara..

  Kilichofanyika binafsi yangu nina mashaka sana na mpango mzima na wahusika wake maana imetokea wakati Ufisadi ndio unatawala siasa na uchumi wa nchi. I believe kuna mkono wa mtu ndani maana unaweza kuwa na McDonalds Bongo akakuuzia share halafu mtu ukadai nina share 50% McDonalds bila kujua kwamba its is a franchize. Gas Station ya BP Shell iliyopo bongo sio mali ya BP Shell ni ya mtu binafsi aliyenunua franchise na kutumia jina la Shell kwa mkataba wa kuuza mafuta ya BP Shell on profit...

  Hivyo inawezekana kabisa hapa tuna mkataba na mtu mkubwa nchini ambaye ni kiongozo aliyenunua Franchise ya PUMA na hivyo kutuingiza ktk Ubia.. Kwa changa la macho hilo watu wanafikiri tuna share Puma energy International ya asilimia 50 wakati sivyo.
   
 13. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kama unategemea viongozi dhaifu wanaokwenda kwa upepo wa wanamtandao wanaweza kuwalinda prof Muhongo na katibu mkuu wake basi umekosea sana! kama waziri hana mpango mkakati wa kujilinda mwenyewe ajihesabu ameliwa. Rushwa imezaliwa na kukulia ikulu hukohuko!
   
 14. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,948
  Likes Received: 37,461
  Trophy Points: 280
  Mkuu naamini utakuwa umefungua njia kwa watu mbalimbali kuanza kuchunguza jambo hili.Jf inatumiwa na watu mbalimbali ikiwamo wanasiasa na watu wengine.Tuvute subira.
   
 15. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,894
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  kwa kutuhumiwa tu kupokea rushwa ushapoteza sifa ya kupeperusha bendera ya urais labda ya ccm hata ukianzisha thread mia kwa id zako feki
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimetoa rai ili viongozi hao wa juu wawasaidie kwa kuwalinda kutokana na vinywa vyenye kiu ya fedha. Bila kulindwa kwa kweli hawatadumu watatengenezewa zengwe hadi wang'oke ili mirija izibuliwe.
   
 17. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,276
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Mkuu mkandara,naanza kuona mwanga fulani hivi hapo kwenye wamiliki wa puma hapa nchini.does the gov have 50% share?who is the other share holder?je ni mbongo aliyenunua share za puma au ni puma wenyewe.kazi ipo.nategemea intelijensia ya jf ita come out na reliable findings.
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kimbunga naona Molemo na Mwita Maranya wanakushambulia kutokana kupingana nao mtazamo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jul 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hii ni muhimu zaidi kwa sababu mtu huyu akijulikana hatakuwa na tofauti na Mhando na bado Symbion na mashrika mengine yote ya kuzalisha umeme yanatakiwa kutazamwa kwa undani. Kifo cha TIPPER hakiwezekani kuwa ilikuwa lazima ife, sioni kabisa sababu..
   
 20. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Duh! theory bado zinaongezeka tu
   
Loading...