Nina uhakika Rais Magufuli kakisoma vema kitabu cha Machiaveli - "The Prince"

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,672
28,967
Za wikendi wanajamvi!

Nimegoogle na kumsoma kwa undani kuhusu huyu jamaa wa Florence Italy aliyeishi karne ya 14 during renaissance. Nimependezwa naye sana. Yani Niccolo Machiaveli ana Nondo Za hatari alizozishusha kwenye kitabu chake cha The Prince.

Nina uhakika kabisa Rais Magufuli anayo nakala ya The Prince toka zamani na ndio anaziapply. Mwengine ni Kagame na El Sisi wao ndio kabisa Niccolo kawateka. Baadhi Za quotes na Nondo Za huyu jamaa ni hizi hapa chini. Pia kwa kumfahamu vizuri unaweza kuingia hizi linki na kusoma quotes

-There is no other way to guard yourself against flattery than by making men understand that telling you the truth will not offend you.

-
f an injury has to be done to a man it should be so severe that his vengeance need not be feared.
Niccolò Machiavelli, The Prince

-it is much safer to be feared than loved because ...love is preserved by the link of obligation which, owing to the baseness of men, is broken at every opportunity for their advantage; but fear preserves you by a dread of punishment which never fails.
Niccolò Machiavelli, The Prince

-he who seeks to deceive will always find someone who will allow himself to be deceived.
Niccolò Machiavelli, The Prince

-Since love and fear can hardly exist together, if we must choose between them, it is far safer to be feared than loved
Niccolò Machiavelli, The Prince

Nondo zake zingine bofya hapo chini

The Prince Quotes by Niccolò Machiavelli

Niccolo Machiavelli
 
Kwani hicho kitabu kimeandikwa kwa lugha gani? Kama sio kisukuma au kiswahili, I doubt!
 
Mifumo ya kiuongozi imebadilika sana duniani, haiwezekani kabisa kiongozi wa sasa afuate mafundisho ya Machiaveli itakuwa ni sawa kabisa kushikiwa akili na mtu mwingine. Tunamsoma machievelle ili kufahamu tu concept za tawala zilivyo evolve na si kuapply. Hata jinsi tunavyowapata viongozi wetu ni tofauti na kipindi cha Machevelle.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Machiavelli was a real father of political science. PM is A Machiavellian, for Him is better to be feared that loved if you cannot be both. The end justifies the means. I give you a thumb for realizing that JP is a follower of Machiavelli (Statesman and political scientist)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haonekani ni kama mtu anayejisomea vitabu. Kitabu cha mwisho amenunua labda ni cha kemia miaka 20 iliyopita.

The Price kina manufaa kwa aristocrats wa miaka ile. Kwa sasa utaonekana jangili tu.

Heshima Mkuu, introvert .

Nakubaliana na wewe kabisa. Leaders are readers, if you fail to read you'll fail to lead. Hatuna viongozi wanaopenda kusoma. So far hata kuhamasisha watu wasome kwa aidha kuonekana katika maktaba zetu au hata mashuleni nayo hakuna.

Kiongozi hupendi kusoma. Sasa utaweza vipi kusoma Mkataba wa kurasa 250 kama si kuishia kupekua pekua na hatimaye kutuingiza utumwani kama kina Mangungo wa Msovero?.

Hivi kiongozi haoni clarity ya kwenda Maktaba kujisomea?. Mbona Mwalimu alipenda kusoma?. Iweje sie tusipende kusoma?.

Ukienda Maktaba Kuu ya Taifa utacheka. Kuna vitabu vya ajabu ajabu sielewi. Watu wameiba vitabu mule na hakuna anayejali. Nani anapenda kusoma?. Kuongozwa na watu wasiopenda watu wasome ni hatari sana kuliko kuwaongoza watu wasiopenda kusoma.

Bado nafanya tafiti za kina ya kuwa ni Taifa gani/lipi limeweza kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja zote za maisha pasina watu wake kupenda kujifunza, kusaili, kudodosa na kadhalika ila bado jitihada zangu hazifui dafu. Gharama ya kuwa na Taifa la Mazuzu ni kubwa sana ukilinganisha na gharama ya kujenga Maktaba ili watu wajisomee.

