Nina ubunifu mkubwa wa vipindi bora vya TV, natafuta mtu mwenye mtaji tushirikiane

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Pengine hujui biashara hii lakini sasa pokea hili toka kwangu kuwa inalipa sana! ilimradi program iliyoandaliwa iwe inagusa hisia za watu, na mara nyingi hili hutokea pale ubunifu unapokaa mahali pake tu!
kusema kweli hapa nchini kwetu bado tuna uhaba wa vipindi bora vyenye kuelimisha na kuburudisha jamii.

Nasema hivyo si kwamba vipindi havipo kabisa , hapana, maana vipindi vya kawaida vimejaa tele katika kila television station kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Sio siri wewe pia ni shahidi, ni mara ngapi umezima tv yako kwa kukosa kabisa kitu chenye mvuto wa kutazama?
Baya zaidi ni pale wote wanapofananisha vipindi vyao. Mimi nilipoona hivyo miaka michache iliyopita niliitambua hiyo ni fursa na nikaifanyia kazi.

Shida yetu kubwa katika hili si wataalamu tu la, isipokuwa tuna tatizo kubwa la ubunifu. Hii ni kwa sababu ubunifu ni kipaji, ndiyo maana si kila mtu anaweza kuwa mbunifu mahiri, hata hivyo ubunifu bila pesa ni sawa na bunduki bila risasi.

Ndiyo maana mimi baada ya kubuni vipindi bora vipatavyo 30 vya Tv, sasa ninaona ni muhimu nitafute mdau wa kibiashara mwenye mtaji ili tuanze biashara kwa kasi.

Kwa upande wa wadhamini wapo tele kwa lengo la kujitangaza kibiashara kupitia vipindi bomba. Ingawa no kweli pia hutoa pesa pale kipindi kinapokuwa tayari kimeanza, ndiyo maana pesa ya kuanzia ni muhimu mno kwetu.

Hakuna ubabaishaji mahali hapa, la muhimu ni mikataba ya kisheria inayoendana haki miriki ya wamiriki.
Usitegemee kunidhurumu wala mimi sitegemei kukudhurumu, maana haya ni mambo ya kisheria mno!

Maono yangu siku za usoni Mungu akipenda ni umiriki binafsi waTelevision Station , njoo na yako tuunganishe nguvu, kwa kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Kwa aliye tayari kwa mazungumzo awasiliane nami kwa namba hii 0786003770.
 
Ipo tofauti ya gharama kwa kipindi na kipindi ndiyo maana Mawasiliano ni muhimu kwa Maelezo zaidi.
 
Unaposema Gharama unamaanisha nini..kununulia Equipment au Pesa kwaajili ya Ofisi...ikitokea MTU ana Office na Vifaa vyakufanyia kazi utakubaliana nae?
 
Fanya weka Youtube kama vizuri utaonekana tu. Ukivutia watu Youtube mitaa ikakuelewa hata wenye vituo vya Tv watakukimbilia
 
hujasema wewe unakitu gani na unahitaji kitu gani, kujua kutengeneza kipindi kuna aspect nyingi, je wewe ni producer,director,editor ama nani? funguka zaidi na hili ndio tatizo kubwa la wajasiriamali wa tz, wanavitu kichwani lakini kuvipresent vikaeleweka inakua issue. tuanzie hapo ili tuone kama tunafit ama la...asante sana. ndg Mchokoo
 
Samahani kwa kuchelewa kujibu.

Nilishasema kuwa shida si hao wataalamu, sijui director au producer nk, hapana, kwani hao wamejaa tele.
Kumbukeni uandaaji wa vipindi ni tofauti na ule uandaaji wa music, ambapo mtunzi akileta kipindi wimbo mbovu ni rahisi kuufanya uwe bora

Ni vizuri tukafahamu kuwa mara nyingi hawa wataalamu wa hapa nchini huwa ni watu wakupokea kipindi kilichobuniwa tayari; na wao huwa ni washauri katika kuboresha kidogo ile idea.
Nimeshasema mimi ni mbunifu wa vipindi ambapo nikishamaliza kubuni huiweka ile idea katika mfumo wa kisanaa, kwa namna ile vitakavyorandana au kuendana.
Baadaye ndipo linapokuja suala la production ambako huko ndiko umaliziaji wa kurekodi hufanyika sambamba na hao wataalamu.

Kimsingi nilichonacho mimi tayari ni ubunifu na vipindi ambavyo vimeshasajiriwa tayari na vile ambavyo bado.

Elewa mpaka umesajiri kipindi huwa umekiandaa tayari, na hiyo yote ni pesa imetumika.
 
Maswali machache:
  1. Unaitaji mtaji wa shilling ngapi na unata huo mtaji kuufanyia nini?
  2. Jee umewai tengeneza kipindi ambacho kimeuza kabla ya hivi? Jee ni kwenye TV gani?
  3. Tatu kama una taaluma ya kutengeneza best quality kwa nini hujapartner na TV wao wakakupa airtime wewe ukaweka human capital kisha mkashare mauzo?
  4. Katika hivyo vipindi vyako jee umefanya proof of concept? wapi? na Matokeo yapoje?
Ni hayo kuanzia.

Mtanganyika
 
Maswali machache:
  1. Unaitaji mtaji wa shilling ngapi na unata huo mtaji kuufanyia nini?
  2. Jee umewai tengeneza kipindi ambacho kimeuza kabla ya hivi? Jee ni kwenye TV gani?
  3. Tatu kama una taaluma ya kutengeneza best quality kwa nini hujapartner na TV wao wakakupa airtime wewe ukaweka human capital kisha mkashare mauzo?
  4. Katika hivyo vipindi vyako jee umefanya proof of concept? wapi? na Matokeo yapoje?
Ni hayo kuanzia.

Mtanganyika
Akijibu haya nampigia
 
Back
Top Bottom