Nina wasiwasi, na Taarifa za CAG zijazo, kama hazitachakachuliwa kuepusha aibu kwa Watawala.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina wasiwasi, na Taarifa za CAG zijazo, kama hazitachakachuliwa kuepusha aibu kwa Watawala..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theophilius, May 3, 2012.

 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi, matokeo ya ripoti ya CAG yalivyoichachafya na yanavyoendelea kuihenyesha serikali ya CCM, kiasi cha kutishia kuangushwa isipochukua hatua za maana dhidi ya madudu yaliyoripotiwa katika ripoti hiyo, naigiwa wasiwasi, ikiwa CAG wetu huyu ataendelea kuwa na ujasili wa kuandaa ripoti nyingine kali kama hii.

  Ninazo sababu.. kwanza nitoe tu mfano wa hili ninalozungumzia, Mwaka juzi pale Baraza la Mitihani lilipotoa matokeo ya kidato cha nne, mabaya sana kuwahi kutangazwa, ambayo yalisababisha zomeazomea kwa serikali na sera yake ya sekondari za kata, kilichofuata ni matokeo yaliyofuata kuwa nafuu kidogo, japo hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa unafuu huo unatokana na kuboreka kwa elimu, kwa msingi wa kutatua matatizo yaliyokuwa yanaikabili sekta hiyo.

  Na hivyo kufanya wengine tufikiri (na pengine ndiyo ukweli) kwamba alipigiwa simu Dk. Ndalichako na kuombwa ajaribu kuweka mambo sawa vinginevyo, nchi inaweza isitawalike.

  Au tujaribu kujiuliza pia kuhusu, kubadilika kwa ufaulu wa shule za serikali ikilinganishwa na shule binafsi, ambapo huko nyuma, karibu shule bora (10) zote zilikuwa za binafsi na nyingi zake zikiwa za seminari. Kwa sasa mambo yamebadilika.

  Itakuwa vyema ikiwa yatakuwa yamebadilika kiuhalisia na wala si kutaka kubadili picha ili ionekane na shule za serikali au makundi mengine katika jamii nazo zinafanya vizuri hata kama hakuna cha maana katika kuziboresha kilichofanyika.

  Ikiwa mifanyo hiyo inaweza kushwii (something to go by), ni dhahiri kwamba kwa usanii wa watawala wetu, wakafanya kila wawezalo, ikibidi kumtisha CAG kuhakikisha anafanya 'Creative Auditing' ili kusafisha hali ya hewa.

  Vinginevyo mwenye ubavu wa kuniambia kwamba CAG he's really Independent in fact and appearence, na atoe hoja tujadili, vinginevyo ninayohofia yatatokea, yetu macho..
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Independence yake ipo Kikatiba ila haya mambo hutegemea uadilifu na uzalendo wa mtu. Katika nchi zetu hizi dola inaweza kukufanya usiwe independent. Lakini pia kuna hili la ufisadi. Kama hatakuwa mwadilifu basi jamaa watafanya kila njia kumnyamazisha kwa kitu kidogo ili report zao ziwe clean.
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  huyu wa sasa akiendelea kuanika uchafu wa viongozi wa nchi usije ukasikia kapigwa chini kawekwa mwingine ambae na yeye ataamua kula nao..but msiwachezee mawaziri...wajanja..huko wizarani watatafuta jinsi ya kuchakachua docs ili kubalance the books lasivyo watakua hawawezi kuchuma mali za umma tena
   
 4. theophilius

  theophilius Senior Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kumbuka wahasibu (wakiwemo wakaguzi) wanapozungumzia independence, hawaishii hapo, wanasema independence in fact and independence in appearence - kwamba hata kama itaandikwa ama katika katiba au katika sheria kwamba atakuwa independent, ishu je anaonekana kuwa ndependent?

  Kwanza anateuliwa na nani?
  Analipwa na nani?
  Na anamkagua nani?
  Jibu ni Serikali

  kama hivyo ndivyo, inakuwaje awe independent?

  mfano mzuri ni wakaguzi wa nje wanapokagua makampuni, mfano ya binafsi, wanalipwa na wanahisa ili wakague hesabu zilizotengenezwa na menejimenti iliyoajiliwa na wanahisa, hili kuwahakikishia wanahisa kwamba hayo mahesabu siyo 'mangumashi' au vinginevyo, kwa utaratibu huu ni rahisi wakaguzi katika hali hii kuikagua menejiment bila kuiangalia machoni.

  tukirudi kwa serikali, je anayewatuma kukagua akiona yanamgeuka yeye si anaweza kuwaelekeza cha kufanya au kuwaambaia "sasa basi uko mnakokwenda siko!"
   
 5. theophilius

  theophilius Senior Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  tunaambia hawei kufukuzwa hivi hivi, maana hata aliyemuweka ana uwezo wa kumfukuza. Utaratibu ni kwamba ikiwa itajitokeza sababu ya kumfukuza ambayo ni ama utovu wa nidhamu, kuugua isipokuwa kifo, itatengenezwa baraza (tribunal) la majaji (wakiwemo wastaafu ktoka nchi yoyote jumuhiya ya madola ikiwemo hapa tanzania) lenye wajumbe wasiopungua watatu ambao watasikiliza na kutolea maamuzi suala hilo, maamuzi yao yatapelekwa kwa Rais kwa utekelezaji, na kwamba katiba inasisitiza ikiwa watashauri asifukuzwe Raisi hatakiwi kumfukuza labda ampige risasi.

  Utaratibu huu kwa juu juu ni mzuri lakini, kumbuka anayeteua wajumbe wa tribunal ikiwa ndiye anayetaka afukuzwe anaweza kuhakikisha wajumbe atakowateuia hawamwangushi, na ikizingatiwa hafungwi mikono kuteua, wateule wake, ambao nao, hawafungwi mikono kulipa fadhila kwa uteuzi wao.. kwa vyovyote vile hili nalo ni suala la mjadala
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu theophilius suala la ukaguzi lina mambo yake mengi na yanaweza kukuchanganya sana. Theoretically ni kwamba shareholders ndio wana mu engage External auditor na kumlipa lakini practically Management huwa inapropose auditor na kupeleka jina kwenye AGM kwa ajili ya kuteuliwa na Management ndiyo inayomlipa Auditor. Kuna shids nyingi sana katika hayo mambo na hili ni somo ambalo wengine tunalifanyia kazi kwenye Corporate Governance. Kuna issue nyiiingi zikiwemo Board papers na jinsi companies zinavyoongozwa, Board Committees na mambo kama hayo. Kwa sasa huko duniani kuna debate kubwa juu ya auditors ikiwa ni pamoja na kwa rotate baada ya muda fulani.

  Independence ya CAG inapatikana kwenye katiba. Ukisoma ibara ya 143 na 144 ya katiba ya JMT utaona majukumu ya CAG pamoja na jinsi anavyotakiwa awe independnt. Independence pia huwa inaangaliwa kwa security of tenure ambayo CAG anayo. Kuonekana kama yupo independent ni hiyo general report ambayo ndiyo gumzo la nchi hadi sasa na imekaribia kuiangusha serikali.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. theophilius

  theophilius Senior Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  huo, ndiyo mjadala wenyewe... Nashukuru mkuu kwa mtazamo wako, wengi tunajifunza, kutokana na mijadala kama hii
   
 8. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wameona wakienda kukagua rushwa haipatikani ila baada ya seke seke hii shavu litaongezeka
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona unataka kuchukuwa mikoba ya Sheikh Yahaya ya utabiri.
   
Loading...