Nirudi kwa Machiaveli, The Prince. Hiki kitabu ni kizuri sana. Tatizo linakuja pale unapokisoma vibaya, hapa wataalamu wa Fasihi wananielewa. Katika usomaji wa Vitabu ni lazima ufanye uchambuzi. Hulazimiki kuamini kila kitu kuhusu alichokiandika mwandishi. Unapembua pumba then unaacha mchele. Hii ndiyo nidhamu ya kusoma. Hatuna kitabu kibaya, tuna usomaji mmbaya.

Baba akisoma, Mama akisoma na mtoto pia atasoma. Tatizo letu ni kuwa Baba na Mama hawapendi kusoma then wanategemea mtoto asome. Hatujui kuwa 75% ya mambo wanayojifunza watoto ni kwa kuyaona kutoka kwa wazazi na si wanayoambiwa na wazazi?.

Books help us to grow. Hekima ni Uhuru, Uhuru ni Hekima.

Asalaam.
 
Mifumo ya kiuongozi imebadilika sana duniani, haiwezekani kabisa kiongozi wa sasa afuate mafundisho ya Machiaveli itakuwa ni sawa kabisa kushikiwa akili na mtu mwingine. Tunamsoma machievelle ili kufahamu tu concept za tawala zilivyo evolve na si kuapply. Hata jinsi tunavyowapata viongozi wetu ni tofauti na kipindi cha Machevelle.

Sent using Jamii Forums mobile app
Doh. Hiki kitabu hujakisoma vizuri mkuu. Hata kama ulikisoma basi ulisoma principalities chache sana.

Mfumo wa utawala kipindi cha machiavelli na sasa haujabadilika sana. Angalia alipokuwa anaelezea mfumo wa kutawala nchi ya kituruki na alipokuwa anafananisha na mfumo wa utawala wa ufaransa. Pale unaweza pata jibu.

Jamaa ameelezea vitu vingi mno. Kwa mfano mtawala mpya anapoingia kwenye uongozi. Hali inakuwaje katika nchi. Pale kiongozi huyo anapoanza kuweka falsafa zake za kiuongozi ni kipi hutokea. Nini kifanyike.

principalities...
 
Heshima Mkuu, introvert .

Nakubaliana na wewe kabisa. Leaders are readers, if you fail to read you'll fail to lead. Hatuna viongozi wanaopenda kusoma. So far hata kuhamasisha watu wasome kwa aidha kuonekana katika maktaba zetu au hata mashuleni nayo hakuna.

Kiongozi hupendi kusoma. Sasa utaweza vipi kusoma Mkataba wa kurasa 250 kama si kuishia kupekua pekua na hatimaye kutuingiza utumwani kama kina Mangungo wa Msovero?.

Hivi kiongozi haoni clarity ya kwenda Maktaba kujisomea?. Mbona Mwalimu alipenda kusoma?. Iweje sie tusipende kusoma?.

Ukienda Maktaba Kuu ya Taifa utacheka. Kuna vitabu vya ajabu ajabu sielewi. Watu wameiba vitabu mule na hakuna anayejali. Nani anapenda kusoma?. Kuongozwa na watu wasiopenda watu wasome ni hatari sana kuliko kuwaongoza watu wasiopenda kusoma.

Bado nafanya tafiti za kina ya kuwa ni Taifa gani/lipi limeweza kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja zote za maisha pasina watu wake kupenda kujifunza, kusaili, kudodosa na kadhalika ila bado jitihada zangu hazifui dafu. Gharama ya kuwa na Taifa la Mazuzu ni kubwa sana ukilinganisha na gharama ya kujenga Maktaba ili watu wajisomee.

Heshima kwako sana!

Umeandika mambo ya msingi sana.

