Nina wasiwasi mtoto si wangu. Nitawezaje kuhakikisha?

Burke

Member
May 12, 2021
27
125
Naweza kusema kweli huwa nina mapenzi ya kweli katika mahusiano, nasema hivi maana huwa nikimpenda mwanamke katika mahusiano basi huwa namaanisha ila shida huja pale ambapo nahisi nimepata mwanamke tofauti na matarajio yangu.

Nasema hivi maana asilimia kubwa ya vile vigezo vya ndani kabisa unakuta hana japo huwa najitahidi sana kumweka arudi kwenye mstari vile ninavyotaka mimi mwanamke wangu awe lakini atatulia ila baada ya siku nne/tano anarudia mambo yaleyale nisiyoyapenda.

Hali hiyo ilienda mpaka akaja kubeba ujauzito, nilihisi kuwa ni yangu lakini shida ni WASIWASI je ni ujauzito wangu au laa! Mpaka amekuja kujifungua mimi nahudumia mtoto na mama lakini tatizo ni wasi wasi je ni mtoto wangu au laa!

Kuna kipindi alikuwa anaishi kwa shemeji yake sasa nahisi usikute kuna namna ilifanyika halafu nije kubambikiwa. Msaada ndugu zanguni nitawezaje kujua kama mtoto ni wangu au sio wangu pasipo kutumia vipimo vya DNA?

Mwanamke nampenda ila nina wasi wasi kwani ni mwongo mwongo sana wakati mwingine na mtoto bado ni mdogo sana hata miezi mitatu hajafikisha hivyo inaniwia vigumu kujua amefanana na nani hasa.

Inawezekana huyu mwanamke alizaa na shemeji yake au ni nini maana sasa hivi yule shemeji yake hana mawasiliano kabisa na yeye tofauti na mwanzoni ilivyokuwa wamezoeana.

Nitajuaje kama mtoto ni wangu pasipo vipimo vya hospitali?

Msaada jamani nateseka nafsini mwangu.

1620924681755.png
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,219
2,000
Yaani hakuna shida yoyote ila tu una wasiwasi, kwanini mnapenda kujiweka kwenye tension hata bila sababu?

Hakuna mtu kajitokeza kudai mtoto ni wake, hakuna mtu umemfumania na mama watoto wako ila akili yako imeamua tu kuwa mtoto si wako, huna hata ushahidi. Ya nini yote haya mkuu. Hebu jipe tafakari wewe mwenyewe alafu kuanzia leo amini huyo mtoto ni wako na umpende kwa dhati utaishi maisha ya amani sana na furaha.

Kutumia tu kigezo kuwa alikuwa anaishi kwa shemeji yake kuamua kuwa mtoto si wako wa shemeji yake kisa hawana mawasiliano aisee umeenda mbali sana na bila sababu. Utaishia kumchukia mtoto bila shida yoyote malaika wa Mungu huyo. Hebu jiamini mkuu, acha kujitungia mambo negative kichwani na uyape nafasi yatakuvuruga hautaamini. Utaishi maisha ya taabu sana kisaikolojia bila sababu.

Labda nikuulize swali ambalo nawe ujiulize mwenyewe, kwanini akusingizie wewe? Una mali nyingi sana hapo ulipo kwamba anataka utajiri wako? Kama jibu ni hapana basi stand up and grow bro. Kuwa mwanaume anaejiamini, mtunze mama na mtunze mtoto.
 
Umezungumza maneno yamenipa tafakuri sana akilini mwangu, ni kweli uliyoyasema ila WASI WASI ni mbaya sana na kisaikolojia inaniathiri sio kidogo. Lakini nashukuru maana nimepata mwangaza na nguvu mpya ya kuendelea kuitunza familia yangu bila hiyana, unajua kuna nyakati tukipishana kauli kidogo anakimbilia kusema ataweza kubadili hata majina yangu kwenye cheti cha mtoto cha kuzaliwa akaandika ya upande wa kwao kana kwamba mtoto aonekane kama vile baba yake hayupo/hausiki kabisa na mtoto maana hata yeye na ndugu zake wote waliozaliwa pamoja hawatumii majina ya baba yao ila mama yao aliwaandikishia majina i mean second&third name upande wa mama na mambo mengine kadha wa kadha ndio maana nikaanza kuingiwa na huu wasi wasi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom