Naweza kusema kweli huwa nina mapenzi ya kweli katika mahusiano, nasema hivi maana huwa nikimpenda mwanamke katika mahusiano basi huwa namaanisha ila shida huja pale ambapo nahisi nimepata mwanamke tofauti na matarajio yangu.
Nasema hivi maana asilimia kubwa ya vile vigezo vya ndani kabisa unakuta hana japo huwa najitahidi sana kumweka arudi kwenye mstari vile ninavyotaka mimi mwanamke wangu awe lakini atatulia ila baada ya siku nne/tano anarudia mambo yaleyale nisiyoyapenda.
Hali hiyo ilienda mpaka akaja kubeba ujauzito, nilihisi kuwa ni yangu lakini shida ni WASIWASI je ni ujauzito wangu au laa! Mpaka amekuja kujifungua mimi nahudumia mtoto na mama lakini tatizo ni wasi wasi je ni mtoto wangu au laa!
Kuna kipindi alikuwa anaishi kwa shemeji yake sasa nahisi usikute kuna namna ilifanyika halafu nije kubambikiwa. Msaada ndugu zanguni nitawezaje kujua kama mtoto ni wangu au sio wangu pasipo kutumia vipimo vya DNA?
Mwanamke nampenda ila nina wasi wasi kwani ni mwongo mwongo sana wakati mwingine na mtoto bado ni mdogo sana hata miezi mitatu hajafikisha hivyo inaniwia vigumu kujua amefanana na nani hasa.
Inawezekana huyu mwanamke alizaa na shemeji yake au ni nini maana sasa hivi yule shemeji yake hana mawasiliano kabisa na yeye tofauti na mwanzoni ilivyokuwa wamezoeana.
Nitajuaje kama mtoto ni wangu pasipo vipimo vya hospitali?
Msaada jamani nateseka nafsini mwangu.