Tatizo letu kubwa ni elimu. Elimu ya darasani ni mbovu na elimu ya kawaida tu ya general knowledge ni hovyo kupindukia. Hii ni kwa sababu watu hawajisomei vitabu na pia watu hawajasafiri kupata exposure (Ujamaa 101, passport kibali kitoke Ikulu).

Kujisomea vitabu kunaongeza maarifa na hata kujua jinsi ya kudeal na mambo fulani. Sasa unapokuwa na kiongozi na taifa la watu ambao hawajisomei ndo unaona watu wanajiamulia mambo kienyeji tu na shangwe kibao.

Wenzetu unakuta kiongozi anahojiwa anaulizwa ni vitabu gani mwaka huu unashauri watu wavisome? Anajibu vitabu vizuri kabisa, latest publications.

Sasa hapa imagine JPM na Cabinet yake (ukitoa Makamba na Mahiga) wakiulizwa swali kama hilo watajibu nini?

Una mawaziri, wakurugenzi, mameneja ambao hawasomi na wala hata hawana subscriptions to newspapers muhimu dunia hii. Lakini ndiyo decision makers. Unabaki unacheka tu.

Wengi wa maprofessa wetu ukitoa fani zao, nje ya hapo hawajui kitu. Aibu. Na sasa wanapewa mavyeo kwa imani kwamba professa anajua kila kitu bila kutambua academicians are not industrialists.

Ukirudi kwa wanasiasa wetu ukiangalia picha za majumba yao ya "kifahari" (talk of bad taste) unaona liTV likubwa sebuleni na makochi yanangaa. Huoni kitabu hata kimoja. Na wananchi wanashangilia "muheshimiwa ana bonge la nyumba".

Ukija kwenye maktaba zetu ndiyo unatamani ulie kabisa. Ni vituko. Vitabu ni vya zamani (vingi vikiwa falsafa za Karl Marx). Wenzetu ukiingia maktaba zao unapata aina karibu zote za vitabu. Ukienda vyuo vyao unaona kabisa wapo serious na elimu.

Viongozi wetu wakisafiri kwenda nje ni kufanya shopping na vimada. Hatembelei vyuo na maktaba kujifunza elimu inavyotolewa huko. Sababu hizo mtu anajenga majengo mawili matatu anaiita ni shule/chuo.

Tupo miaka kama 500 nyuma.
 
I'm speechless, introvert .

Nimeona niache unazi wa ku-quote uzi mrefu (kupunguza kujaza servers), rejea hii ni kwa ajili ya comment hapo Juu.

Nikupongeze kwa uandishi makini wenye kuzingatia weledi kwa dhana ya kimantiki. Kujifunza daima ndiyo nidhamu ya kiakili, na nidhamu kwa lugha rahisi yamaanisha kujifunza. Tunavaa mabegi ya gharama sana migongoni, tatizo si kuvaa. Tatizo ni je kuna nini humo ndani?.

Kama vile Walter Russel wa Marikani Kaskazini, mwanamaono, mvumbuzi na msanii alivyopata kusema kuwa "Udunya ni maradhi ya kujitakia, kipaji ni kujifadhili". Katika lugha yake akimaanisha "Mediocrity is self inflicted, genius is self bestowed".

Haya mambo ya kutokuwa na kiu ya kujifunza ni ya kujikakia. Tuseme mathalani, mbona mtoto akipatwa na maradhi ya mwili tunafanya juu chini ili apone?, iweje mtoto huyu huyu akiwa hovyo (kumradhi) kichwani hatufanyi juu chini kumsaidia?.

Mtu asiye na mwongozo na asiyefunzwa, maumbile yake kisilika hufanana na mnyama wa porini. Anaweza kuwa mbogo au dubu.

Kasumba, itikadi ama msimamo mkali wowote ule, aidha wa dini moja au nyingine, dhehebu moja hadi lingine, fasheni moja hadi nyingine, tabia moja hadi nyingine, ainisho ya maisha moja hadi nyingine na kadhalika si fahari..Ni uduni na upeo wa kujitakia.

Dunia yote, watu wake, tamaduni yote na Jamii yote ni fahari za utu, mwangaza na fanaka kujaaliwa kheri na kweli moja iliyo ni uzima.

Mheshimiwa Zitto pia anapenda kusoma. Lakini sikuwahi kumuona akihamasisha watu wapende kusoma. Tatizo ni nini?. Au wakituhamasisha tutakuwa changamoto kwao?.

Hebu muone Zito Kabwe,
TheVibe: Zitto ashare vitabu 31 alivyosoma mwaka 2012!!
Vitabu alivyosoma Zitto Kabwe mwaka 2014 - Raizoni Blog http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/orodha-ya-vitabu-alivyosoma-zitto-kabwe-mwaka-2016

Vipi Mh Rais walau angekuwa anafanya hivi?, Mawaziri, Wakurugenzi, Wabunge, Wakuu wa Wilaya/Mikoa, Madiwani, Baba, Mama na kadhalika?. Je tusingepiga hatua?.

Tunasoma kwa lugha za kigeni halafu tunaiita Elimu?. Tunashiriki mashindano ya U-miss na Big brother halafu tunachekelea kama wanazi. Hatufuatilii vitu vya maana katika vyombo vyetu vya uongo (Si vyombo vya habari). Hatumfuatilii aliyeshinda tuzo ya Amani ya Nobel, Hatufahamu Jina la mwanafunzi aliyepata maksi za Juu katika mtihani wa darasa la saba, kidato cha nn, cha sita na kadhalika.

Tunamfuatilia aliyeshinda Miss world kama vichaa, Big brother, Music awards nk. Nadhani tunatengenezewa namna ya kufikiri. Tufkiri wenyewe. Ndiyo msingi wa mtu.

Bob Nesta Marley anakuambia "Emancipate yourself from mental slavery, non but ourself can free our mind". Can we just emancipate our child mindset, our mind so far?. If yes, lets try.

Ipo haja ya kuanzisha midahalo ya kuwavua mamilioni ya Watanzania wanaoogelea kwenye ' povu la ujinga'. Nani atawasaidia kuwavua kutoka kwenye povu hili la ujinga?. Nadhani hili jukumu letu sote si la mtu mmoja, ni jukumu la jamii nzima.

Hekima Ni Uhuru, Uhuru ni Hekima.
 
Doh. Hiki kitabu hujakisoma vizuri mkuu. Hata kama ulikisoma basi ulisoma principalities chache sana.

Mfumo wa utawala kipindi cha machiavelli na sasa haujabadilika sana. Angalia alipokuwa anaelezea mfumo wa kutawala nchi ya kituruki na alipokuwa anafananisha na mfumo wa utawala wa ufaransa. Pale unaweza pata jibu.

Jamaa ameelezea vitu vingi mno. Kwa mfano mtawala mpya anapoingia kwenye uongozi. Hali inakuwaje katika nchi. Pale kiongozi huyo anapoanza kuweka falsafa zake za kiuongozi ni kipi hutokea. Nini kifanyike.

principalities...
Heshima Mkuu.

Huhitajiki kutumia kanuni za ki-paithagoras au Gallileo kumfahamu kiongozi mwenye kusoma vitabu. Hajifichi, ni kama pembe ya ng'ombe.

Hatuna viongozi wasomi wa vitabu, hatuna viongozi-tuna watawala. Hiko kitabu kipo poa mno. Kama kitakuwa kibovu, basi msomaji ndiye mbovu.

Rais anasema Katika serikali yangu kuna viongozi wapumbavu?, serious?. Sasa sikia hii, Katika The Prince, ,Machiaveli anakuambia kuwa "Ukiona Mawaziri ni wabovu, Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya/mikoa na kadhalika ujue tatizo si wao. Tatizo ni la Rais aliyewateua". Je Rais kasoma kitabu hiko?. Usiniambie jibu.

Kwa paragrafu hapo juu, Iweje Rais ajikaange kwa kusema ana Mawaziri wapumbavu?. Waziri mpumbavu anapatikana vipi pasina kuchaguliwa na Rais ....

Hekima ni Uhuru, Uhuru ni Hekima.
 
Back
Top Bottom